Muro kakosea kwenda Yanga, Yanga nayo imekosea kumpata Muro

Hujamuelewa Muro wewe!! Amesema atamfukuza Ngasa!.. yaani yeye kama yeye wala hajatumwa kutoa tamko hilo
Kama amesema atamfukuza Ngasa as an individual hapo sawa naweza kuhoji mamlaka ameyatoa wapi otherwise kama amesema kwa niaba ya taasisi yupo right
 
unadhani ni busara kuita waandishi wa habari kuzungumzia makato ya deni la laki tano mlilokubaliana kwenye vikao vyenu vya ndani? busara zenu ndio zimeishia hapo?
Deni sio laki 5, Ngasa alikopa pesa bank, mwajiri wake ambaye ni Yanga akamdhamini kwa makubaliano ya mshahara wa Ngasa upite bank kwa makato ya laki tano kila mwezi (ambayo wewe ndio umesema anadaiwa laki tano) ama kwa makusudi ama vipi, mwajiri ambae ni Yanga hakupeleka mshahara wa Ngasa bank kwa muda wa mwaka mmoja. Bank wakaiandikia Yanga ambae ni mwajiri na mdhamini wa Ngasa na kuchukua hatua ya kuingiza mshahara wa Ngasa bank na makato yakawa makubwa kwa kuwa mwaka mzima deni halikulipwa. Ngasa akatangaza mgogoro na Yanga (migogoro yetu watz si unaijua ile ya kusema chini chini wakati ukweli wewe ndio tatizo)

Walichofanya Yanga wapo sahihi kwa kuwa wamekuja kuufahamisha umma wa watz kwamba uongozi uliopita haukuingiza mshahara wa Ngasa bank hivyo ukasababisha na Ngasa kukwepa kulipa deni wakti hata kama alikuwa anachuwa mshahara kwa cash au kupitia bank nyingine bado alikuwa ana uwezo wa kupeleka hilo deni. Uongozi mpya umeingia madarakani ukakutana na barua toka bank na kwa kuwa Yanga ni taasisi huwezi kusema tatizo lilitokea uongozi uliopita bali walichofanya ni kuchukua hatua.

Walikuwa sahihi kwa kuwa mhusika alinununa na kutaka kusambaza sumu kwa watz hivyo Yanga walikuja kuweka rekodi sawa kwani Ngasa alichukulia huo mwanya wa kutokulipa kutokana na timu zetu nyingi zinaendeshwa kisiasa pia walishazoewa kulelewa na hapo alitegemea mapedeshee wa club wangemlipia kama alivyokula ela za usajiri mara mbili mwaka juzi I think. HUYO NI HURUKA YAKE NA TUKIWAFANYIA HIVI WACHEZAJI WETU TUTAWAJENGA NA KUWAFANYA MIKOPO WANAOCHUKUA KUITUMIA KWA MALENGO YANAYOKUSUDIWA
 
Rage akukosea kuwaita mbu3

Mkuu wa chama langu ngoja niwakumbushe jambo hawa mikia. Mwishoni mwa miaka ya 1980 au mwanzoni mwa miaka 1990, Yanga tulikuwa na mechi na mikia. Mikia waliweka kambi Njuweni pale Kibaha. Pale kambini ikaja gundulika mmoja wao analiwa (Voda) AKA Tigo. Na kwa mujibu wa vyombo vya habari mtu mwenyewe ambae wachezaji walikuwa na shaka nae kutatuliwa Marinda, ni yule jamaa sasa hivi yupo kwa wachimba vito kule akiwa kama kocha.Walipokuja uwanjani shamba la bibi ( uwanja wa taifa wa zamani) tukawapiga 3-1. Hiyo mechi nilikuwa jukwaa la Main stand, tulipowapiga bao la 3 kuna Yanga Wenzetu walikuja na Shanga pale uwanjani (Shanga hizi zinazovaliwa na kina dada kurembesha viuno vyao na kuleta ladha ya unyago) tukaanza kuwamwagia Shanga mikia....unajua Kwanini tuliwamwagia Shanga?!! Kuwakumbusha yale ya Njuweni Kibaha.Mpaka leo Lunyasi wana shanga viunoni mwao tulizowavisha miaka hiyo. Nikimsikia mtu anajiita " SIMBA MSHABIKI WA DAMU" namuonea huruma. Mke wangu ndio hao hao Lunyasi, lkn simuonei huruma maana kuvaa shanga wajibu wake.POLENI SIMBA. Sijui mtakuja vua lini zile Shanga tulizowavisha kuadhimisha kuliwa AIRTEL yake yule jamaa yenu na kipigo cha 3-1 juu yake.
 
wazee wa mabonanza aka mikia fc, ndo staili yao ya kujifariji wanashindwa kuizungumzia club yao wamekazana kupiga domo kuizungumzia YANGA..wanashindwa kuhoji kwa nini hanspope amegeuka kuwa msemaji wa mambumbumbu, pengine labda mpaka rage atengue jina alilowaita wanazi wa mikia "mambumbumbu" ndo labda ufahamu utawajia japo kidogo.....Aisee rage aliona mbali sana na alijua Ni aina gani ya watu anaowaongoza hadi kufikia kuwaita mambumbumbu
 
Jana nimemsikia ktk Sports Leo ya Radio One, nikashangaa jinsi anavyoongelea suala la Ngassa, anaongea kwa mamlaka makubwa kana kwamba ana uwezo na mamlaka juu ya Ngasa.
Hivi kati ya Ngasa na Muro nani yuko juu ya mwenzake? AU Muro ndiyo mwajiri wa Ngasa?
 
bujashi25

Mbumbumbu hawezi kumpiga mtu bao 5 bila, lazima Yanga watakuwa mambumbumbu waandamizi daraja la I.
 
