Muongozo wa kununua vifaa vinavyotumia processor za intel

Muongozo wa kununua vifaa vinavyotumia processor za intel

Chief-Mkwawa

kuna hii mashine mtu anataka niuzia 150k ni HP ya kulala

i3 -3220 @3.30ghz hii,unasemaje kwenye hii bei ni sawa?

unaionaje ktk utendaji kazi? nikiiweka GPU itaweza kazi

za Graphic muda mrefu? nakutegemea wewe boss...
Bei nzuri kiasi mkuu,

Kwenye gpu mkuu unaangalia psu kwanza. Na sababu we ni mzee wa machimbo unaweza tafuta i5 ama i7 cpu tupu na kui upgrade kwa baadae.

Ingekuwa mimi ningeinunua.
 
na comment ili kesho niendelee kusoma pale nilipo ishia 😷 😷 thanks chief mkwawa
 
Wakuu nisaidieni spec zinazo faa kwa laptop ya kazi za video editing na photo editing.
 
Computer nyingi tunazonunua huwa zinatumia processor za intel au amd, lakini ni intel ambaye ametawala sana kushinda amd kwenye computer zetu. Leo nimeamua niandike uzi huu kuhusu hizi processor za intel na namna ya kuzichagua ili kuwasaidia watu wanapotaka kununua laptop/desktop mpya wafanye maamuzi sahihi.

Processor ni nini?

Labda utakuwa unajiuliza kwa nini ukitaka kununua laptop mpya unatakiwa uangalie processor? Nini cha muhimu kuhusu hii processor?

-Kwa lugha rahisi processor ni kifaa ndani ya computer yako kinachobeba maagizo ya program za computer. Maagizo hayo yanaweza kuwa ya kimahesabu, kimantiki, maagizo yanayoingia kwenye computer na yanayotoka.

-jinsi processor inavyokuwa na speed kubwa ndio jinsi maagizo yatakavyofanywa haraka na ndio jinsi program za computer zitakavyofanya kazi upesi.
processor_01.jpg

Familia ya processor za intel

Intel wana processor za aina nyingi na ni ngumu kuzitaja kwa pamoja, ila wameturahisishia kwa kuzipanga processor zao kwenye familia. Na hii ndio familia yao.

1. Atom processor- processor hizi hutumika kwenye vimini laptop na tablet ni ndogo kiumbo ndio maana hata vifaa vyake ni vidogo, processor hizi hazina nguvu sana na vifaa vyake hukaa sana na chaji.

2. Celeron processor- Haina tofauti sana na atom ila hii ina afadhali kidogo. Inatumika kwenye vifaa vikubwa kuliko atom kama vile laptop kubwa na desktop

3. Pentium- hii ina speed kuliko celeron na atom pia inatumika kwenye vifaa vikubwa.

4. Core 2 duo- hii ni maarufu kwa perfomance yake ya multitasking, inauwezo wakufanya mambo mengi kwa wakati mmoja ila nyingi ni za kizamani.

5. Core i3- hii ni processor latest za intel ni dual core lakini core zake zina perfomance kubwa na pia inakuwa na thread 2 kwenye kila core, ni nzuri kwa wanaotaka perfomance kubwa kwa bei rahisi.

6. Core i5- ya laptop ni dualcore na ya desktop ni quadcore isiyokuwa na thread, software nyingi kubwa duniani zimekuwa optimized kutumia core kama za i5, ni nzuri sana kwa watu wanaotumia software zinazodemand perfomance lakini hawafanyi multitasking.

7.Core i7- hii inakuwa na quadcore processor na thread 8 kwenye desktop na pia inaweza kuwa dualcore kwenye laptop. Hii ndio processor nzuri zaidi kwa watu wa kawaida na inafanya multitasking hata kama software zinademand sana.

8. Xeon- hii ndio processor yenye speed zaidi kwenye processor za intel lakini imekuwa designed kufanya kazi kwenye computer kubwa kama vile server. Unapohost website processor kama hii ndio inayoprocess webpages.

Generation ya processor(muhimu)

Ni muhimu sana kujua processor inatokea generation ipi kuna processor zenye i7 ya 2010 ambazo zipo slow vibaya mno, na pia kuna uwezekano i3 kuipita i7 kwenye perfomance kama zinatoka generation tofauti. Hivyo eneo hili inabidi uwe makini kuepuka kuuziwa mbuzi kwenye gunia. Hivyo unaponunua laptop/desktop ni lazima ujue ipo generation gani la sivyo upo hatarini na hivi ndio namna ya kujua.

- Processor yenye namba inayoanziwa na elfu nne ni fourth generation(4xxx)
Mfano Intel i3-4130.

