1. Kutoka i3 mpaka i5 kwenye desktop Mara nyingi core zinaongezeka, mfano unakuta i3 ina core 4 na i5 ina core 6, kwenye laptop ni Hivyo Hivyo Sema imeanza hivi karibuni kuanzia gen ya 8. Gen ya 2 mpaka 7 utofauti wa baina ya i3 na i5 ilikuwa ni turbo clock tu, i3 haikua na turbo.
2. Gen kwa gen kunakuwa na kitu kinaitwa Architecture ya hio generation, mfano gen ya 11 inaitwa Tiger lake na sifa zake ni kwamba ina Gpu zenye nguvu za Xe, ina perfomance kubwa, Artifical intelligence etc Hivyo vitu vyote hivi utavikuta kwenye i3 mpya ila ya zamani huvipati.
3. Utofauti baina ya i5 kwenye same generation Mara nyingi ni clock speed tu, unakuta moja ina 2.5ghz nyengine Ina 2.6ghz etc.