Last edited by a moderator:
Mbumbumbu hawezi kumpiga mtu bao 5 bila, lazima Yanga watakuwa mambumbumbu waandamizi daraja la I.

Ujerumani imeipiga brazil 7_0,man u ilipigwa 6 na mancity,arsenal ilipigwa 8 na man..nk nk hao wote hawazungumzii hivo vipigo coz wanajua point ni 3 tu walizopata...ww mbumbu ndo unazungumzia goli 5 miaka nenda rudi alafu unasahau kwamba upo nafasi ya9..pole
 
Kama magoli 5 ni miaka nenda rudi je bao 2 bila nazo ni nenda rudi? Kweli mbumbumbu mwandamizi Daraja la I mko fiti.
 
Jodoki Kalimilo

Mwenye jukumu la kupeleka hizo hela benki ni nani? Je ni Ngasa au ni Yanga?
 
Last edited by a moderator:
Mwenye jukumu la kupeleka hizo hela benki ni nani? Je ni Ngasa au ni Yanga?
Mwenye jukumu ni Yanga kama mdhamini lakini bado haikuondolei kinga kwa kuwa upo na hujafa, wala hujatoroka na unafahamika utawajibika na bank watamfuata mdhamini ambae ni Yanga na mwisho wa siku itaonekana kuna mtu amefanya uzembe atawajibishwa lakini mwisho wa siku wanarudi kwako yaani Ngasa, unless ulikuwa hulipwi mshahara vinginevyo itaonekana ni deal kati ya mchezaji na afisa wa Yanga. Na ndio maana Yanga waliamua kupeleka mshahara wake bank na makato yakaongezeka, ila kama angeingia mitini yanga wangewajibika kwa kuwa walikuwa hawapeleki mshahara wake. Sema tu kwa kuwa ni vijana na wachezaji wa mpira wanapewa heshima maalumu kama hiyo ya kukaa na kuamua kama walivyofanya Yanga, lakini ungekuwa ni Masuke au mie Jodoki ambao hatujaonyesha mchango kwa Taifa kila mwananchi atutambue, lazima methodology ya kudai deni ingebadilika ikiwa sambamba na kukamata mali zetu na wala miezi miwili isingekatika bila kutusumbua yaani mwezi wa kwanza tu mshahara umekata jamaa hao
 
Last edited by a moderator:
Jodoki Kalimilo

Kuna sehemu nimesoma, Ngasa alikopa milion 45 benki kwa makubaliano kwamba yeye alipe laki 5 kila mwezi na timu yake ilipe laki 5 kila mwezi, lakini baadaye timu ikamgeuka na kuanza kumkata milioni moja, Ngasa akakubali sasa yeye kilichomuudhi zaidi ni pale ilipoonekana kwamba hela ilikuwa inakatwa halafu haiendi benki kwa zaidi ya mwaka sasa na ndo kilichosababisha aanze kukatwa milioni mbili kila mwezi ni kama mshahara wake wote unachukuliwa.

Kama hali ndo hiyo kwa nini aendelee kucheza mpira na huyo aliyekuwa na jukumu la kupeleka hela kwa nini hakupeleka na kama Yanga alikuwa mdhamini tu kwa nini wasingefungua akaunti benki husika na mshahara wake wakawa wanaupeleka huko halafu yeye anapata salary slip na benki wanakata hela yao juu kwa juu.

Bado Ngasa ana haki ya kulalamika na malalamiko yake makubwa ni kwa nini wakate hela yake milioni moja halafu wasiipeleke benki? Hayo mengine ya kulipiwa laki tano anaweza kusamehe na kusema alitapeliwa ila kwa sasa kukatwa mshahara wote na usipate chochote hata kama ningekuwa mimi naachana na hiyo kazi na hilo deni tutajuana mbele kwa mbele.
 
Last edited by a moderator:
Masuke

Si unajua habari zenyewe zinakuja nusu nusu na kila mtu anasema lake, na yule anaepaza sauti ya juu ndio anaonekana yupo right, vinginevyo ahsante kwa kunihabarisha
 
Last edited by a moderator:
Jodoki Kalimilo

Pamoja na kuisoma sehemu hiyo habari lakini pia hata jana kuna radio nadhani ni Efm walicheza sauti ya Ngasa akilalamika kiasi hicho cha hela kukatwa na nadhani hii inaweza kuwa ni bahati kwa Ngasa kutokana na yale magoli aliyowafunga Mtibwa inabidi hayo magoli ayatumie kama kichocheo na ikitokea amefunga pia kwenye mechi nyingine ndo inabidi akoleze moto na kwa sababu ni haki yake lazima watafikiria mara mbili mbili na akiona hawafikirii kuhusu madai yake mkataba wake umebaki mfupi anaweza kuanza kujivunja tu dakika mbili wanakutoa umeumia

ila ukiongea na magazeti unawaambia unaumia kwa sababu hauko sawa kisaikolojia na hivyo anashindwa kuwa timamu kimwili na kushindwa kucheza mpira kwa ushindani.
 
