MTAZAMO
JF-Expert Member
- Feb 8, 2011
- 19,675
- 33,583
Ndugu na kiongozi wetu,
Kipindi chote cha utawala wako hukuwa tofauti na wajumbe wengine wa bodi. Umeshindwa kabisa kuonekana ni mwakilishi wa wanachama.
Matawi ya Simba hamasa imekufa na uliacha kabisa kuwa karibu na wanachama na matawi yenyewe. Nguvu ya wanachama ipo kwenye matawi ulipaswa kukutana nao mara kwa mara kujadili maendeleo ya club.
Uwakilishi wa wanachama umekosa nguvu kabisa kwenye bodi zaidi ya kuonekana kwenye matukio muhimu ya club. Hili itapaswa liangaliwe vizuri ili majukumu ya nafasi yako yawe wazi kuzuia mgongano wa maslahi.
Unaonekana ni muweledi kiutendaji na muelewa lakini hii miaka 4 ni kama uliwekwa pale bora liende tu na wewe ukajisahau ipo siku utahitaji kuomba kura.
Kipindi chako ndio Simba imeshindwa kabisa kufurukuta kwa Yanga na hii hata ujivue vipi lakini raha ya wanachama ni kumfunga mtani otherwise wewe kiongozi wao hutaeleweka.
Huu uchaguzi ukipita kwa bahati inabidi ubadilike sana! Wewe wako ni wanachama, unapaswa kulala na kuamka huko kuanzia kadi, hamasa na kusimamia maslahi ya wanachama kwa ujumla sio tu kuonekana kwenye picha za vikao vya bodi na kusafiri na timu.
Unazidiwa hata na Ahmed Ally ambaye anajichanganya na wanachama kuliko wewe mwenye wanachama na angegombea hakuna ambaye angemshinda.Badilika brother, miaka 4 iliyopita ulipwaya sana lakini bado unaweza kufanya vizuri.
Ni mimi shabiki nisiye na kadi ila nipo hapa tawini Bunju!
Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app