johrobby
JF-Expert Member
- Jan 7, 2017
- 1,062
- 2,230
shukhran mkuu ngoja nitajarb kufanya ivoJuu ya processor, mahala ambapo processor na cooling system zinakutana. Cheki youtube video kibao. Ni kama dawa ya mswaki hivi.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
shukhran mkuu ngoja nitajarb kufanya ivoJuu ya processor, mahala ambapo processor na cooling system zinakutana. Cheki youtube video kibao. Ni kama dawa ya mswaki hivi.
Kiongozi kwa laptop yenye processorComputer nyingi tunazonunua huwa zinatumia processor za intel au amd, lakini ni intel ambaye ametawala sana kushinda amd kwenye computer zetu. Leo nimeamua niandike uzi huu kuhusu hizi processor za intel na namna ya kuzichagua ili kuwasaidia watu wanapotaka kununua laptop/desktop mpya wafanye maamuzi sahihi.
Processor ni nini?
Labda utakuwa unajiuliza kwa nini ukitaka kununua laptop mpya unatakiwa uangalie processor? Nini cha muhimu kuhusu hii processor?
-Kwa lugha rahisi processor ni kifaa ndani ya computer yako kinachobeba maagizo ya program za computer. Maagizo hayo yanaweza kuwa ya kimahesabu, kimantiki, maagizo yanayoingia kwenye computer na yanayotoka.
-jinsi processor inavyokuwa na speed kubwa ndio jinsi maagizo yatakavyofanywa haraka na ndio jinsi program za computer zitakavyofanya kazi upesi.
![]()
Familia ya processor za intel
Intel wana processor za aina nyingi na ni ngumu kuzitaja kwa pamoja, ila wameturahisishia kwa kuzipanga processor zao kwenye familia. Na hii ndio familia yao.
1. Atom processor- processor hizi hutumika kwenye vimini laptop na tablet ni ndogo kiumbo ndio maana hata vifaa vyake ni vidogo, processor hizi hazina nguvu sana na vifaa vyake hukaa sana na chaji.
2. Celeron processor- Haina tofauti sana na atom ila hii ina afadhali kidogo. Inatumika kwenye vifaa vikubwa kuliko atom kama vile laptop kubwa na desktop
3. Pentium- hii ina speed kuliko celeron na atom pia inatumika kwenye vifaa vikubwa.
4. Core 2 duo- hii ni maarufu kwa perfomance yake ya multitasking, inauwezo wakufanya mambo mengi kwa wakati mmoja ila nyingi ni za kizamani.
5. Core i3- hii ni processor latest za intel ni dual core lakini core zake zina perfomance kubwa na pia inakuwa na thread 2 kwenye kila core, ni nzuri kwa wanaotaka perfomance kubwa kwa bei rahisi.
6. Core i5- ya laptop ni dualcore na ya desktop ni quadcore isiyokuwa na thread, software nyingi kubwa duniani zimekuwa optimized kutumia core kama za i5, ni nzuri sana kwa watu wanaotumia software zinazodemand perfomance lakini hawafanyi multitasking.
7.Core i7- hii inakuwa na quadcore processor na thread 8 kwenye desktop na pia inaweza kuwa dualcore kwenye laptop. Hii ndio processor nzuri zaidi kwa watu wa kawaida na inafanya multitasking hata kama software zinademand sana.
8. Xeon- hii ndio processor yenye speed zaidi kwenye processor za intel lakini imekuwa designed kufanya kazi kwenye computer kubwa kama vile server. Unapohost website processor kama hii ndio inayoprocess webpages.
Generation ya processor(muhimu)
Ni muhimu sana kujua processor inatokea generation ipi kuna processor zenye i7 ya 2010 ambazo zipo slow vibaya mno, na pia kuna uwezekano i3 kuipita i7 kwenye perfomance kama zinatoka generation tofauti. Hivyo eneo hili inabidi uwe makini kuepuka kuuziwa mbuzi kwenye gunia. Hivyo unaponunua laptop/desktop ni lazima ujue ipo generation gani la sivyo upo hatarini na hivi ndio namna ya kujua.
- Processor yenye namba inayoanziwa na elfu nne ni fourth generation(4xxx)
Mfano Intel i3-4130.
