Muro : Pesa za CAF tutailipia Simba SC deni la Musoti

Muro : Pesa za CAF tutailipia Simba SC deni la Musoti

Kwani ule ujenzi wa Jangwani Complex bado upo kwenye hatua ya upembuzi yakinifu? Kwa nini hizo hela wanazotaka kumlipa Mosoti wasianze kumwaga kifusi pale Jangwani ili wajenge huo uwanja wenye hostel na kila kitu?
 
Msemaji wa klabu ya Yanga Jerry Muro amesema watawalipia klabu ya Simba deni wanalodaiwa na Mkenya Mosoti kwa kuwa ghawataki Simba washuke daraja na mpira ni umoja na kusaidiana,

Ikumbukwe kuwa Simba waliamrishwa na FIFA walipe deni hilo la sivyo watashushwa daraja.
Msikilize Jerry Murro hapa
 
Jerry Muro ananirudisha enzi zile makabila yetu jinsi yalivokuwa yakitaniana hadi misibani........yaani mtu una uchungu wakufiwa lakini mtani wako anakuja kukuongezea uchungu zaidi na hauwezi rusha ngumi maana unajua na wewe ipo siku utarudisha ama mwenzako ndo anrudisha hivyoo wakati wako wakutania ulishapita
 


Klabu ya Yanga kupitia kwa mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano Jerry Muro, wamesema wako tayari kuisaidia Simba kulipa deni la Musoti ili klabu hiyo ya Msimbazi isishushwe daraja.

Muro amsema, wako tayari kuichangia Simba kulipa deni lao linalowakabili ili FIFA isiishushe daraja na wao wakakosa pointi sita katika msimu ujao wa VPL.

“Tunaomba watuletee barua na karatasi za malipo za yule mchezaji ili sisi tu-process malipo kwa sababu tuliahidi tukifika hatua ya makundi ya michuano ya Afrika tutawasaidia kulipa deni lao. Sisi hatukubali Simba ishushwe daraja kwasababu pale tunapointi sita za wazi kwenye msimu ujao wa ligi”.

“Sasa kwanini tukose pointi sita ambazo tunaweza tukazitetea zikabaki. Inaweza ikashuka Simba halafu ikapanda timu ya Milambo ya Tabora halafu ikatusumbua sana, sisi tunazihitaji ponti sita za Simba na tulisema tukifika hatua ya makundin tutawalipia”.

“Ili tuweze kufanya transaction na kwakua hela hii inalipwa kupitia FIFA, tutawaandikia CAF barua ya kufanya malipo kwenda FIFA ili kuisaidia Simba isishuke daraja. Mhasibu wetu anasubiri karatasi za malipo na kwakua malipo yanafanyika kwa dollar, tutawaandikia CAF watoe kiasi cha pesa kwenda FIFA kwa ajili ya kuwasaidia ndugu zetu”.

Simba imeelezwa kupuuza kumlipa mchezaji Donald Musoti Omanua kwa wakati tangu mkataba wake uvunjwe. Musoto aliyesajiliwa na Simba msimu wa 2014/15 na kuachwa alilalamika FIFA ambayo iliona ana hoja na hivyo Simba kutakiwa kumlipa dola 29,250 (sawa na Sh 62.8 milioni) na kiasi kingine anachodai ni Dola 600 (Sh 1,290,000) zilizobaki katika usajili ambapo jumla yake ni Sh 64.2 milioni. Pia Mosoti anamlipa Mwanasheria wake dola 2,000 (Sh 4.3 milioni) kwa ajili ya kusimamia kesi hiyo.

Hivi wachaga nao wanaimba taarabu? Huyu Jane muro an anafanya nizidi kuchikia yanga, hachoki kuimba chimba chimba chimba, akilala chimba, akiamka chimba, aaaaaaa too much is harmful bhana.
 
Wapi Haji Manara?
Barua za viporo alipeleka mwenyewe hadi kwa Nape. Na hii, apeleke mwenyewe ofisi za Yanga! Teh teh teh
 
Aaaaa hii sasa kalj kuliko!amenikumbusha wazili wa habar wa Irak pind inapigana na mmarekan wakat wa utawala wa Bush jamaa alikua na bit balaa.Saf sana Jmulo
 
Wanalamba shilingi ngapi?
...kwa kuingia tu hatua ya makundi wana uhakika wa kupata milioni 320 km watakuwa wa mwisho kwenye kundi, milioni 513 km watakamata nafasi ya tatu!, wacha watutukane tu,mpk yale matapeli yetu yaondoke pale msimbazi!
 
Kwanza huu mpira ameanza kuushabikia lini? Maana tunasikia habari zake zaidi kuliko hata za Yanga. Too much is harmful, lkn ni vzr hata yeye anaonekana kuanza kulielewa na kuchukua hatua stahiki kama ile ya jana ya kujiombesha msamaha.

Wakati watu wote nchini issue kubwa ilitakiwa iwe ni Yanga kufuzu lkn Simba ndio inatajwa zaidi kufanya kwake vibaya kwenye ligi as if imeshuka daraja
 
Kipofu kaona mwezi! Haya matusi si tabia ya timu kubwa ya Simba. Endeleeni kutukana maana mnaonja ladha ya fedha za CAF.
Sisi ndio tulikuwa wa kwanza kula fedha za CAF 1998 miaka mitano baaadaye mwaka 2003 ndipo mlipojitutumua na kula fedha mara moja na mwisho hadi leo. Acha ushamba! Leteni makaratasi (invoices) tuwalipie deni lenu mbaki ligi kuu ili mwaka kesho tujichukulie pointi zetu 6.
 
Subiri tunamwangalia tu huyu muro cha moto atakiona.Simba kwanini tunaruhusu dharau kama hizi lakini?
Hizi dharau zitaendelea kuwa juu yenu hadi hapo mtakapobadilisha viongozi. Kwa hawa waliopo jina la Simba litaendelea kupigwa vijembe na kejeli za kutosha.
 
Back
Top Bottom