Nimekupata vizuri sana kakaDesktop ni muhimu sana mkuu kama umeshajitosheleza. Sababu itakuwa mama wa vifaa vyako vyote kama TV, simu, Tablet, gaming console etc. Sio idea mbaya.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nimekupata vizuri sana kakaDesktop ni muhimu sana mkuu kama umeshajitosheleza. Sababu itakuwa mama wa vifaa vyako vyote kama TV, simu, Tablet, gaming console etc. Sio idea mbaya.
lovely lessonComputer nyingi tunazonunua huwa zinatumia processor za intel au amd, lakini ni intel ambaye ametawala sana kushinda amd kwenye computer zetu. Leo nimeamua niandike uzi huu kuhusu hizi processor za intel na namna ya kuzichagua ili kuwasaidia watu wanapotaka kununua laptop/desktop mpya wafanye maamuzi sahihi.
Processor ni nini?
Labda utakuwa unajiuliza kwa nini ukitaka kununua laptop mpya unatakiwa uangalie processor? Nini cha muhimu kuhusu hii processor?
-Kwa lugha rahisi processor ni kifaa ndani ya computer yako kinachobeba maagizo ya program za computer. Maagizo hayo yanaweza kuwa ya kimahesabu, kimantiki, maagizo yanayoingia kwenye computer na yanayotoka.
-jinsi processor inavyokuwa na speed kubwa ndio jinsi maagizo yatakavyofanywa haraka na ndio jinsi program za computer zitakavyofanya kazi upesi.
![]()
Familia ya processor za intel
Intel wana processor za aina nyingi na ni ngumu kuzitaja kwa pamoja, ila wameturahisishia kwa kuzipanga processor zao kwenye familia. Na hii ndio familia yao.
1. Atom processor- processor hizi hutumika kwenye vimini laptop na tablet ni ndogo kiumbo ndio maana hata vifaa vyake ni vidogo, processor hizi hazina nguvu sana na vifaa vyake hukaa sana na chaji.
2. Celeron processor- Haina tofauti sana na atom ila hii ina afadhali kidogo. Inatumika kwenye vifaa vikubwa kuliko atom kama vile laptop kubwa na desktop
3. Pentium- hii ina speed kuliko celeron na atom pia inatumika kwenye vifaa vikubwa.
4. Core 2 duo- hii ni maarufu kwa perfomance yake ya multitasking, inauwezo wakufanya mambo mengi kwa wakati mmoja ila nyingi ni za kizamani.
5. Core i3- hii ni processor latest za intel ni dual core lakini core zake zina perfomance kubwa na pia inakuwa na thread 2 kwenye kila core, ni nzuri kwa wanaotaka perfomance kubwa kwa bei rahisi.
6. Core i5- ya laptop ni dualcore na ya desktop ni quadcore isiyokuwa na thread, software nyingi kubwa duniani zimekuwa optimized kutumia core kama za i5, ni nzuri sana kwa watu wanaotumia software zinazodemand perfomance lakini hawafanyi multitasking.
7.Core i7- hii inakuwa na quadcore processor na thread 8 kwenye desktop na pia inaweza kuwa dualcore kwenye laptop. Hii ndio processor nzuri zaidi kwa watu wa kawaida na inafanya multitasking hata kama software zinademand sana.
8. Xeon- hii ndio processor yenye speed zaidi kwenye processor za intel lakini imekuwa designed kufanya kazi kwenye computer kubwa kama vile server. Unapohost website processor kama hii ndio inayoprocess webpages.
Generation ya processor(muhimu)
Ni muhimu sana kujua processor inatokea generation ipi kuna processor zenye i7 ya 2010 ambazo zipo slow vibaya mno, na pia kuna uwezekano i3 kuipita i7 kwenye perfomance kama zinatoka generation tofauti. Hivyo eneo hili inabidi uwe makini kuepuka kuuziwa mbuzi kwenye gunia. Hivyo unaponunua laptop/desktop ni lazima ujue ipo generation gani la sivyo upo hatarini na hivi ndio namna ya kujua.
- Processor yenye namba inayoanziwa na elfu nne ni fourth generation(4xxx)
Mfano Intel i3-4130.
- Processor yenye namba inayoanziwa na elfu tatu ni third generation (3xxx)
Mfano i3-3130.
- Processor inayoanziwa na elfu mbili ni second generation(2xxx)
Mfano i3-2140
Sishauri kabisa kununua processor ya first generation, mtu unatakiwa atleast ununue ya second generation na pia bei inatakiwa iwe ndogo kwa hii second compare na third/fourth.
Processor ndogo kama atom na celeron zina generation zake ambazo ni
-clover trail
-bay trail
Processor za zamani za atom zilikuwa mbaya sana na zipo slow ila baytrail ikaja kuzipa nguvu na kuzifanya ziwe na perfomance kubwa, hivyo kama unataka kifaa cha atom/celeron make sure processor yake iwe inatoka generation ya baytrail.
Herufi za mbele ya processor(muhimu)
Kama umechunguza mbele ya processor kunakuwa na herufi mbali mbali hizi pia ni muhimu sana kuzijua kwani usipozizingatia unaweza kujuta.