- Processor yenye namba inayoanziwa na elfu tatu ni third generation (3xxx)
Mfano i3-3130.

- Processor inayoanziwa na elfu mbili ni second generation(2xxx)
Mfano i3-2140

Sishauri kabisa kununua processor ya first generation, mtu unatakiwa atleast ununue ya second generation na pia bei inatakiwa iwe ndogo kwa hii second compare na third/fourth.

Processor ndogo kama atom na celeron zina generation zake ambazo ni
-clover trail
-bay trail

Processor za zamani za atom zilikuwa mbaya sana na zipo slow ila baytrail ikaja kuzipa nguvu na kuzifanya ziwe na perfomance kubwa, hivyo kama unataka kifaa cha atom/celeron make sure processor yake iwe inatoka generation ya baytrail.

Herufi za mbele ya processor(muhimu)

Kama umechunguza mbele ya processor kunakuwa na herufi mbali mbali hizi pia ni muhimu sana kuzijua kwani usipozizingatia unaweza kujuta.

Mfano processor inaweza kuitwa i5-4000m au i5-4000u au i5-4000y je nini kinatofautisha hizi processor?

1. Herufi kwenye processor za desktop.

Bila herufi – hii inakuwa na speed halisi ya processor mfano i7-4770

K- herufi hii inamaanisha processor ipo unlocked na unaweza kui over clock na kuongeza speeed. Processor yenye 3.5ghz unaweza kui overclock ikafika 4ghz. Jina lake linakuwa mfumo huu i7-4770K. ni nzuri sana kwa wanaocheza magame na kufanya rendering.

R- herufi hii inamaanisha processor hii ni ndogo sana na inaweza kutumika kwenye videsktop vyenye umbo dogo hali ya kuwa ina graphic kubwa kama iris pro. Jina lake linakuwa mfumo huu i7-4770R hii ni nzuri kwa wale wenye ofisi ambazo ni safi hawataki mawaya mengi na desktop kubwa kukaa kwenye meza. angalia picha hapo chini uone desktop ndogo.

brix1_s.gif

S- herufi hii inamaanisha hiyo proceesor wame optimize perfomance mara nyingi wanai underclock kuzuia processor kupata joto sana. Mfano i7-4770 ina 3.4ghz lakini i7-4770S ina 3.1ghz tu, ina maana hapa wamepunguza 300mhz kutoka stock kuja S.

T- herufi hii inamaanisha processor inatumia power ndogo, kwa wale wenzangu wanaotumia luku kama unataka desktop isiokula umeme basi hii ndio yenyewe ila perfomance nayo itapungua kidogo. Mfano wa jina ni i7-4770T

2. Herufi mbele ya processor za laptop(mobile)

Tumeshaona herufi mbele ya desktop, sasa hivi tuangalie herufi mbele ya processor za laptop ambazo pia zinaweza kutumika kwenye home theatre pc (htpc) au wengine wanaita mini desktop.

M- herufi hii inamaanisha hio processor ni mobile, ndio herufi common kwenye processor za laptop mfano i5-4000M

U- herufi hii inamaanisha processor ya laptop inatumia power ndogo hizi processor zinatumika sana kwenye vilaptop vyembamba (ultrabook). Kwa sababu zinakaa na chaji kutokana na kutumia power ndogo, perfomance yake nayo pia ni ndogo. Mfano i5 4250U

Y- hii ni ultra low power yaani inakula umeme mdogo kushinda hata U lakini vile vile perfomance inazidi kushuka nayo mfano i7-4610Y

HQ- herufi hii inamaanisha high perfomance, zinauzwa bei ghali sana na power yake inashindana na desktop. Usije ukajaribu kuieka kwenye mapaja laptop ya design hii maana zinashika moto upesi sana kutokana na quality ya processor. Ni nzuri kwa wale wanaopenda kucheza game, kutumia software kubwa wakiwa kitandani. Mfano ni i7-4700HQ

MQ- herufi hii inamaanisha hio procesor ni quad core. Kama umesoma vizuri juu i5 na i7 za desktop ni quadcore lakini za laptop ni dualcore, hivi processor hii inamaanisha unaweza tumia quadcore kwenye laptop yako kama unataka mfano i7-4900MQ

MX- herufi hii inamaanisha ni xtreme edition, processor hii unaweza kui over clock kama vile K series ya desktop na ina perfomance kubwa sanaaa, ila kuwa makini na mapaja tu.
Mfano i7-4940MX

Huu ndio muongozo wa kununua processor za intel, kama kuna sehemu hujapaelewa unaweza kuuliza nitaelezea zaidi.
. @#Somo zuri Sana 😍😍😍
 
Tafuta Ryzen 5, utapata combination nzuri za cpu na gpu bei around laki 9, tembelea hapa tuliwahi kui discuss

Naomba ushauri wa Lapotop itakayofaa kwa kazi hizi

Ambayo utaipata kwa urahisi ni Ryzen 5 2500u ama 3500u, hapo 3500u ndio bora zaidi, tafuta hio.

