Nimesoma mahali kuwa kuna jamaa wameanza kuandaa na kunoa mapanga,wanadamu hatujifunza tunauana wenyewe kwa wenyewe kwa manufaa ya viongozi wachache ambao shida zetu wala hawazijui,sioni kwa nini Mluhya,Mjaluo ,Mkikuyu,Mkale wawe na uhasama kwa sababu ya hao masultani wa kikabila,leo kaibuka mwingine kwa jina la MuDVD na Wamalwa ,wanadai safari ii lazima watu wa kabila lao waungane ili raisi atoke huko,je hao milioni 2,4 wakimchagua ndio atawapa sembe hao wote au itakuwa kwa wateule wachache wanaomsifia kuwa kavaa suti nzuri ilihali yu uchi,wandugu nilikuwa Nakuru ule wakati wa machafuko ,sikutegemea tena wananchi na wanasiasa wangeanza tena kurudi kulekule,je bado mnategemea tena Annan na Mkapa waje kuwafundisha jinsi ya kuishi pamoja