Muongozo wa kununua vifaa vinavyotumia processor za intel

Muongozo wa kununua vifaa vinavyotumia processor za intel

Computer nyingi tunazonunua huwa zinatumia processor za intel au amd, lakini ni intel ambaye ametawala sana kushinda amd kwenye computer zetu. Leo nimeamua niandike uzi huu kuhusu hizi processor za intel na namna ya kuzichagua ili kuwasaidia watu wanapotaka kununua laptop/desktop mpya wafanye maamuzi sahihi.

Processor ni nini?

Labda utakuwa unajiuliza kwa nini ukitaka kununua laptop mpya unatakiwa uangalie processor? Nini cha muhimu kuhusu hii processor?

-Kwa lugha rahisi processor ni kifaa ndani ya computer yako kinachobeba maagizo ya program za computer. Maagizo hayo yanaweza kuwa ya kimahesabu, kimantiki, maagizo yanayoingia kwenye computer na yanayotoka.

-jinsi processor inavyokuwa na speed kubwa ndio jinsi maagizo yatakavyofanywa haraka na ndio jinsi program za computer zitakavyofanya kazi upesi.
processor_01.jpg


Familia ya processor za intel

Intel wana processor za aina nyingi na ni ngumu kuzitaja kwa pamoja, ila wameturahisishia kwa kuzipanga processor zao kwenye familia. Na hii ndio familia yao.

1. Atom processor- processor hizi hutumika kwenye vimini laptop na tablet ni ndogo kiumbo ndio maana hata vifaa vyake ni vidogo, processor hizi hazina nguvu sana na vifaa vyake hukaa sana na chaji.

2. Celeron processor- Haina tofauti sana na atom ila hii ina afadhali kidogo. Inatumika kwenye vifaa vikubwa kuliko atom kama vile laptop kubwa na desktop

3. Pentium- hii ina speed kuliko celeron na atom pia inatumika kwenye vifaa vikubwa.

4. Core 2 duo- hii ni maarufu kwa perfomance yake ya multitasking, inauwezo wakufanya mambo mengi kwa wakati mmoja ila nyingi ni za kizamani.

5. Core i3- hii ni processor latest za intel ni dual core lakini core zake zina perfomance kubwa na pia inakuwa na thread 2 kwenye kila core, ni nzuri kwa wanaotaka perfomance kubwa kwa bei rahisi.

6. Core i5- ya laptop ni dualcore na ya desktop ni quadcore isiyokuwa na thread, software nyingi kubwa duniani zimekuwa optimized kutumia core kama za i5, ni nzuri sana kwa watu wanaotumia software zinazodemand perfomance lakini hawafanyi multitasking.

7.Core i7- hii inakuwa na quadcore processor na thread 8 kwenye desktop na pia inaweza kuwa dualcore kwenye laptop. Hii ndio processor nzuri zaidi kwa watu wa kawaida na inafanya multitasking hata kama software zinademand sana.

8. Xeon- hii ndio processor yenye speed zaidi kwenye processor za intel lakini imekuwa designed kufanya kazi kwenye computer kubwa kama vile server. Unapohost website processor kama hii ndio inayoprocess webpages.


Generation ya processor(muhimu)

Ni muhimu sana kujua processor inatokea generation ipi kuna processor zenye i7 ya 2010 ambazo zipo slow vibaya mno, na pia kuna uwezekano i3 kuipita i7 kwenye perfomance kama zinatoka generation tofauti. Hivyo eneo hili inabidi uwe makini kuepuka kuuziwa mbuzi kwenye gunia. Hivyo unaponunua laptop/desktop ni lazima ujue ipo generation gani la sivyo upo hatarini na hivi ndio namna ya kujua.

- Processor yenye namba inayoanziwa na elfu nne ni fourth generation(4xxx)
Mfano Intel i3-4130.

- Processor yenye namba inayoanziwa na elfu tatu ni third generation (3xxx)
Mfano i3-3130.

- Processor inayoanziwa na elfu mbili ni second generation(2xxx)
Mfano i3-2140

Sishauri kabisa kununua processor ya first generation, mtu unatakiwa atleast ununue ya second generation na pia bei inatakiwa iwe ndogo kwa hii second compare na third/fourth.