Last edited by a moderator:

Sisi Ma-Tanzania kum'may zetu hatuna akili bongo zetu zimejaa makamasi! Hela ukope Wewe halafu ukat...m...b..ee uje umsusie mwajiri deni? Hayo ndo yalikuwa makubaliano? Sijawahi kuiona popote eti mdhamini wako kwenye mkopo ndo akipe deni lako! Kosa la Muro ni lipi Wewe Mbwiga Wa Mbwiguke? Muro kaeleza ukweli ulivyo Wewe ulitaka aeleze nini? Hapo mikia wamepata kiki na wamchukue! Machezaji yetu yanasumbuliwa na kutokuwa na elimu, hili toto lingekuwa limesoma wala lisingekuwa linahaha hivyo! Nilipenda uchambuzi Wa Shafii Dauda yeye alihitimisha kwa kusema makato hayo ndo yanamfanya Ngassa apige kelele! Mleta mada unashindwaje kutumia akili kidogo aliyokuachia Rage!??
 
Job K

Malalamiko ya Ngasa ni ya msingi sana; kwanza wamekiuka makubaliano ya kumlipia laki tano wakati mwanzoni walikubali(ningekuwa mimi hilo nisingeona kama ni tatizo, ningehesabu kwamba nimetapeliwa) na mbili ni kwamba pamoja na kukataa kumlipia hiyo laki tano ikalazimika yeye mwenyewe akatwe milioni ambayo ilikuwa haipelekwi benki, amekatwa milioni zaidi ya mwaka benki haiendi na kwenye mshahara haipo halafu unataka Ngasa akae kimya hiyo ni haki kweli?
 
Last edited by a moderator:
Mijitu Mambo yasiowahusu Mnatakia Nini?akimfokea Akimtusi inahuuuu!acheni ubarmed wenu Mbona nyie hatumjui PR wEnu mara haz popo mara sijui mwenyekiti nae msemaji Jadili huo ufundi seremala wenu kuchonga midroo tu hatuoni hata kabati maaaaaamaaaninia
 
Masuke

Kama ana ushahidi wa hayo makubaliano na hiyo hela kwamba ilikuwa inakatwa haipelekwi benki anasubiri nini kufungua kesi mahakamani ili apate haki yake? Tuache kutetea uvivu, kama hakuna ushahidi wa maandishi anapiga kelele kwenye vyombo vya habari ya nini? Kama hana mkataba wowote wa hayo makubaliano apige kimya maana ndo elimu yetu wa-TZ hiyo.

Mambo makubwa kama hayo mnakubaliana mitaani tena kwa mdomo? Shame on him, shame on you guys!! Maana kama amekatwa laki 5 kwa mwaka mzima maana yake ni milion 6, je! Ana ushahidi kwamba hela ilikuwa inakatwa? Hajui ni wapi atapata haki yake?

Mimi nasema lazima huyu jamaa alikuwa anakunja mkwanja anapiga kimya akitegemea mdhamini atalipa, tena ukute alikuwa anajisifia hadi miataani kwamba kawapiga goli Yanga na benki maana hawakati fedha ya mkopo!!

Alipe bwana aache kulalamika! Kama hiyo hela alikopa halafu haikumpa manufaa yoyote ndo majuto hayo!!
 
Last edited by a moderator:
Job K

Naona wewe umeamua kuside na Yanga katika kudhulumu haki ya Ngasa, jana Ngasa kaeleza na Jerry Muro hakukanusha badala yake akasema uongozi utakaa na Ngasa na kuyamaliza.

Halafu iliyokatwa sio laki tano tu bali ni milioni moja, hiyo ya makubaliano hata yeye Ngasa alikubali yaishe na akakubali wamkate hiyo milioni moja sasa badala ya kuipeleka benki ikaservice mkopo wenyewe wanajua walikokuwa wanaipeleka na Yanga ndo walikuwa na jukumu la kupeleka hiyo hela, watendaji wapya wameingia wakakutana na barua ya CRDB inawataka wapeleke hela na kwa sababu kulikuwa na malimbikizo mengi wakaanza kukata milioni mbili ambayo ni kama mshahara mzima.

Kwa walichomfanyia ngasa sio sawa, mmekataa kumlipia deni lake basi pelekeni benki ambayo mnaitoa kwenye mshahara wake na kama hamtaki kupeleka basi mlipeni mshahara wake wote apeleke mwenyewe.
 
Last edited by a moderator:
Job K

ngasa alikubaliana na nani mambo hayo?...naona hujui hata kinachojadiliwa hapa! upeo wako umegota kwenye tope la uwanja wenu
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…