Muongozo wa kununua vifaa vinavyotumia processor za intel

Kiongozi kwa laptop yenye processor
Intel(R)cor(TM) i5-5200U @2.2Ghz
Kwa sasa ina Ram 4GB lakini ina nafasi ya kuweka ram 2 nikiongezea Ram 8GB
Vp perfomance yake itakuwa nzuri au inaweza kuzingua
 
Kiongozi kwa laptop yenye processor
Intel(R)cor(TM) i5-5200U @2.2Ghz
Kwa sasa ina Ram 4GB lakini ina nafasi ya kuweka ram 2 nikiongezea Ram 8GB
Vp perfomance yake itakuwa nzuri au inaweza kuzingua
Ongeza mkuu, ddr3 bei rahisi na itasaidia kukupa perfomance.

Pia kama haina ssd weka.
 
Chief-Mkwawa naomba unipe utofauti wa processors za AMD Ryzen na Intel Core i series.

Utofauti kwenye performance, battery life etc.

Na unipe equivalents zake mfano, core i7, core i5, core i9 ni sawa na Ryzen ipi?
 
Chief-Mkwawa naomba unipe utofauti wa processors za AMD Ryzen na Intel Core i series.

Utofauti kwenye performance, battery life etc.

Na unipe equivalents zake mfano, core i7, core i5, core i9 ni sawa na Ryzen ipi?
Mkuu Ryzen ni mpya mpya za Karibuni kama ilivyo intel i3, i5, i7 na i9 zenyewe pia zimegawanyika kwa Ryzen 3, 5, 7 na 9, hivyo inakuwa rahisi kuzi compare na intel.

Kama ilivyo intel Ryzen pia inakuwa na generation zake kuna Zen, zen+, zen2, zen3 na zen 4.


naweza kuzigawanya kama makundi matatu.

Ryzen za mwanzo kabisa 1xxx, 2xxx, 3xxx na 4xxx hizi zina base na zen mpaka zen 3 ni nzuri ila sio za kisasa na latest kabisa zinafanya mambo ya kawaida na comparison yake ni kama gen ya 8 mpaka ya 10 intel.

Ryzen zinazobase na zen 3, hizi cpu zake zinaanziwa na 5 kama Ryzen 5 5500u, kwenye Zen 3 ndio Amd alimpiku intel kwenye mambo mengi hasa ukaaji chaji, hapa ndio unapata Laptop zinazokaa na chaji masaa kuanzia 10, kwa value hizi zipo vizuri. Baadae Amd walitoa revision ya Zen 3 ijulikanayo kama Rembrandt cpu zake zinaanziwa na 6xxx kama 6600u na 6800u, hizi zilikuwa na Gpu ya ndani ijulikanayo kama Rdna2, ukiwa na Cpu hii huhitaji tena gpa ya nje ya Nvidia ama radeon maana inacheza games hadi 1080p na vitu kama basic video editing na production unafanya bila matatizo.



Ryzen za kisasa za Zen 4 hizi zinaanzia na 7xxx (sio ryzen 7xxx zote ni zen 4) hapa Amd alimfikia intel kwa perfomance huku akiendelea kuwa na cpu zinazokula umeme kidogo sana. Hizi ndio mpya na za kisasa zinaanza kusambaa mtaani ila si rafiki wa pesa, bei ndefu. Pia Zen 4 inakuja na Gpu za rdna3 ambazo ni nzuri zaidi.

Kuelezea mabano hapo juu Amd alipozindua cpu za 7xxx amemix architecture kuna Zen 2, zen 3 na zen 4 hivyo wajinga waliwao, ukijichanganya tu unauziwa kimeo, wadau wengi wamelalamika mtandaoni, mpaka nikae chini nizichambue naweza leta uzi kamili wa Ryzen.

Amd vs Intel.
Kwa sasa mkuu maeneo pekee ambayo intel yupo competitive ni
1. Low end Cpu kama i3 hadi i5 hivi ni bora zaidi kuliko ryzen na unazipata bei rahisi sometime chini ya laki 7 huko ughaibuni.
2. Perfomance ya single core bado intel yupo vizuri hasa software za kiofisi kama Excel
3. Encoding na decoding za video kwa kutumia Quicksync.

Amd Ryzen yupo vizuri kwenye
1. Ukaaji chaji kiujumla cpu zake zinakula umeme kidogo
2. Gpu zake ni kali sana hasa Rdna2 kupanda
3. Multithreaded perfomance ni kubwa sababu zinakuja na Core nyingi hasa Ryzen 7 unapata core 8 na thread 16.

