Hemu chief tufafanulie specifications za gpu maana kuna dedicated memory na video memory na mengneyo yanatupa shda hadi kufkia hatua ya kutoelewa ukubwa wa gpu ni upi!
-dedicated ni ram inayokuja na gpu yenyewe,
-shared ni memory ambayo gpu na ram ya computer vina share.
dedicated ni nzuri sababu siku zote ipo kwa ajili ya gpu wakati shared ram hutumiwa na system nzima hivyo ukirun app ikila sana ram basi gpu nayo haita run vizuri.
pia dedicated memory za gpu nyingi zinakuwa na speed kuliko ram za kawaida,
mfano gpu za iris pro memory yake inaitwa edram ambayo ina speed kama 50Gbps wakati ram ya kawaida ikiwa na speed sana ni 25gbps (ddr4 3200mhz) ram za kawaida za mtaani ni kama 10gbps (ddr3 1300mhz)
kujua gpu nzuri hauangalii ukubwa wa ram yake tu kuna mambo mengi kama
-bandwidth ya hio ram mfano gpu yenye ddr5 ina speed kuliko yenye ddr3
-speed ya gpu, nyengine zina 300mhz wakati nyengine zina 1500mhz etc
-manufacturing technology, kuna 28nm, 22nm, 14nm etc
-memory bus
-core (gpu inaweza kuwa na core zaidi ya 1000)
ila gpu ni complicated sana ni vyema ukaangalia review kwanza nyengine on paper zinavutia lakini perfomance ndogo.