Murtaza Mangungu una kazi nzito kupenya!

MTAZAMO

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2011
Posts
19,675
Reaction score
33,583
Ndugu na kiongozi wetu,

Kipindi chote cha utawala wako hukuwa tofauti na wajumbe wengine wa bodi. Umeshindwa kabisa kuonekana ni mwakilishi wa wanachama.

Matawi ya Simba hamasa imekufa na uliacha kabisa kuwa karibu na wanachama na matawi yenyewe. Nguvu ya wanachama ipo kwenye matawi ulipaswa kukutana nao mara kwa mara kujadili maendeleo ya club.

Uwakilishi wa wanachama umekosa nguvu kabisa kwenye bodi zaidi ya kuonekana kwenye matukio muhimu ya club. Hili itapaswa liangaliwe vizuri ili majukumu ya nafasi yako yawe wazi kuzuia mgongano wa maslahi.

Unaonekana ni muweledi kiutendaji na muelewa lakini hii miaka 4 ni kama uliwekwa pale bora liende tu na wewe ukajisahau ipo siku utahitaji kuomba kura.

Kipindi chako ndio Simba imeshindwa kabisa kufurukuta kwa Yanga na hii hata ujivue vipi lakini raha ya wanachama ni kumfunga mtani otherwise wewe kiongozi wao hutaeleweka.

Huu uchaguzi ukipita kwa bahati inabidi ubadilike sana! Wewe wako ni wanachama, unapaswa kulala na kuamka huko kuanzia kadi, hamasa na kusimamia maslahi ya wanachama kwa ujumla sio tu kuonekana kwenye picha za vikao vya bodi na kusafiri na timu.

Unazidiwa hata na Ahmed Ally ambaye anajichanganya na wanachama kuliko wewe mwenye wanachama na angegombea hakuna ambaye angemshinda.Badilika brother, miaka 4 iliyopita ulipwaya sana lakini bado unaweza kufanya vizuri.

Ni mimi shabiki nisiye na kadi ila nipo hapa tawini Bunju!

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Unaweza kumlaumu mengine yooote lakini si la kufurukuta Kwa Yanga. Ili Simba ifurukute Kwa Yanga ni mpaka Hali ya Yanga kiuchumi iyumbe.
Kama Simba na Yanga kiuchumi zinalingana, Sahau swala la Simba kuwa juu ya Yanga.
Network ya Yanga nchi hii imefika mbalisana ndio maana hata Yanga ikiyumba ki uchumi haijawahi kuwa mnyonge Kwa Simba au kushika nafasi zaidi ya ya pili tena huwa panachimbika.
 
Kipindi Cha Manji mnakumbuka tuliwafunga mara ngapi Tena wakati mwingine tukiwa pungufu
 
Unaweza kumlaumu mengine yooote lakini si la kufurukuta Kwa Yanga. Ili Simba ifurukute Kwa Yanga ni mpaka Hali ya Yanga kiuchumi iyumbe.
Kama Simba na Yanga kiuchumi zinalingana, Sahau swala la Simba kuwa juu ya Yanga.
Network ya Yanga nchi hii imefika mbalisana ndio maana hata Yanga ikiyumba ki uchumi haijawahi kuwa mnyonge Kwa Simba au kushika nafasi zaidi ya ya pili tena huwa panachimbika.
Yanga ipi unayoizungumzia?
Yanga ambayo ilikuwa ikifungwa na simba pungufu ya hakina mavugo?
Yanga ambayo huwa inapigwa hadi magoli 5 ,0 na simba?
Mashabiki wa kinyesi fc huwa mnavichwa vya kuku mnapoteza Sana kumbukumbu

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Adv Kaluwa nimeona hata wanachama maarufu wako nae anaweza kupindua meza. Mangungu anataja mafanikio ambayo hana mchango nayo moja kwa moja.

Hakuna alilofanya kwaajili ya wanachama. Hata wabunge wanapitaga majimboni walau kinafiki. Imefika muda kati ya wajumbe wote yeye ana mzigo mzito zaidi maana anawajibika kwa wanachama moja kwa moja! Alifikiri nafasi yake kama Asha Baraka [emoji38]

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Unaweza kumlaumu mengine yooote lakini si la kufurukuta Kwa Yanga. Ili Simba ifurukute Kwa Yanga ni mpaka Hali ya Yanga kiuchumi iyumbe.
Kama Simba na Yanga kiuchumi zinalingana, Sahau swala la Simba kuwa juu ya Yanga.
Network ya Yanga nchi hii imefika mbalisana ndio maana hata Yanga ikiyumba ki uchumi haijawahi kuwa mnyonge Kwa Simba au kushika nafasi zaidi ya ya pili tena huwa panachimbika.
Mwaka 2012 pale Yanga alipofungwa 5-0,hali ya uchumi wa Yanga ilikuwaje?
 
Adv Kaluwa nimeona hata wanachama maarufu wako nae anaweza kupindua meza. Mangungu anataja mafanikio ambayo hana mchango nayo moja kwa moja.

Hakuna alilofanya kwaajili ya wanachama. Hata wabunge wanapitaga majimboni walau kinafiki. Imefika muda kati ya wajumbe wote yeye ana mzigo mzito zaidi maana anawajibika kwa wanachama moja kwa moja! Alifikiri nafasi yake kama Asha Baraka [emoji38]

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
Ukweli tunahitaji sura mpya na mawazo mapya.Mangungu apumzike kwanza.
 
Back
Top Bottom