Pia ipo ryzen 5 4500u, ngumu kwa hio budget ila ni nzuri zaidi ya hizo hapo juu.
Mkuu samahani naomba msaada wako nahitaji pc inayoweza perform program za video graphics and design , mi niliona hii sehemu nikafkr inanifaa kabla sjajiachia nipe mwongozo mkuu , natanguliza shukran bei yao 850k
IMG_20200902_100603.jpg
 
Mkuu hiyo Ryzen 5 3500u spec zake zinakuwaje?. Je nikikosa ipi una suggest tofauti na ryzen?
 
Mkuu hiyo Ryzen 5 3500u spec zake zinakuwaje?. Je nikikosa ipi una suggest tofauti na ryzen?
Ryzen 5 3500u ina core 4 na thread 8 hivyo itasaidia kukupa speed wakati wa kurender,

Pia gpu yake ni Radeon Vega 8, ambayo ni decent, haina nguvu sana pia sio dhaifu.

Kama unakosa hio ryzen 5 angalau upate intel core i5 gen ya 8, hii pia ina core 4 na thread 8,

Kwa intel ukitumia software inayosupport quicksync inakuwa na speed kubwa sana wakati wa kurender, sema si software zote zinasuport hii technology, na weakness kubwa ni software za Adobe hazikubali hii kwa version zote za zamani, ila version mpya za 2018 kupanda naona wameanza kuweka hii technology.
 
Asante mkuu, je nawezaje kufaham wakati na nunua laptop Kuwa hii ina core 4 na thread 8 au zaidi ya hapo?
 
Asante mkuu, je nawezaje kufaham wakati na nunua laptop Kuwa hii ina core 4 na thread 8 au zaidi ya hapo?
Device manager inaonesha, kila core wanaiandika separate.

Pia unaweza search neno dxdiag ama kwenda my computer kisha properties, utapata model husika kisha igoogle angalia result ya kwanza toka site ya Intel/Amd kuona specs kwa kirefu.
 
Mkuu samahani naomba msaada wako nahitaji pc inayoweza perform program za video graphics and design , mi niliona hii sehemu nikafkr inanifaa kabla sjajiachia nipe mwongozo mkuu , natanguliza shukran bei yao 850k
View attachment 1556168
kwa kuangalia hio frequency ya 2.0ghz mbona kama ni i3? hii laptop ina walakin sana hayo maneno ya juu hapo, i7 gen ya 8 mainstream base clock ni 1.8ghz, vyema uipitie uiangalie vizuri.
 
jamani nimeuliza swali langu lakin halijajibiwa bado ni kuusu hizi Intel uhd 620 nimeona zina nguvu sana bila hata kuweka graphics card unaweza Fanya editor za maana je? kuna chochote nyuma ya hili,
 
jamani nimeuliza swali langu lakin halijajibiwa bado ni kuusu hizi Intel uhd 620 nimeona zina nguvu sana bila hata kuweka graphics card unaweza Fanya editor za maana je? kuna chochote nyuma ya hili,
Hd 620 ni gpu nzuri mkuu, kama nilivyomwambia mdau hapo juu, intel wana Technology inaitwa quicksync, ikiwa software inatumia hii quicksync ina edit video na kurender kwa haraka sana, inaweza hata ku compete na pc za mamilioni, mfano wa software ya quicksync ni final cut ya mac ama Cyberlink kwenye pc, pia adobe kwenye version zao mpya wameanza kuiweka,

Tatizo la quicksync kama ilivyo tech nyengine za hardware acceleration hairetain quality 100%, sababu kuna compression inafanyika, sema kwa project za kawaida kibongo bongo hutoona tofauti, ila kwa wanaotengeneza movies na vitu serious wanatumia software rendering (cpu) kwa kutumia processor zenye core nyingi, hii inatumia resource nyingi ila wanapata quality original.

Na intel gen mpya wametoa gpu mpya zinaitwa Xe, hizi ndio balaa, zinaipita hadi Nvidia 960M, hapa video editing, games na mambo mengine utafanya kwa urahisi tu.
 
dah basi acha tuisubiri hio maana mpaka ije kufika bongo itakuwa mda sana
 
Back
Top Bottom