Yah sasa mkuu kwa hiyo bei napata laptop gn?? Namaana 700000
Kwa kifupi mkuu hizo pentium na celeron za sasa hivi zimegawanyika makundi kama manne hivi
-Braswell (Airmont architecture)
-Apollo lake (goldmont architecture)
-Gemini lake (goldmont plus Architecture)
-jasper lake (tremont architecture)
Braswell ilikuwa ya zamani zaidi ya miaka 5 iliopita, ilikuwa slow na ndo cpu za mwanzo kabisa, hii celeron 3060 ndio ipo kundi hili, laptop niliyokuambia usichukue.
Apollo lake ikafuatia ika improve perfomance kiasi chake.
Gemini ika improve zaidi na sasa hivi jasper lake imetoka. Nimeangalia jasper lake perfomance yake ni kubwa kushinda i7 7th gen.
Ningekuambia uchukue laptop za hizi jasper lake ila uongo hutazipata mtaani maana ndio zinatoka, realistic tafuta za Gemini lake, zipo.
Hizi ni cpu za laptop za gemini lake
-celeron N4000
-Celeron N4100
-Pentium N5000
Hivyo Angalia source zako ukiipata laptop yenye hio Cpu chukua kwa bei around laki 5 mpaka 7.
Na N4000 ni dual core sana sana Angalia N4100 na N5000 ndio nzuri zaidi.