Muongozo wa kununua vifaa vinavyotumia processor za intel

Muongozo wa kununua vifaa vinavyotumia processor za intel

ukitumia 3rd party player kama vlc je? then uongeze saut had mwisho
Jinsi inavyo sound ni kama zimewekwa vi- tweeter tupu tu. Na yeye kitu cha kwanza alichofanya aliweka VLC player, zaidi kama iliongezeka sauti kidogo. Ila inavyo sound ni vile vile.
 
Hp envy ts 14 sleekbook
Cpu intel core i5 4200u
Ram 4gb 798.1mhz
Gpu intel hd graphic 4600
Nvidia geforce gt 740m

Vp hyo mkuu kwa gaming na kurun software kubwa inaweza?
 
Hp envy ts 14 sleekbook
Cpu intel core i5 4200u
Ram 4gb 798.1mhz
Gpu intel hd graphic 4600
Nvidia geforce gt 740m

Vp hyo mkuu kwa gaming na kurun software kubwa inaweza?
ipo fresh , utacheza low to medium settings,
 
Hp envy ts 14 sleekbook
Cpu intel core i5 4200u
Ram 4gb 798.1mhz
Gpu intel hd graphic 4600
Nvidia geforce gt 740m

Vp hyo mkuu kwa gaming na kurun software kubwa inaweza?
angalia vizuri hizo specs intel i5 4200u ina hd4400, hio ni either 4200m au hio gpu ni hd4400.

ila sababu ina gt 740m utacheza kwa low setting.
 
Jinsi inavyo sound ni kama zimewekwa vi- tweeter tupu tu. Na yeye kitu cha kwanza alichofanya aliweka VLC player, zaidi kama iliongezeka sauti kidogo. Ila inavyo sound ni vile vile.
labda ni tatizo la hardware mkuu maana nimeangalia review yake notebookcheck wamesema ni average na inatosha matumizi ya kawaida, hivyo haikutakiwa itoe sauti kama hivyo, labda kuna speaker nyengine ambayo ni ya bass haifanyi kazi, umeifungua?
 
yes ni hiyo hiyo 5750m ,
hio ndio top mkuu, so ku updgrade ni ngumu, naziona cpu zake hapa ebay $40 hadi $90, na sababu ni apu hio ina gpu na cpu pamoja ndio maana hujaona motherboard zenye gpu, kwa lugha nyengine ukinunua cpu itakuja na gpu yake pamoja imetengenezewa ndani
 
Computer nyingi tunazonunua huwa zinatumia processor za intel au amd, lakini ni intel ambaye ametawala sana kushinda amd kwenye computer zetu. Leo nimeamua niandike uzi huu kuhusu hizi processor za intel na namna ya kuzichagua ili kuwasaidia watu wanapotaka kununua laptop/desktop mpya wafanye maamuzi sahihi.

Processor ni nini?

Labda utakuwa unajiuliza kwa nini ukitaka kununua laptop mpya unatakiwa uangalie processor? Nini cha muhimu kuhusu hii processor?

-Kwa lugha rahisi processor ni kifaa ndani ya computer yako kinachobeba maagizo ya program za computer. Maagizo hayo yanaweza kuwa ya kimahesabu, kimantiki, maagizo yanayoingia kwenye computer na yanayotoka.

-jinsi processor inavyokuwa na speed kubwa ndio jinsi maagizo yatakavyofanywa haraka na ndio jinsi program za computer zitakavyofanya kazi upesi.
processor_01.jpg

Familia ya processor za intel

Intel wana processor za aina nyingi na ni ngumu kuzitaja kwa pamoja, ila wameturahisishia kwa kuzipanga processor zao kwenye familia. Na hii ndio familia yao.

1. Atom processor- processor hizi hutumika kwenye vimini laptop na tablet ni ndogo kiumbo ndio maana hata vifaa vyake ni vidogo, processor hizi hazina nguvu sana na vifaa vyake hukaa sana na chaji.

2. Celeron processor- Haina tofauti sana na atom ila hii ina afadhali kidogo. Inatumika kwenye vifaa vikubwa kuliko atom kama vile laptop kubwa na desktop

3. Pentium- hii ina speed kuliko celeron na atom pia inatumika kwenye vifaa vikubwa.

4. Core 2 duo- hii ni maarufu kwa perfomance yake ya multitasking, inauwezo wakufanya mambo mengi kwa wakati mmoja ila nyingi ni za kizamani.