Mfano processor inaweza kuitwa i5-4000m au i5-4000u au i5-4000y je nini kinatofautisha hizi processor?
1. Herufi kwenye processor za desktop.
Bila herufi – hii inakuwa na speed halisi ya processor mfano i7-4770
K- herufi hii inamaanisha processor ipo unlocked na unaweza kui over clock na kuongeza speeed. Processor yenye 3.5ghz unaweza kui overclock ikafika 4ghz. Jina lake linakuwa mfumo huu i7-4770K. ni nzuri sana kwa wanaocheza magame na kufanya rendering.
R- herufi hii inamaanisha processor hii ni ndogo sana na inaweza kutumika kwenye videsktop vyenye umbo dogo hali ya kuwa ina graphic kubwa kama iris pro. Jina lake linakuwa mfumo huu i7-4770R hii ni nzuri kwa wale wenye ofisi ambazo ni safi hawataki mawaya mengi na desktop kubwa kukaa kwenye meza. angalia picha hapo chini uone desktop ndogo.
![]()
S- herufi hii inamaanisha hiyo proceesor wame optimize perfomance mara nyingi wanai underclock kuzuia processor kupata joto sana. Mfano i7-4770 ina 3.4ghz lakini i7-4770S ina 3.1ghz tu, ina maana hapa wamepunguza 300mhz kutoka stock kuja S.
T- herufi hii inamaanisha processor inatumia power ndogo, kwa wale wenzangu wanaotumia luku kama unataka desktop isiokula umeme basi hii ndio yenyewe ila perfomance nayo itapungua kidogo. Mfano wa jina ni i7-4770T
2. Herufi mbele ya processor za laptop(mobile)
Tumeshaona herufi mbele ya desktop, sasa hivi tuangalie herufi mbele ya processor za laptop ambazo pia zinaweza kutumika kwenye home theatre pc (htpc) au wengine wanaita mini desktop.
M- herufi hii inamaanisha hio processor ni mobile, ndio herufi common kwenye processor za laptop mfano i5-4000M
U- herufi hii inamaanisha processor ya laptop inatumia power ndogo hizi processor zinatumika sana kwenye vilaptop vyembamba (ultrabook). Kwa sababu zinakaa na chaji kutokana na kutumia power ndogo, perfomance yake nayo pia ni ndogo. Mfano i5 4250U
Y- hii ni ultra low power yaani inakula umeme mdogo kushinda hata U lakini vile vile perfomance inazidi kushuka nayo mfano i7-4610Y
HQ- herufi hii inamaanisha high perfomance, zinauzwa bei ghali sana na power yake inashindana na desktop. Usije ukajaribu kuieka kwenye mapaja laptop ya design hii maana zinashika moto upesi sana kutokana na quality ya processor. Ni nzuri kwa wale wanaopenda kucheza game, kutumia software kubwa wakiwa kitandani. Mfano ni i7-4700HQ
MQ- herufi hii inamaanisha hio procesor ni quad core. Kama umesoma vizuri juu i5 na i7 za desktop ni quadcore lakini za laptop ni dualcore, hivi processor hii inamaanisha unaweza tumia quadcore kwenye laptop yako kama unataka mfano i7-4900MQ
MX- herufi hii inamaanisha ni xtreme edition, processor hii unaweza kui over clock kama vile K series ya desktop na ina perfomance kubwa sanaaa, ila kuwa makini na mapaja tu.
Mfano i7-4940MX
Huu ndio muongozo wa kununua processor za intel, kama kuna sehemu hujapaelewa unaweza kuuliza nitaelezea zaidi.
Mkuu hizo gen10 zinacheza bila GPU?Ndio mkuu zipo nyingi sema gen ya 10 tofauti na gen nyengine zipo aina mbili
-ice lake
-comet lake
Ice lake yenyewe inaishiwa na G kwa mbele kama G1, G4, G7 etc mfano i3 1005G1
Comet lake inaishiwa na U
Nzuri ni hizo zinazoishiwa na G. Zina graphics nzuri na zinacheza almost games zote.
Zina gpu ila ya ndani imeunganika na processor.Mkuu hizo gen10 zinacheza bila GPU?
Mkuu simu yangu baadhi ya apps zinagoma access mobile data, na-fix vipi hili tatizo.Zina gpu ila ya ndani imeunganika na processor.
Gpu yake ni nzuri sana compare na gen za nyuma.
Na gen ya 11 itakuwa na Gpu kali zaidi.
App zipi?Mkuu simu yangu baadhi ya apps zinagoma access mobile data, na-fix vipi hili tatizo.
Playstore, social networks n.kApp zipi?
Kudownload unaweza? Weka vpn yoyote itafunguka.Playstore, social networks n.k
Ngoja nijaribuKudownload unaweza? Weka vpn yoyote itafunguka.
mkuu nimeangalia Z400 max cpu inayo support ni Xeon W3570 ambayo inapitwa nguvu hadi na pentium za kisasa, kifupi mkuu haifai kwa muono wangu, ni ya kizamani sana toka 2009. z600 pia max cpu ni xeon X5570 ambayo ni mule mule haina maana.Chief-Mkwawa
Samahani Chief,kuna mashine nataka kuchukua kati ya hiii HP Z400 na kuna HP Z600 kwa ajili ya kazi kazi ila Bajeti yangu ninavyoiona imeegemea zaidi kwenye Z400.
