Muosha Magari apatisha ajali gari lenye thamani zaidi ya Milioni 100. Akutwa anaruka sarakasi

Muosha Magari apatisha ajali gari lenye thamani zaidi ya Milioni 100. Akutwa anaruka sarakasi

Kwanini umesema hivi? Nadhani mwenye gari hiyo anashindwa kwa mwaka kulipa 980K au 1.2mill iwe ulinzi wake kwa emergency kama hizi?

Then kama analipa hivi kwanini isiwe msaada kwake?
Ni ajali lakini bima waweza kuichukulia ni uzembe kwa mwenye gari ...na ukikuta hugo Dogo hata licence hana ndio kabisaa bima watakuwa wamepata kigezo cha kuhepa mzigo
 
Wengi naona wanasema wanasema gari haina bima ila inayo tena bima kubwa kupitia system mpya ya tiramis unaiona fresh imekatwa kampuni ya UAP.
Changamoto kubwa nayo iona ni dogo kutokuwa na leseni hii itamkosesha mwenye gari malipo.

Screenshot_20210803-191414.jpg
 
Nina mawazo kama yako. Ila Tanzania kwa watu kujifanya ma-boss ni kiboko. Hivi inakuwaje mtu anashindwa kuosha gari mwenyewe? Na mwenye gari utakuta pengine ana bonge la kitambi, akitembea hatua mbili anahema kama chura! Anyways, hata kama huwezi kuosha mwenyewe kwa nini ulipeleke sehemu uwaachie na funguo? Kwa nini usisubiri mpaka wamalize! Nasema hivi kwa sababu Tanzania watu wengi wala hawako busy kiasi cha kushindwa kuosha gari wenyewe au kusubiri. Wengu inakuta analiacha sehemu hivyo anakwenda bar kunywa.
Mawazo yako na ya jamaa yana ka ukweli lakini mkuu lazima ujuwe ya kwamba licha ya hilo gari kuwa na thamani ya zaidi ya 100 mil ila mmiliki unakuta analiona kama wewe unavoona IST tu. Lina thamani kwake ndio lakini sio kiasi cha kumfanya awe nalo makini hadi asioshe car wash japo ni uzembe kumpa muoshaji funguo. Unaweza ukawekewa hata madawa ya kulevya then kesho yake Takukuru,pccb nk wako nyumbani kwako
Mimi home mzee hapendi kuosha gari car wash huwa anawapa vijana wakaaji wa Home au sisi tukiwa likizo, alikuwa anaibiwa sana speaker nk akipeleka car wash

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mambo mengine unasamehe tu mie niliwah mpa dogo anirekebishie taa pikipiki yangu ya kichina niliyoununua kwa taabu na ina wiki mbili tu dogo kapanda kuzunguka mtaani na vile ni kubwa akaishia kudondoka ,kuvunjika yeye mkono ,kuvunja taa zote na usukani.

Hata sikuona haja ya kumhukumu niliamua kuiweka store kwa miez kadhaaa maana nilihisi ilikuwa na lengo la kuniua mimi .
 
Actor iyo 😂 mwenye ndinga kaingizwa town masikini.


Mwenye gari namhulumia sana, si ajabu ndinga ina deni.
 
Habari wakuu, tunakumbushana kuweni makini na waosha magari mnapowaachia funguo wakati wa kuosha dinga zenu, Jamaa kapeleka gari aina ya Ford Ranger carwash huku Dom kaacha funguo na kuondoka, mwoshaji kamaliza akachukua ford ranger ya Mteja kwenda kutamba nalo, kilichotokea kala mzinga ndinga haitamaniki yeye kapata uchizi wa ghafla.

View attachment 1877570View attachment 1877572
View attachment 1877571
Huyu jamaa mwenye kibukta ndo mwoshaji, hiyo video ndo inaonyesha kichaa cha ghafla alichopata, sipati picha mmiliki ana hali gani hiki ndo ukute alikuwa na third party tu.

View attachment 1878612
ukweli mchungu ni kwamba mleta habari umemsababishia jamaa apoteze 120m zake bila kujua na huenda akawa anakulaani wewe na wenzako.

sababu hyo gari ni lazma iwe na bima kubwa ,hivyo kama angecheza vizuri na trafik ungeandalkwa tu mchoro vizuri akapeleka bima akalipwa hela yake bila wasi wasi.

but kwa taarifa mlivyozitoa kampuni ya bima watakuwa tayari walishaipata hyo gari na historia yake yote hivyo jamaa hapo ajiandae tu kula hasara
 
Yaani hii story ilivyo trend hata kama jamaa alitaka afabricate evidence na kila kitu alipwe itashindikana sasa, maana wengine wanakagua bima na hata gari sio yao[emoji23] ndio wameiona kwenye picha bongo kazi kweli kweli
 
Mzima huyo.

Anaigiza kurukwa na akili ili kuua soo na sarakasi zake za kupiga beki
 
Back
Top Bottom