Muongozo wa kununua vifaa vinavyotumia processor za intel

Muongozo wa kununua vifaa vinavyotumia processor za intel

Sata ssd inakubali bila shida hiyo. Ila kama mashine yako ni gen ya 10 itakuwa na slot ya m2 nvme ssd cheki kwanza. Yenyewe unakuwa unakapachila tu kàma ram.
Ni Gen ya 10 mkuu maana ile HDD naona inanisumbua nataka niitoe niweke SSD tu maana kila nikipiga window nikianza kutumia inaniletea hv au Black screen mara iji repair [emoji24][emoji24] ndio maana nataka kuagiza SSD
PXL_20230815_124054671.jpg
 
Kwahiyo ambayo natakiwa nichukue ni hii? Maana nataka niitoe HDD ya 1TB
Sata ssd inakubali bila shida hiyo. Ila kama mashine yako ni gen ya 10 itakuwa na slot ya m2 nvme ssd cheki kwanza. Yenyewe unakuwa unakapachila tu kàma ram.
Screenshot_20230816-192152.jpg
 
Leta model yake kwanza tuone kama inayo slot ya ssd.

Maana kuna zingine zina mpaka slot zaid ya moja.

Mfano yangu ina slot mbili.
Nahisi ipo hapo kaka, nisaidie niagize ipi ili nifanikishe ?
PXL_20230816_172102860.jpg
 
Naombeni mwongozo tafadhali, nahitaji kununua PC na nimekutana na hizi mbili tofauti, kwa kuzingatia ubora wa kila eneo, nichukue ipi;-

1. Dell Latitude 3420
Core i5 11th Generation
HDD 1TB
RAM 8GB DDR4
Processor 2.40GHz
NON-TOUCHSCREEN
Price: Around 800K


2. HP ELITEBOOK 840 G5
Core i7 8th Generation
SSD 512
RAM 16GB
Processor 2.1GHz
TOUCHSCREEN,
Price: Around 900K.


Ahsanteni sana.

CC: Chief-Mkwawa
 
Naombeni mwongozo tafadhali, nahitaji kununua PC na nimekutana na hizi mbili tofauti, kwa kuzingatia ubora wa kila eneo, nichukue ipi;-

1. Dell Latitude 3420
Core i5 11th Generation
HDD 1TB
RAM 8GB DDR4
Processor 2.40GHz
NON-TOUCHSCREEN
Price: Around 800K


2. HP ELITEBOOK 840 G5
Core i7 8th Generation
SSD 512
RAM 16GB
Processor 2.1GHz
TOUCHSCREEN,
Price: Around 900K.


Ahsanteni sana.

CC: Chief-Mkwawa
i5 11th gen nzuri mkuu, 11th gen japo ni i5 ina nguvu kushinda hio i7 8th gen na pia ina Gpu nzuri.

Hio laki inayobaki ongezea kidogo upgrade ram na ssd.
 
Computer nyingi tunazonunua huwa zinatumia processor za intel au amd, lakini ni intel ambaye ametawala sana kushinda amd kwenye computer zetu. Leo nimeamua niandike uzi huu kuhusu hizi processor za intel na namna ya kuzichagua ili kuwasaidia watu wanapotaka kununua laptop/desktop mpya wafanye maamuzi sahihi.

Processor ni nini?

Labda utakuwa unajiuliza kwa nini ukitaka kununua laptop mpya unatakiwa uangalie processor? Nini cha muhimu kuhusu hii processor?

-Kwa lugha rahisi processor ni kifaa ndani ya computer yako kinachobeba maagizo ya program za computer. Maagizo hayo yanaweza kuwa ya kimahesabu, kimantiki, maagizo yanayoingia kwenye computer na yanayotoka.

-jinsi processor inavyokuwa na speed kubwa ndio jinsi maagizo yatakavyofanywa haraka na ndio jinsi program za computer zitakavyofanya kazi upesi.
processor_01.jpg


Familia ya processor za intel

Intel wana processor za aina nyingi na ni ngumu kuzitaja kwa pamoja, ila wameturahisishia kwa kuzipanga processor zao kwenye familia. Na hii ndio familia yao.

1. Atom processor- processor hizi hutumika kwenye vimini laptop na tablet ni ndogo kiumbo ndio maana hata vifaa vyake ni vidogo, processor hizi hazina nguvu sana na vifaa vyake hukaa sana na chaji.

2. Celeron processor- Haina tofauti sana na atom ila hii ina afadhali kidogo. Inatumika kwenye vifaa vikubwa kuliko atom kama vile laptop kubwa na desktop

3. Pentium- hii ina speed kuliko celeron na atom pia inatumika kwenye vifaa vikubwa.

4. Core 2 duo- hii ni maarufu kwa perfomance yake ya multitasking, inauwezo wakufanya mambo mengi kwa wakati mmoja ila nyingi ni za kizamani.