5. Core i3- hii ni processor latest za intel ni dual core lakini core zake zina perfomance kubwa na pia inakuwa na thread 2 kwenye kila core, ni nzuri kwa wanaotaka perfomance kubwa kwa bei rahisi.

6. Core i5- ya laptop ni dualcore na ya desktop ni quadcore isiyokuwa na thread, software nyingi kubwa duniani zimekuwa optimized kutumia core kama za i5, ni nzuri sana kwa watu wanaotumia software zinazodemand perfomance lakini hawafanyi multitasking.

7.Core i7- hii inakuwa na quadcore processor na thread 8 kwenye desktop na pia inaweza kuwa dualcore kwenye laptop. Hii ndio processor nzuri zaidi kwa watu wa kawaida na inafanya multitasking hata kama software zinademand sana.

8. Xeon- hii ndio processor yenye speed zaidi kwenye processor za intel lakini imekuwa designed kufanya kazi kwenye computer kubwa kama vile server. Unapohost website processor kama hii ndio inayoprocess webpages.

Generation ya processor(muhimu)

Ni muhimu sana kujua processor inatokea generation ipi kuna processor zenye i7 ya 2010 ambazo zipo slow vibaya mno, na pia kuna uwezekano i3 kuipita i7 kwenye perfomance kama zinatoka generation tofauti. Hivyo eneo hili inabidi uwe makini kuepuka kuuziwa mbuzi kwenye gunia. Hivyo unaponunua laptop/desktop ni lazima ujue ipo generation gani la sivyo upo hatarini na hivi ndio namna ya kujua.

- Processor yenye namba inayoanziwa na elfu nne ni fourth generation(4xxx)
Mfano Intel i3-4130.

- Processor yenye namba inayoanziwa na elfu tatu ni third generation (3xxx)
Mfano i3-3130.

- Processor inayoanziwa na elfu mbili ni second generation(2xxx)
Mfano i3-2140

Sishauri kabisa kununua processor ya first generation, mtu unatakiwa atleast ununue ya second generation na pia bei inatakiwa iwe ndogo kwa hii second compare na third/fourth.

Processor ndogo kama atom na celeron zina generation zake ambazo ni
-clover trail
-bay trail

Processor za zamani za atom zilikuwa mbaya sana na zipo slow ila baytrail ikaja kuzipa nguvu na kuzifanya ziwe na perfomance kubwa, hivyo kama unataka kifaa cha atom/celeron make sure processor yake iwe inatoka generation ya baytrail.

Herufi za mbele ya processor(muhimu)

Kama umechunguza mbele ya processor kunakuwa na herufi mbali mbali hizi pia ni muhimu sana kuzijua kwani usipozizingatia unaweza kujuta.

Mfano processor inaweza kuitwa i5-4000m au i5-4000u au i5-4000y je nini kinatofautisha hizi processor?

1. Herufi kwenye processor za desktop.

Bila herufi &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; hii inakuwa na speed halisi ya processor mfano i7-4770

K- herufi hii inamaanisha processor ipo unlocked na unaweza kui over clock na kuongeza speeed. Processor yenye 3.5ghz unaweza kui overclock ikafika 4ghz. Jina lake linakuwa mfumo huu i7-4770K. ni nzuri sana kwa wanaocheza magame na kufanya rendering.

R- herufi hii inamaanisha processor hii ni ndogo sana na inaweza kutumika kwenye videsktop vyenye umbo dogo hali ya kuwa ina graphic kubwa kama iris pro. Jina lake linakuwa mfumo huu i7-4770R hii ni nzuri kwa wale wenye ofisi ambazo ni safi hawataki mawaya mengi na desktop kubwa kukaa kwenye meza. angalia picha hapo chini uone desktop ndogo.

brix1_s.gif

S- herufi hii inamaanisha hiyo proceesor wame optimize perfomance mara nyingi wanai underclock kuzuia processor kupata joto sana. Mfano i7-4770 ina 3.4ghz lakini i7-4770S ina 3.1ghz tu, ina maana hapa wamepunguza 300mhz kutoka stock kuja S.

T- herufi hii inamaanisha processor inatumia power ndogo, kwa wale wenzangu wanaotumia luku kama unataka desktop isiokula umeme basi hii ndio yenyewe ila perfomance nayo itapungua kidogo. Mfano wa jina ni i7-4770T

2. Herufi mbele ya processor za laptop(mobile)

Tumeshaona herufi mbele ya desktop, sasa hivi tuangalie herufi mbele ya processor za laptop ambazo pia zinaweza kutumika kwenye home theatre pc (htpc) au wengine wanaita mini desktop.