Processor ndogo kama atom na celeron zina generation zake ambazo ni
-clover trail
-bay trail

Processor za zamani za atom zilikuwa mbaya sana na zipo slow ila baytrail ikaja kuzipa nguvu na kuzifanya ziwe na perfomance kubwa, hivyo kama unataka kifaa cha atom/celeron make sure processor yake iwe inatoka generation ya baytrail.


Herufi za mbele ya processor(muhimu)

Kama umechunguza mbele ya processor kunakuwa na herufi mbali mbali hizi pia ni muhimu sana kuzijua kwani usipozizingatia unaweza kujuta.

Mfano processor inaweza kuitwa i5-4000m au i5-4000u au i5-4000y je nini kinatofautisha hizi processor?

1. Herufi kwenye processor za desktop.

Bila herufi &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; hii inakuwa na speed halisi ya processor mfano i7-4770

K- herufi hii inamaanisha processor ipo unlocked na unaweza kui over clock na kuongeza speeed. Processor yenye 3.5ghz unaweza kui overclock ikafika 4ghz. Jina lake linakuwa mfumo huu i7-4770K. ni nzuri sana kwa wanaocheza magame na kufanya rendering.

R- herufi hii inamaanisha processor hii ni ndogo sana na inaweza kutumika kwenye videsktop vyenye umbo dogo hali ya kuwa ina graphic kubwa kama iris pro. Jina lake linakuwa mfumo huu i7-4770R hii ni nzuri kwa wale wenye ofisi ambazo ni safi hawataki mawaya mengi na desktop kubwa kukaa kwenye meza. angalia picha hapo chini uone desktop ndogo.

brix1_s.gif


S- herufi hii inamaanisha hiyo proceesor wame optimize perfomance mara nyingi wanai underclock kuzuia processor kupata joto sana. Mfano i7-4770 ina 3.4ghz lakini i7-4770S ina 3.1ghz tu, ina maana hapa wamepunguza 300mhz kutoka stock kuja S.

T- herufi hii inamaanisha processor inatumia power ndogo, kwa wale wenzangu wanaotumia luku kama unataka desktop isiokula umeme basi hii ndio yenyewe ila perfomance nayo itapungua kidogo. Mfano wa jina ni i7-4770T

2. Herufi mbele ya processor za laptop(mobile)

Tumeshaona herufi mbele ya desktop, sasa hivi tuangalie herufi mbele ya processor za laptop ambazo pia zinaweza kutumika kwenye home theatre pc (htpc) au wengine wanaita mini desktop.

M- herufi hii inamaanisha hio processor ni mobile, ndio herufi common kwenye processor za laptop mfano i5-4000M

U- herufi hii inamaanisha processor ya laptop inatumia power ndogo hizi processor zinatumika sana kwenye vilaptop vyembamba (ultrabook). Kwa sababu zinakaa na chaji kutokana na kutumia power ndogo, perfomance yake nayo pia ni ndogo. Mfano i5 4250U

Y- hii ni ultra low power yaani inakula umeme mdogo kushinda hata U lakini vile vile perfomance inazidi kushuka nayo mfano i7-4610Y

HQ- herufi hii inamaanisha high perfomance, zinauzwa bei ghali sana na power yake inashindana na desktop. Usije ukajaribu kuieka kwenye mapaja laptop ya design hii maana zinashika moto upesi sana kutokana na quality ya processor. Ni nzuri kwa wale wanaopenda kucheza game, kutumia software kubwa wakiwa kitandani. Mfano ni i7-4700HQ

MQ- herufi hii inamaanisha hio procesor ni quad core. Kama umesoma vizuri juu i5 na i7 za desktop ni quadcore lakini za laptop ni dualcore, hivi processor hii inamaanisha unaweza tumia quadcore kwenye laptop yako kama unataka mfano i7-4900MQ

MX- herufi hii inamaanisha ni xtreme edition, processor hii unaweza kui over clock kama vile K series ya desktop na ina perfomance kubwa sanaaa, ila kuwa makini na mapaja tu.
Mfano i7-4940MX