- Processor yenye namba inayoanziwa na elfu tatu ni third generation (3xxx)
Mfano i3-3130.
- Processor inayoanziwa na elfu mbili ni second generation(2xxx)
Mfano i3-2140
Sishauri kabisa kununua processor ya first generation, mtu unatakiwa atleast ununue ya second generation na pia bei inatakiwa iwe ndogo kwa hii second compare na third/fourth.
Processor ndogo kama atom na celeron zina generation zake ambazo ni
-clover trail
-bay trail
Processor za zamani za atom zilikuwa mbaya sana na zipo slow ila baytrail ikaja kuzipa nguvu na kuzifanya ziwe na perfomance kubwa, hivyo kama unataka kifaa cha atom/celeron make sure processor yake iwe inatoka generation ya baytrail.
Herufi za mbele ya processor(muhimu)
Kama umechunguza mbele ya processor kunakuwa na herufi mbali mbali hizi pia ni muhimu sana kuzijua kwani usipozizingatia unaweza kujuta.
Mfano processor inaweza kuitwa i5-4000m au i5-4000u au i5-4000y je nini kinatofautisha hizi processor?
1. Herufi kwenye processor za desktop.
Bila herufi – hii inakuwa na speed halisi ya processor mfano i7-4770
K- herufi hii inamaanisha processor ipo unlocked na unaweza kui over clock na kuongeza speeed. Processor yenye 3.5ghz unaweza kui overclock ikafika 4ghz. Jina lake linakuwa mfumo huu i7-4770K. ni nzuri sana kwa wanaocheza magame na kufanya rendering.
R- herufi hii inamaanisha processor hii ni ndogo sana na inaweza kutumika kwenye videsktop vyenye umbo dogo hali ya kuwa ina graphic kubwa kama iris pro. Jina lake linakuwa mfumo huu i7-4770R hii ni nzuri kwa wale wenye ofisi ambazo ni safi hawataki mawaya mengi na desktop kubwa kukaa kwenye meza. angalia picha hapo chini uone desktop ndogo.
![]()
S- herufi hii inamaanisha hiyo proceesor wame optimize perfomance mara nyingi wanai underclock kuzuia processor kupata joto sana. Mfano i7-4770 ina 3.4ghz lakini i7-4770S ina 3.1ghz tu, ina maana hapa wamepunguza 300mhz kutoka stock kuja S.
T- herufi hii inamaanisha processor inatumia power ndogo, kwa wale wenzangu wanaotumia luku kama unataka desktop isiokula umeme basi hii ndio yenyewe ila perfomance nayo itapungua kidogo. Mfano wa jina ni i7-4770T
2. Herufi mbele ya processor za laptop(mobile)
Tumeshaona herufi mbele ya desktop, sasa hivi tuangalie herufi mbele ya processor za laptop ambazo pia zinaweza kutumika kwenye home theatre pc (htpc) au wengine wanaita mini desktop.
M- herufi hii inamaanisha hio processor ni mobile, ndio herufi common kwenye processor za laptop mfano i5-4000M
U- herufi hii inamaanisha processor ya laptop inatumia power ndogo hizi processor zinatumika sana kwenye vilaptop vyembamba (ultrabook). Kwa sababu zinakaa na chaji kutokana na kutumia power ndogo, perfomance yake nayo pia ni ndogo. Mfano i5 4250U
Y- hii ni ultra low power yaani inakula umeme mdogo kushinda hata U lakini vile vile perfomance inazidi kushuka nayo mfano i7-4610Y
HQ- herufi hii inamaanisha high perfomance, zinauzwa bei ghali sana na power yake inashindana na desktop. Usije ukajaribu kuieka kwenye mapaja laptop ya design hii maana zinashika moto upesi sana kutokana na quality ya processor. Ni nzuri kwa wale wanaopenda kucheza game, kutumia software kubwa wakiwa kitandani. Mfano ni i7-4700HQ
MQ- herufi hii inamaanisha hio procesor ni quad core. Kama umesoma vizuri juu i5 na i7 za desktop ni quadcore lakini za laptop ni dualcore, hivi processor hii inamaanisha unaweza tumia quadcore kwenye laptop yako kama unataka mfano i7-4900MQ
MX- herufi hii inamaanisha ni xtreme edition, processor hii unaweza kui over clock kama vile K series ya desktop na ina perfomance kubwa sanaaa, ila kuwa makini na mapaja tu.
