Ni ajali lakini bima waweza kuichukulia ni uzembe kwa mwenye gari ...na ukikuta hugo Dogo hata licence hana ndio kabisaa bima watakuwa wamepata kigezo cha kuhepa mzigoKwanini umesema hivi? Nadhani mwenye gari hiyo anashindwa kwa mwaka kulipa 980K au 1.2mill iwe ulinzi wake kwa emergency kama hizi?
Then kama analipa hivi kwanini isiwe msaada kwake?
kwa hili lazima ajifanye kung fu snake monkey shedo aiseeUtamu zaidi ni kwamba aligongana na gari nyingine pia pale mbele ya kona ya morena njia ya kuelekea Makulu/UDOM
Ukiangalia vizuri kuna brevis nayo imebinuka tako juu
Kwahiyo Ranger+ Brevis lazima ujifanye kung fu snake monkey shedo
Hajawehuka mtu hapo...pigeni viboko..Video hii hapa chini inaonyesha akiwa amewehuka, inasikitishaView attachment 1877604
Haina bima hiyo gariWengi naona wanasema wanasema gari haina bima ila inayo tena bima kubwa kupitia system mpya ya tiramis unaiona fresh imekatwa kampuni ya UAP.
Changamoto kubwa nayo iona ni dogo kutokuwa na leseni hii itamkosesha mwenye gari malipo.
View attachment 1878916
Mkuu nimekuwekea attachment hapo huna macho?Haina bima hiyo gari
Achana nae huyo hivi ni nani atasubutu kutembeza gari ya thamani kama hiyo bila bima?Mkuu nimekuwekea attachment hapo huna macho?
Mawazo yako na ya jamaa yana ka ukweli lakini mkuu lazima ujuwe ya kwamba licha ya hilo gari kuwa na thamani ya zaidi ya 100 mil ila mmiliki unakuta analiona kama wewe unavoona IST tu. Lina thamani kwake ndio lakini sio kiasi cha kumfanya awe nalo makini hadi asioshe car wash japo ni uzembe kumpa muoshaji funguo. Unaweza ukawekewa hata madawa ya kulevya then kesho yake Takukuru,pccb nk wako nyumbani kwakoNina mawazo kama yako. Ila Tanzania kwa watu kujifanya ma-boss ni kiboko. Hivi inakuwaje mtu anashindwa kuosha gari mwenyewe? Na mwenye gari utakuta pengine ana bonge la kitambi, akitembea hatua mbili anahema kama chura! Anyways, hata kama huwezi kuosha mwenyewe kwa nini ulipeleke sehemu uwaachie na funguo? Kwa nini usisubiri mpaka wamalize! Nasema hivi kwa sababu Tanzania watu wengi wala hawako busy kiasi cha kushindwa kuosha gari wenyewe au kusubiri. Wengu inakuta analiacha sehemu hivyo anakwenda bar kunywa.
Nimemuwekea attachent hapo. Tira walianzisha mfumo mpya wa tiramis unaotumia e-stickers ambao sikuhiz hawatoi physical stickers za kubandika.Achana nae huyo hivi ni nani atasubutu kutembeza gari ya thamani kama hiyo bila bima?
ukweli mchungu ni kwamba mleta habari umemsababishia jamaa apoteze 120m zake bila kujua na huenda akawa anakulaani wewe na wenzako.Habari wakuu, tunakumbushana kuweni makini na waosha magari mnapowaachia funguo wakati wa kuosha dinga zenu, Jamaa kapeleka gari aina ya Ford Ranger carwash huku Dom kaacha funguo na kuondoka, mwoshaji kamaliza akachukua ford ranger ya Mteja kwenda kutamba nalo, kilichotokea kala mzinga ndinga haitamaniki yeye kapata uchizi wa ghafla.
View attachment 1877570View attachment 1877572
View attachment 1877571
Huyu jamaa mwenye kibukta ndo mwoshaji, hiyo video ndo inaonyesha kichaa cha ghafla alichopata, sipati picha mmiliki ana hali gani hiki ndo ukute alikuwa na third party tu.
View attachment 1878612
Zaidi ya wiki haukufa mkuu??Iliwahi nitokea miaka 12 iliyopita. Mwoshaji baada ya kuosha alienda kukata mitaa na dinga yangu...TOYOTA RAUM NEW MODEL, enzi hizo Dar nzima zilikuwepo mbili tu...Nilipagawa balaa sikula chakula zaidi ya wiki!