Naomba nisaidie elimu kidogo ya faida na hasara za Z400 na je naweza ifanyia upgrade atleast ikajitahdi tahdi kuchuana na Z600,sijajua kuhusu z600 ila nahisi ni bora zaidi sema mimi ki uwezo nmeishia kwenye z400.
Je nikaichukue Z400 au haifai tena kwa dunia tuliyopo sasa? (kama haifai) je unanishauri nichukue mashine gani yenye uwezo uliotukuka kama workstation?
Natanguliza shukurani zangu kwako kwa misaada ya kimawazo/ushauri unayo nipatia/tupatia humu jukwaani,naomba ktk hili pia nikupe muda wakusumbua ubongo wako kunishauri kitu yenye itanifaaa..
Napokea idea na mawazo mengine utayoamua kunipatia,maana najua umeshajua nataka mashine ya aina gani na ni mtu wa matumizi kiasi gani.
Asante.
Tafuta i3 gen ya 6 ama 7 used unapata kwa hii budget.Kwa 400k - 450k PC gani ita nifaa kwa matumizi ya kawaida tu
sasa chief hebu nisaidie mashine gani itaweza faaa yenye uwezo wa kupokea internal HDD zisizopungua 4 na kupokea dvd rom mbili?mkuu nimeangalia Z400 max cpu inayo support ni Xeon W3570 ambayo inapitwa nguvu hadi na pentium za kisasa, kifupi mkuu haifai kwa muono wangu, ni ya kizamani sana toka 2009. z600 pia max cpu ni xeon X5570 ambayo ni mule mule haina maana.
hizi workstation zimejaa kibao kibongo bongo wengi hawazijui na hawana time nazo, tafuta zenye xeon kuanzia gen ya pili kupanda juu, kwa hizi HP z series naona kama namba ya kati inamaanisha gen ya kisasa zaidi z410, z420, z440 etc
alternative achana nazo, maana hazina gpu ya ndani mpaka ununue dedicated gpu na pia zinakula umeme kama pasi, unaweza ukajipa stress zisizo na maana, desktop za kawaida zina nguvu ya kutosha kuliko hizi workstation za kizamani.
Sitaki tumia External Drive wala External DVD romsasa chief hebu nisaidie mashine gani itaweza faaa yenye uwezo wa kupokea internal HDD zisizopungua 4 na kupokea dvd rom mbili?
mbona zile desktop kubwa (full tower) zinaweza hii kazi?Sitaki tumia External Drive wala External DVD rom
natamani vitu vyote viwe ndani ya CPU kazi yangu iwe
kujaza tu HDD lakini pia iweze kuhimili kazi kwa muda mrefu
Chief-Mkwawa
Hii maana yake ni lazima nichanganye HDD za 3.5 na 2.5mbona zile desktop kubwa (full tower) zinaweza hii kazi?
kwenye specs angalia 5.25 inch bay hio unaweka mlango wa cd na 3.5 ama 2.5 inch hio unaweka hdd ama mlango mdogo wa cd.
mfano hizi specs za dell optiplex 9020
View attachment 1619018
ina 5.25 inch bay 2 ina maana unaweza weka milango miwili ya cd
pia ina 3.5 inch milango miwili hapa zinakaa hdd kubwa 2 za desktop
2.5inch nazo ni mbili, kunakaa hdd mbili ndogo za laptop.
![]()
hata ukiangalia kwa mbele chini ya mlango wa cd unaona nafasi imeekwa kama unataka kuongeza mlango wa pili wa cd
Ki theory mkuu hdd ya 2.5 na 3.5 ni sawa, sababu zinatumia connector moja, hivyo kama una space ndani ya Desktop unaweza kuweka hata ya 3.5 ila itakuwa loose,Hii maana yake ni lazima nichanganye HDD za 3.5 na 2.5
niweke mbili kwa mbili,sasa chief "what if" sitaki kutumia
HDD za 2.5 (zile za laptop) nataka internal nitumie 3.5 ONLY
na option za ROM ziwe mbili hivyo hivyo kama picha inavyojionyesha kwenye hiyo optilex 9020.
Mkuu kwa budget hii ni sahihi kuchukua hii PC au jamaa ana bei za ajabuNdio mkuu zipo nyingi sema gen ya 10 tofauti na gen nyengine zipo aina mbili
-ice lake
-comet lake
Ice lake yenyewe inaishiwa na G kwa mbele kama G1, G4, G7 etc mfano i3 1005G1
Comet lake inaishiwa na U
Nzuri ni hizo zinazoishiwa na G. Zina graphics nzuri na zinacheza almost games zote.
Hii pc ina run gta V, sema tafuta angalau i5 same generetion.Mkuu kwa budget hii ni sahihi kuchukua hii PC au jamaa ana bei za ajabu
Pia kwa 500k naweza pata PC ya aina gani nzuri ambayo ita run GTA V.