Mfano i7-4940MX
Huu ndio muongozo wa kununua processor za intel, kama kuna sehemu hujapaelewa unaweza kuuliza nitaelezea zaidi.
Ongeza mkuu, ddr3 bei rahisi na itasaidia kukupa perfomance.Kiongozi kwa laptop yenye processor
Intel(R)cor(TM) i5-5200U @2.2Ghz
Kwa sasa ina Ram 4GB lakini ina nafasi ya kuweka ram 2 nikiongezea Ram 8GB
Vp perfomance yake itakuwa nzuri au inaweza kuzingua
Hapo ddr3 pamoja na ssd sinakuelewa mkuuOngeza mkuu, ddr3 bei rahisi na itasaidia kukupa perfomance.
Pia kama haina ssd weka.
Ddr3 aina ya ram ambayo laptop yako inakubali,Hapo ddr3 pamoja na ssd sinakuelewa mkuu
Shukrani mkuu hapo nimekupata ngoja niifanyie kazi hiliDdr3 aina ya ram ambayo laptop yako inakubali,
Ssd ni storage yenye speed kushinda HDD.
Mkuu Ryzen ni mpya mpya za Karibuni kama ilivyo intel i3, i5, i7 na i9 zenyewe pia zimegawanyika kwa Ryzen 3, 5, 7 na 9, hivyo inakuwa rahisi kuzi compare na intel.Chief-Mkwawa naomba unipe utofauti wa processors za AMD Ryzen na Intel Core i series.
Utofauti kwenye performance, battery life etc.
Na unipe equivalents zake mfano, core i7, core i5, core i9 ni sawa na Ryzen ipi?
Nasubiri huo uzi wa RyzenMkuu Ryzen ni mpya mpya za Karibuni kama ilivyo intel i3, i5, i7 na i9 zenyewe pia zimegawanyika kwa Ryzen 3, 5, 7 na 9, hivyo inakuwa rahisi kuzi compare na intel.
Kama ilivyo intel Ryzen pia inakuwa na generation zake kuna Zen, zen+, zen2, zen3 na zen 4.
naweza kuzigawanya kama makundi matatu.
Ryzen za mwanzo kabisa 1xxx, 2xxx, 3xxx na 4xxx hizi zina base na zen mpaka zen 3 ni nzuri ila sio za kisasa na latest kabisa zinafanya mambo ya kawaida na comparison yake ni kama gen ya 8 mpaka ya 10 intel.
Ryzen zinazobase na zen 3, hizi cpu zake zinaanziwa na 5 kama Ryzen 5 5500u, kwenye Zen 3 ndio Amd alimpiku intel kwenye mambo mengi hasa ukaaji chaji, hapa ndio unapata Laptop zinazokaa na chaji masaa kuanzia 10, kwa value hizi zipo vizuri. Baadae Amd walitoa revision ya Zen 3 ijulikanayo kama Rembrandt cpu zake zinaanziwa na 6xxx kama 6600u na 6800u, hizi zilikuwa na Gpu ya ndani ijulikanayo kama Rdna2, ukiwa na Cpu hii huhitaji tena gpa ya nje ya Nvidia ama radeon maana inacheza games hadi 1080p na vitu kama basic video editing na production unafanya bila matatizo.
Ryzen za kisasa za Zen 4 hizi zinaanzia na 7xxx (sio ryzen 7xxx zote ni zen 4) hapa Amd alimfikia intel kwa perfomance huku akiendelea kuwa na cpu zinazokula umeme kidogo sana. Hizi ndio mpya na za kisasa zinaanza kusambaa mtaani ila si rafiki wa pesa, bei ndefu. Pia Zen 4 inakuja na Gpu za rdna3 ambazo ni nzuri zaidi.
Kuelezea mabano hapo juu Amd alipozindua cpu za 7xxx amemix architecture kuna Zen 2, zen 3 na zen 4 hivyo wajinga waliwao, ukijichanganya tu unauziwa kimeo, wadau wengi wamelalamika mtandaoni, mpaka nikae chini nizichambue naweza leta uzi kamili wa Ryzen.
