JOAQUEM
JF-Expert Member
- Jul 28, 2012
- 2,020
- 1,671
yap processor inabadilishwa
1.kwa desktop nafikiri zote zinabadilishika
2. kwa laptop inabidi ufungue halafu uangalie kama ipo socketed (inachomoka) kuna nyengine zinachomelewa humo humo huwa hazitoki.
kwa desktop unaangalia tu aina ya motherboard mfano motherboard inaitwa lga-1150 basi hii inakubali processor zote za haswell (4th generation) iwe ni pentium, i3, i5, i7, xeon nk zote zitakubali cha muhimu tu uwe na cooler (feni) ambalo litapulizia vizuri. mfano computer ilikua na processor ya pentium ambayo thermal design power (TDP) yake ni 54 watts na kafeni kadogo ukabadili ukaeka i7 ambayo TDP yake ni 88W basi kale kafeni hakatapuliza vizuri hii i5 na computer itapata moto sana itabidi ueke feni kubwa kubwa
kwa laptop kubadilisha sio tu unaangalia motherboard bali pia unatakiwa uangalie na TDP (sababu huwezi kubadilisha mafeni ya laptop ukaeka makubwa) kuna processor za aina mbili hapa ambazo unatakiwa uzijue
-zinazoishiwa na u mbele
-zinazoishiwa na m mbele
hizi zinazoishiwa na u mbele nyingi zina TDP ya 15w zinatumia umeme mdogo hivyo ukibadili processor yake itabidi utafute u mwenzake. mfano unabadili i3 4010u kwenda i7 4600u
zinazoishiwa na m mbele nyingi zina TDP ya 35-37w ambayo ni kubwa kwa laptop hivyo ukibadilisha processor yabidi utafute yenye m kwa mbele. mfano i3 4000m ibadili iwe i7 4600m.
si kazi ngumu sana ni rahisi sana,
KWA HII NAWEZA BADILI NA IPI???