Huu ndio muongozo wa kununua processor za intel, kama kuna sehemu hujapaelewa unaweza kuuliza nitaelezea zaidi.
sawa nikienda sokoni nitaenda za uzi huu
 
mimi nimeamua ku invest on gaming pc kuliko hizi consoles like ps4,ps4 pro nk, ivi kwa pc c rahic kucheza new titles bureeee,au bora nichukue ps4 sema roho haitak kabisaa

Sent using Jamii Forums mobile app
mkuu kwenye pc pia kuna games ni ngumu kuchakachulika, mfano fifa 17 imechukua almost mwaka mzima hadi wakaweza kuichakachua, lakini overall utacheza games nyingi bure.

na kama una tv au monitor yenye display nzuri kama full HD au 4K kwa pc uta enjoy zaidi sababu hizi console zinazingua kwenye hizi mambo.

uzuri wa console ni kama umeihack, hapo uta enjoy tu games, huna haja ya kuanza kuhakikisha specs kama zinafaa
 
nazan nkianza ku build pc yang ntakutafta kwa ushauri zaidi,nataka ni upgrade hizi OEM mashines nimejarib kuchek unatakiwa uwe na power supply at least 500watts, hio nkiweka na gtx 1060 miaka 3-5 nadundaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nazan nkianza ku build pc yang ntakutafta kwa ushauri zaidi,nataka ni upgrade hizi OEM mashines nimejarib kuchek unatakiwa uwe na power supply at least 500watts, hio nkiweka na gtx 1060 miaka 3-5 nadundaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
na baadhi ya oem pc power supply zake haziingiliani na pc nyengine hivyo hata ukitaka hio ya 500w unaweza usiipate.

mkuu pia angalia na laptop kama mfuko upo vizuri, hizi series za nvidia za 1xxx zimetulia kwenye laptop, perfomance difference ni kama 10% tu, unapata laptop za 1050ti na 1060 kwa around dola 700 hadi 800.
 
na baadhi ya oem pc power supply zake haziingiliani na pc nyengine hivyo hata ukitaka hio ya 500w unaweza usiipate.

mkuu pia angalia na laptop kama mfuko upo vizuri, hizi series za nvidia za 1xxx zimetulia kwenye laptop, perfomance difference ni kama 10% tu, unapata laptop za 1050ti na 1060 kwa around dola 700 hadi 800.
mkuu hii dell optiplex 9020 either i5 au i7, inatumia socket 1150.hizi OEM PC nikiweka power supply tofauti ita support??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nlipiga hesabu sana mkuuu nkaona hizo laptop dola 700-800 bado ni bei za abroad ikifika bongo pigia hesab had dolla 1000-1200 ndo unakuwa nayo,hapo parefu xana asee,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba msaada
Hii ya kwangu ni Intel(R) core (TM) duo CPU T8100 @2.10GHz,
nimeshindwa kutambua generation na zile herufi mbele ya processor
 
mkuu hii dell optiplex 9020 either i5 au i7, inatumia socket 1150.hizi OEM PC nikiweka power supply tofauti ita support??

Sent using Jamii Forums mobile app
hizi optiplex zinakuwa na 8 pin power supply, huwezi upgrade kawaida, ila naskia kuna adapter ya ku convert 8 pin kwenda 24pin, sina uhakika ufanyaji kazi wake upoje
 
20170913_091414.jpg
20170913_091333.jpg
mkuu habari,kwa hizi spec hivi naweza cheza latest games..mfano GTA ? ?hizi mpya mpya?

"gentlemanx "
 
300 watts mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
itafaa mkuu, sema unatakiwa ujue hizi gpu zipo za aina mbili,
-gpu ya kawaida ambayo inahitaji umeme toka power supply yako, hii haitafanya kazi kwenye pc yako.

-gpu ambazo ni low profile, hizi zinatumia umeme mdogo, na zinafyonza tu umeme toka kwenye motherboard, hakuna haja ya umeme toka kwenye power supply.

ukitafuta 1050ti ambayo ni low profile (watts 75) itakubali pc yako.
 
Back
Top Bottom