Amd vs Intel.
Kwa sasa mkuu maeneo pekee ambayo intel yupo competitive ni
1. Low end Cpu kama i3 hadi i5 hivi ni bora zaidi kuliko ryzen na unazipata bei rahisi sometime chini ya laki 7 huko ughaibuni.
2. Perfomance ya single core bado intel yupo vizuri hasa software za kiofisi kama Excel
3. Encoding na decoding za video kwa kutumia Quicksync.
Amd Ryzen yupo vizuri kwenye
1. Ukaaji chaji kiujumla cpu zake zinakula umeme kidogo
2. Gpu zake ni kali sana hasa Rdna2 kupanda
3. Multithreaded perfomance ni kubwa sababu zinakuja na Core nyingi hasa Ryzen 7 unapata core 8 na thread 16.
Hivyo mkuu hapo utaangalia matumizi yako, na siku hizi zipo mini pc kama $400 barebone na around $550 configured zenye Ryzen 7 6800u
Laptop siku hizi zinakuja na intergrated ram ambazo zimechomelewa halafu wanakuachia slot za kuongeza mwenyewe.Mkuu Chief-Mkwawa, hii mashine inayo shemu mbili ambazo hazina ram yaani ziko empty. Lakini nikiangalia kwenye setting inaonyesha kuna ram ya 4GB. hii Ram inaweza kuwa upande gani wa hii mashine?
Ingia task manager then perfomance then kwenye memory niekee screenshot hapa nikuchekie ram.2. niktaka kuongeza ram naweza ongeza mpaka ngapi? kwasababu nina mpango wa kuweka ssd nitoe hdd
Ndio as long as hio ssd mpya ni sata unaweza weka hata 4TB.3. alafu kuna ki ssd nafikiri ni sata lakini ni kile kifupi kina gb 24 tu. naweza kukitoa na kuweka kingine chenye uwezo mkubwa zaid?
mashine ni HP EliteBook 8570w
Hii hapa nimekuwekea mkuu.Laptop siku hizi zinakuja na intergrated ram ambazo zimechomelewa halafu wanakuachia slot za kuongeza mwenyewe.
Ingia task manager then perfomance then kwenye memory niekee screenshot hapa nikuchekie ram.
Ndio as long as hio ssd mpya ni sata unaweza weka hata 4TB.
Pia nimekutumia picha mbili.Laptop siku hizi zinakuja na intergrated ram ambazo zimechomelewa halafu wanakuachia slot za kuongeza mwenyewe.
Ingia task manager then perfomance then kwenye memory niekee screenshot hapa nikuchekie ram.
Ndio as long as hio ssd mpya ni sata unaweza weka hata 4TB.
Click hapo kwenye memory mkuu.Hii hapa nimekuwekea mkuu.
Hii mkuu ni msata ssd ila kwa kuangalia kwa macho sio 2280 ambazo ni common na ndefu. Pia kuna utofauti baina ya Sata na msata.Pia nimekutumia picha mbili.
1. moja ni hzo sehemu za kuweka Ram japo sijajua ni aina gani ya ram naweka na mwisho iwe ukubwa gani?
2. picha ya pili ni ssd lakini ina gb 24 tu, japo kwenye pc haionekani kama kuna hiyo space ya 24GB
hii hapa mkuu upande wa memoryClick hapo kwenye memory mkuu.
Mkuu sababu hii ni workstation ina slot 4, kuna laptop ram zinakaa juu na chini, hapo hapo pa kueka ram angalia kama kinabinuka na kuna slot nyengine mbili kwa chini.hii hapa mkuu upande wa memory
Asante mkuu, nimegoogle inaonekana ram nyingine ipo kwa ndani mpaka utoe keyboard ndio upate sehemu nyingine iliyo na ram. lakini katika hizo space mbili zilizobaki nitaweka 4gb*2Mkuu sababu hii ni workstation ina slot 4, kuna laptop ram zinakaa juu na chini, hapo hapo pa kueka ram angalia kama kinabinuka na kuna slot nyengine mbili kwa chini.
Sababu inatumia ddr3 na ddr3 siku hizi ni rahisi unaweza ukaweka 4gbx4 ukitafuta vizuri haiwezi zidi 45,000