Hivyo mkuu hapo utaangalia matumizi yako, na siku hizi zipo mini pc kama $400 barebone na around $550 configured zenye Ryzen 7 6800u
 
Nasubiri huo uzi wa Ryzen
 
Mkuu Chief-Mkwawa, hii mashine inayo shemu mbili ambazo hazina ram yaani ziko empty. Lakini nikiangalia kwenye setting inaonyesha kuna ram ya 4GB. hii Ram inaweza kuwa upande gani wa hii mashine?
2. niktaka kuongeza ram naweza ongeza mpaka ngapi? kwasababu nina mpango wa kuweka ssd nitoe hdd
3. alafu kuna ki ssd nafikiri ni sata lakini ni kile kifupi kina gb 24 tu. naweza kukitoa na kuweka kingine chenye uwezo mkubwa zaid?

mashine ni HP EliteBook 8570w
 

Attachments

  • Capture 2.JPG
    45.8 KB · Views: 23
  • Capture.JPG
    57.4 KB · Views: 21
Mkuu Chief-Mkwawa, hii mashine inayo shemu mbili ambazo hazina ram yaani ziko empty. Lakini nikiangalia kwenye setting inaonyesha kuna ram ya 4GB. hii Ram inaweza kuwa upande gani wa hii mashine?
Laptop siku hizi zinakuja na intergrated ram ambazo zimechomelewa halafu wanakuachia slot za kuongeza mwenyewe.
2. niktaka kuongeza ram naweza ongeza mpaka ngapi? kwasababu nina mpango wa kuweka ssd nitoe hdd
Ingia task manager then perfomance then kwenye memory niekee screenshot hapa nikuchekie ram.
3. alafu kuna ki ssd nafikiri ni sata lakini ni kile kifupi kina gb 24 tu. naweza kukitoa na kuweka kingine chenye uwezo mkubwa zaid?

mashine ni HP EliteBook 8570w
Ndio as long as hio ssd mpya ni sata unaweza weka hata 4TB.
 
Hii hapa nimekuwekea mkuu.
 

Attachments

  • Capture3.JPG
    89 KB · Views: 20
Pia nimekutumia picha mbili.
1. moja ni hzo sehemu za kuweka Ram japo sijajua ni aina gani ya ram naweka na mwisho iwe ukubwa gani?
2. picha ya pili ni ssd lakini ina gb 24 tu, japo kwenye pc haionekani kama kuna hiyo space ya 24GB
 

Attachments

  • 1.jpg
    94 KB · Views: 11
  • 2.jpg
    75.6 KB · Views: 23
Pia nimekutumia picha mbili.
1. moja ni hzo sehemu za kuweka Ram japo sijajua ni aina gani ya ram naweka na mwisho iwe ukubwa gani?
2. picha ya pili ni ssd lakini ina gb 24 tu, japo kwenye pc haionekani kama kuna hiyo space ya 24GB
Hii mkuu ni msata ssd ila kwa kuangalia kwa macho sio 2280 ambazo ni common na ndefu. Pia kuna utofauti baina ya Sata na msata.

Hivyo wakati wa kununua kuwa makini ama vyema uende na machine muuzaji afanye installation mwenyewe huku unamuona.

Ssd ambazo ni common zinatumika sana ni m.2 na Sata ya kawaida. ila Vyema utafute hio msata ili port ya kawaida ya Sata iendelee kukaa hdd.
 
hii hapa mkuu upande wa memory
Mkuu sababu hii ni workstation ina slot 4, kuna laptop ram zinakaa juu na chini, hapo hapo pa kueka ram angalia kama kinabinuka na kuna slot nyengine mbili kwa chini.

Sababu inatumia ddr3 na ddr3 siku hizi ni rahisi unaweza ukaweka 4gbx4 ukitafuta vizuri haiwezi zidi 45,000
 
Asante mkuu, nimegoogle inaonekana ram nyingine ipo kwa ndani mpaka utoe keyboard ndio upate sehemu nyingine iliyo na ram. lakini katika hizo space mbili zilizobaki nitaweka 4gb*2
 
Wakuu mwenye uhitaji wa graphics card iyo hapo
Rx 550 2gb
Gddr5
Bado Iko vizuri sana now days Sina kazi nayo
Bei ya offer 150,000
Location kigamboni
0688823704
 
Nataka nijitose hapa Mkuu ushauri, siyo touch!


HP EliteBook 840 G6 8th gen slim laptop price 750,000/= Free sleave bag👜


BASIC DETAILS
brand name: HP elitebook 840 G6 core i5
Generation type: 8th generation.
Processor :inter core i5-8350U CPU @1.9GHz (8CPUs)
max turbo: 3.9Ghz

Memory : 8gb DDR 4-1600(RAM)
Storage :256GB

DISPLAY DETAILS
screen size :14.0 inches wide
Resolution: *1366 full HD panel
Graphics type=Inter(R) graphics 620
Total graphics=4164 inter graphics
video memory=128 (dedicated)

SOUND CARD :BANG & OLUFSEN

FEATURES
backlight keyboard (inawaka taaa)
finger print ✅
bluetooth✅
TYPE c port✅
HDMI port
Ethernet
Web cam

COLOUR:sliver
Condition:refublished clean as new

OPERATING systeam :window 10 pro
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…