M- herufi hii inamaanisha hio processor ni mobile, ndio herufi common kwenye processor za laptop mfano i5-4000M

U- herufi hii inamaanisha processor ya laptop inatumia power ndogo hizi processor zinatumika sana kwenye vilaptop vyembamba (ultrabook). Kwa sababu zinakaa na chaji kutokana na kutumia power ndogo, perfomance yake nayo pia ni ndogo. Mfano i5 4250U

Y- hii ni ultra low power yaani inakula umeme mdogo kushinda hata U lakini vile vile perfomance inazidi kushuka nayo mfano i7-4610Y

HQ- herufi hii inamaanisha high perfomance, zinauzwa bei ghali sana na power yake inashindana na desktop. Usije ukajaribu kuieka kwenye mapaja laptop ya design hii maana zinashika moto upesi sana kutokana na quality ya processor. Ni nzuri kwa wale wanaopenda kucheza game, kutumia software kubwa wakiwa kitandani. Mfano ni i7-4700HQ

MQ- herufi hii inamaanisha hio procesor ni quad core. Kama umesoma vizuri juu i5 na i7 za desktop ni quadcore lakini za laptop ni dualcore, hivi processor hii inamaanisha unaweza tumia quadcore kwenye laptop yako kama unataka mfano i7-4900MQ

MX- herufi hii inamaanisha ni xtreme edition, processor hii unaweza kui over clock kama vile K series ya desktop na ina perfomance kubwa sanaaa, ila kuwa makini na mapaja tu.
Mfano i7-4940MX

Huu ndio muongozo wa kununua processor za intel, kama kuna sehemu hujapaelewa unaweza kuuliza nitaelezea zaidi.
3bae56adc796435b733ad2c88b40e0c7.jpg

Vp hii apa mkuu
 
6th Gen Intel Quad-Core i5-6300HQ Processor up to 3.2GHz, 8GB DDR3, 256GB SSD, Nvidia GeForce GTX 960M,

PC yenye sifa hizi nitaipata Tanzania hapa
 
Mkuu me pc yangu toshiba satelite c850-b839 shida yake inawaka vizuri ila ikianza kuload kuelekea kwenye welcome screen inazima ghafla. Na ikifanikiwa kuwaka nikifungua tu apps inazima ghafla. Naitumia bila bettery ilishakufa je inaweza ikawa ndo shida. Me nahisi shida ni processor kwasababu inakoroma flani hivi kama kitu kinachemka. Kama ndo shida hiyo naweza kubadili kwa kuupgrade sababu hii pc inatumika mara nyingi apa nyumbani kwa kuchezea game. W10
71ba50d3a43f550bc70870454c9757a6.jpg
20170519_223619.jpg
 
View attachment 511607
katika computer cpu ni kitu kigumu sana, sio rahisi kufa ovyo. feni linazunguka? maybe cooling ya hio laptop imechomoka, haipati joto sanA?

pia imaweza kuwa motherboard ama tatizo jengine hupati beep au error yoyote ile unapowasha?
 
Nimechek feni ipo vizuri inapiga kazi. Napata media test failure . Pxe......
Na ikiwaka inachukua muda mrefu kwenye welcome screen kama dk5-7 na nikizima hivyohivyo.
 
Nimechek feni ipo vizuri inapiga kazi. Napata media test failure . Pxe......
Na ikiwaka inachukua muda mrefu kwenye welcome screen kama dk5-7 na nikizima hivyohivyo.

1. kama inachukua muda kuboot inamaana ni tatizo la HDD
2. pxe nayo ni pre boot execution enviroment pia inaashiria hivyo hiyo kwenye HDD

jaribu kwenda bios kaangalie umeeka uboot na nini? kuna mambo mengi kama network boot, boot from CD, usb boot na hio HDD yako. hakikisha HDD ndio kama primary boot.
 
Kama kuna MTU ana key za Microsoft word 2016 naomba tuwasiliane nahitaji sana
 
1. kama inachukua muda kuboot inamaana ni tatizo la HDD
2. pxe nayo ni pre boot execution enviroment pia inaashiria hivyo hiyo kwenye HDD

jaribu kwenda bios kaangalie umeeka uboot na nini? kuna mambo mengi kama network boot, boot from CD, usb boot na hio HDD yako. hakikisha HDD ndio kama primary boot.
Kwenye bios inaonesha
1.Hdd
2.CD
3.USb
4.pxe
 
Back
Top Bottom