1. Hizi Gpu zina series mfano kwa Nvidia utakuta 1030, 1050, 1060, 1070, 2060 etc same kwa Amd na intel
Gpu za intel ni low end zinapambana tu na GPU za Nvidia ama Amd za bei rahisi.
Kuhusu Amd vs Nvidia ni kama wanafanana Sema Nvidia Ana drivers nzuri zaidi most of time utakuta Gpu zake zinatumika kwenye gaming machine wakati Amd yeye Gpu zake zina nguvu kwa price point fulani na GPU zake Mara nyingi hutumika kwenye Uchimbaji crypto currency.
2.mara nyingi laptop zinazowekwa Gpu za Nvidia ama Amd zinakuwa laptop high-end za bei ghali kama vile gaming laptop ama laptop za proffesional mbalimbali.
3.huwezi kutoa Gpu ya Intel maana imeungana na cpu na pia huwezi toa Ya Nvidia maana umegundishwa kwenye motherboard. Na vile vile huwezi kuzi upgrade. Ipo option ya nje kama laptop Ina port ya pcie ama thunderbolt unachomeka Gpu ya nje. Ila case tu ya hio Gpu inaweza Fika laki 4 pamoja na GPU itaku cost.
4.kuna umuhimu mwingi tu, kuna hizi cad softwares kama Autocad, kufanya video editing, browser siku hizi zinatumia Gpu,
Kuangalia video za resolution kubwa, ku drive monitor ama display yenye resolution kubwa etc
5. Gpu kubwa kabisa ya Intel inaitwa Xe na inapatikana kwenye gen yao mpya ya 11, kwa Nvidia Gpu kubwa ni Rtx 3080.