1. kuhusu UHD graphics
mkuu kuanzia gen ya 7 mpaka ya 10 baadhi ya cpu zinatumia tu gpu moja ni ile ile intel hd 620/630, cpu yako sema haitumii gpu hio sababu ni ice lake, generation ya 10 imegawanyika mara mbili ice lake ambayo ni 10nm na canon lake ambayo ni 14nm
kuanzia hii cpu yako sasa yaani ice lake kwenda mbele, gen ya 11 tiger lake na 12 alder lake etc intel officially anaweka gpu kali, maana na yeye amejiingiza kwenye utengenezaji dedicated gpu kama amd na nvidia.
ya kwako wewe inayoishiwa na G1 ni ndogo zaidi (sema kali kushinda gen zote 9 kushuka chini), kuna g4 na g7 ambazo ni nzuri zaidi.
hivyo sasa hivi badala ya kuangalia intel hd 4000 ama hd 530 unaangalia hizo G kwa mbele G1 ndogo g4 size ya kati na G7 kubwa.
2. kuhusu cpu kuna kitu kinaitwa turbo na base clock
base clock ndio hio 1.2ghz hii manufacture anakuhakikishia unaipata na hio turbo 3.4ghz unaipata pale tu cpu ikiwa haina joto sana, mfano laptop yako ina cooling nzuri, umeiweka mahala kuna upepo wa kutosha na feni halijazibwa basi itarun hio 3.4ghz, ila sijui umeweka laptop juu ya godoro, shuka limeziba feni inachemka vibaya basi ujue itadrop hadi 1.2ghz.
most of time laptop kubwa inch 14 kupanda zinasustain turbo, tablet na vilaptop vidogo ndio vinashuka 1.2ghz