5. Core i3- hii ni processor latest za intel ni dual core lakini core zake zina perfomance kubwa na pia inakuwa na thread 2 kwenye kila core, ni nzuri kwa wanaotaka perfomance kubwa kwa bei rahisi.

6. Core i5- ya laptop ni dualcore na ya desktop ni quadcore isiyokuwa na thread, software nyingi kubwa duniani zimekuwa optimized kutumia core kama za i5, ni nzuri sana kwa watu wanaotumia software zinazodemand perfomance lakini hawafanyi multitasking.

7.Core i7- hii inakuwa na quadcore processor na thread 8 kwenye desktop na pia inaweza kuwa dualcore kwenye laptop. Hii ndio processor nzuri zaidi kwa watu wa kawaida na inafanya multitasking hata kama software zinademand sana.

8. Xeon- hii ndio processor yenye speed zaidi kwenye processor za intel lakini imekuwa designed kufanya kazi kwenye computer kubwa kama vile server. Unapohost website processor kama hii ndio inayoprocess webpages.


Generation ya processor(muhimu)

Ni muhimu sana kujua processor inatokea generation ipi kuna processor zenye i7 ya 2010 ambazo zipo slow vibaya mno, na pia kuna uwezekano i3 kuipita i7 kwenye perfomance kama zinatoka generation tofauti. Hivyo eneo hili inabidi uwe makini kuepuka kuuziwa mbuzi kwenye gunia. Hivyo unaponunua laptop/desktop ni lazima ujue ipo generation gani la sivyo upo hatarini na hivi ndio namna ya kujua.

- Processor yenye namba inayoanziwa na elfu nne ni fourth generation(4xxx)
Mfano Intel i3-4130.

- Processor yenye namba inayoanziwa na elfu tatu ni third generation (3xxx)
Mfano i3-3130.

- Processor inayoanziwa na elfu mbili ni second generation(2xxx)
Mfano i3-2140

Sishauri kabisa kununua processor ya first generation, mtu unatakiwa atleast ununue ya second generation na pia bei inatakiwa iwe ndogo kwa hii second compare na third/fourth.

Processor ndogo kama atom na celeron zina generation zake ambazo ni
-clover trail
-bay trail

Processor za zamani za atom zilikuwa mbaya sana na zipo slow ila baytrail ikaja kuzipa nguvu na kuzifanya ziwe na perfomance kubwa, hivyo kama unataka kifaa cha atom/celeron make sure processor yake iwe inatoka generation ya baytrail.


Herufi za mbele ya processor(muhimu)

Kama umechunguza mbele ya processor kunakuwa na herufi mbali mbali hizi pia ni muhimu sana kuzijua kwani usipozizingatia unaweza kujuta.

Mfano processor inaweza kuitwa i5-4000m au i5-4000u au i5-4000y je nini kinatofautisha hizi processor?

1. Herufi kwenye processor za desktop.

Bila herufi – hii inakuwa na speed halisi ya processor mfano i7-4770

K- herufi hii inamaanisha processor ipo unlocked na unaweza kui over clock na kuongeza speeed. Processor yenye 3.5ghz unaweza kui overclock ikafika 4ghz. Jina lake linakuwa mfumo huu i7-4770K. ni nzuri sana kwa wanaocheza magame na kufanya rendering.

R- herufi hii inamaanisha processor hii ni ndogo sana na inaweza kutumika kwenye videsktop vyenye umbo dogo hali ya kuwa ina graphic kubwa kama iris pro. Jina lake linakuwa mfumo huu i7-4770R hii ni nzuri kwa wale wenye ofisi ambazo ni safi hawataki mawaya mengi na desktop kubwa kukaa kwenye meza. angalia picha hapo chini uone desktop ndogo.

brix1_s.gif


S- herufi hii inamaanisha hiyo proceesor wame optimize perfomance mara nyingi wanai underclock kuzuia processor kupata joto sana. Mfano i7-4770 ina 3.4ghz lakini i7-4770S ina 3.1ghz tu, ina maana hapa wamepunguza 300mhz kutoka stock kuja S.

T- herufi hii inamaanisha processor inatumia power ndogo, kwa wale wenzangu wanaotumia luku kama unataka desktop isiokula umeme basi hii ndio yenyewe ila perfomance nayo itapungua kidogo. Mfano wa jina ni i7-4770T

2. Herufi mbele ya processor za laptop(mobile)

Tumeshaona herufi mbele ya desktop, sasa hivi tuangalie herufi mbele ya processor za laptop ambazo pia zinaweza kutumika kwenye home theatre pc (htpc) au wengine wanaita mini desktop.

M- herufi hii inamaanisha hio processor ni mobile, ndio herufi common kwenye processor za laptop mfano i5-4000M

U- herufi hii inamaanisha processor ya laptop inatumia power ndogo hizi processor zinatumika sana kwenye vilaptop vyembamba (ultrabook). Kwa sababu zinakaa na chaji kutokana na kutumia power ndogo, perfomance yake nayo pia ni ndogo. Mfano i5 4250U

Y- hii ni ultra low power yaani inakula umeme mdogo kushinda hata U lakini vile vile perfomance inazidi kushuka nayo mfano i7-4610Y

HQ- herufi hii inamaanisha high perfomance, zinauzwa bei ghali sana na power yake inashindana na desktop. Usije ukajaribu kuieka kwenye mapaja laptop ya design hii maana zinashika moto upesi sana kutokana na quality ya processor. Ni nzuri kwa wale wanaopenda kucheza game, kutumia software kubwa wakiwa kitandani. Mfano ni i7-4700HQ

MQ- herufi hii inamaanisha hio procesor ni quad core. Kama umesoma vizuri juu i5 na i7 za desktop ni quadcore lakini za laptop ni dualcore, hivi processor hii inamaanisha unaweza tumia quadcore kwenye laptop yako kama unataka mfano i7-4900MQ

MX- herufi hii inamaanisha ni xtreme edition, processor hii unaweza kui over clock kama vile K series ya desktop na ina perfomance kubwa sanaaa, ila kuwa makini na mapaja tu.
Mfano i7-4940MX

Huu ndio muongozo wa kununua processor za intel, kama kuna sehemu hujapaelewa unaweza kuuliza nitaelezea zaidi.
1693255341598.jpg
IMG_20230901_174446.jpg
1693338739969.jpg


Ipi nichukue hapa Kwa ajili ya programming na chuo (engineering).
 
Kitu chochote kinacho generate picha 2D/3D ni render inaweza kuwa ku edit video, kutumia Cad software kama Autocad, Animations etc
Habari chief? Naomba ushauri kidogo maana siko deep sana kwenye issue za Tech.
Nataka niupgrade PC yangu..
Dell Latitude E7270
Spec DDR4 PC4-17000
SSD 250
Core(TM) i5- 6200U

Nataka niupgrade RAM, SSD.. Ushauri wako hapa
 
Habari chief? Naomba ushauri kidogo maana siko deep sana kwenye issue za Tech.
Nataka niupgrade PC yangu..
Dell Latitude E7270
Spec DDR4 PC4-17000
SSD 250
Core(TM) i5- 6200U

Nataka niupgrade RAM, SSD.. Ushauri wako hapa
Habari

Mkuu nimecheki online machine yako ssd yake ni m.2 ya sata na sio Nvme, inabidi uwe makini hapa vyema uitoe uipige picha uhakikishe unanunua Exactly same form factor, ssd yako sio common.

Alternative angalia kama kuna slot ya hdd unaweza bakisha hio ssd yako ukaongeza ssd nyengine kwenye sehemu ya kawaida ya sata.

Kuhusu ram angalia exactly una ram ngapi na zina speed gani. Ingia task manager kisha chagua performance kisha chagua memory utaona details za ram zako za sasa.
 
Habari

Mkuu nimecheki online machine yako ssd yake ni m.2 ya sata na sio Nvme, inabidi uwe makini hapa vyema uitoe uipige picha uhakikishe unanunua Exactly same form factor, ssd yako sio common.

Alternative angalia kama kuna slot ya hdd unaweza bakisha hio ssd yako ukaongeza ssd nyengine kwenye sehemu ya kawaida ya sata.

Kuhusu ram angalia exactly una ram ngapi na zina speed gani. Ingia task manager kisha chagua performance kisha chagua memory utaona details za ram zako za sasa.
Slot iliyotumika ni moja ya 8GB.. So nadhani naweza kuongeza nyingine moja ya 8GB!

Vip kuhusu SSD ya type hiyo zinapatikana?
 
Slot iliyotumika ni moja ya 8GB.. So nadhani naweza kuongeza nyingine moja ya 8GB!

Vip kuhusu SSD ya type hiyo zinapatikana?
Ssd zinapatikana ila ni adimu kidogo compare na nvme.

M2 sata yenyewe ina vipengo viwili na m2 nvme ina kipengo kimoja.

Soma hapa kuzielewa zaidi

Uzuri ni kwamba ssd zote zimeshuka bei unaweza pata 1TB chini ya laki.

Kuhusu ram vyema ujue speed, ni muhimu sana kwa ddr4, kama una 2400mhz ukiweka 2200mhz utaifanya speed ya machine yako kushuka.
 
Back
Top Bottom