Fundi Mchundo
Sina haja ya kushinda kama unavyotaka. Hivi unafahamu kwamba geologists miaka ya 1960's walikuwa wanasoma baada ya kupata first degree? Vile vile Geotechnics kuna topics ambazo siku hizi wanasoma kwenye first degree lakini zilikuwa so advanced wakati ule na hakukuwa na programmes kwenye computer kufanya baadhi ya calculations. Kitu ambacho unashindwa kuelewa ni umbumbumbu ambao viongozi wetu wanauendekeza.
Kwa hiyo miaka ya sitini walikuwa wanachukua digrii ya kwanza halafu wanaenda Dodoma kusomea geology, hiyo miaka ya sitini? Unaamini kweli hiyo?
Hii ndiyo sentensi uliyoikana!Aha,kumbe ulisema programmes za kwenye computer! Samahani Mkuu kwa kusingizia. Lakini kama hizo calculations zilikuwa so advanced kwa nini walizifundisha? Walimu waliwapa na waliposhindwa waliwaambia wasiwe na wasiwasi, programme zinakuja? Sijaelewa umbumbu unaoendekezwa na viongozi wetu katika hili. Kutokuwa na programme za computer advanced miaka ya sitini? Au kutowatumia hao mageologists wa miaka ile wenye digrii ya kwanza? Au kutowatumia hao Civil Engineers waliochukua elective ya Geo-technics?
Ninarudia ukienda leo hii Bulyankulu wanaofanya kazi wataalam wa kitanzania wanalipwa pesa ndogo kulinganisha na wale wa nje kisa wao wana ngozi nyeusi rejea malalamiko yao kwenye mgomo. Tatizo sio kuwa na uwezo ni ubaguzi wa kipumbavu ambao serikali inaufumbia macho.
Katika soko huria, unaomba kazi na kabla ya kuingia mkatba mnakubaliana mshahara na marupurupu na haki zako nyingine. Kama mshahara anaoku"offer" mwajiri unaona ni mbuzi unakataa kusaini mkataba na unajiondokea. Ukisaini mkataba na ukakuta kuna mtu ambae kiuwezo unaona unamshinda na alipwa zaidi, unamweleza mwajiri wako. Mkishindwa kuelewana, unaacha kazi! Mathlani, umeajiriwa Microsoft halafu ukagundua kuwa Bill Gates ni kilaza hata digrii hana, na wewe una Ph.D ya nguvu,una haki ya kwenda kwa bosi na kulalamika. Wakikataa kukupandisha kumzidi Bw. Gates au kumshusha ili umzidi, unajiondokea na stock options zao unawatupia usoni.
Kuhusu hiyo budget support ndio nasema hatuihitaji kwani nchi kama Kenya wameondokana nayo na sisi tangu pale WB au IMF whoever suggested it and tried that system ndio tumeikumbatia lakini haina faida kwa sababu hiyo misaada haiwafikii walengwa inatafunwa na wajanja wachache.
Kwa vile wajanja wachache wanatafuna budget support tunasema hatuihitaji badala ya kuwachukulia hatua. Hivi kweli tumefikia mahali pa kuionea wivu Kenya? Mnyonge mwenzetu! Wale mabwana walikataa budget support kwa vile hawakutaka kuulizwa kulikoni katika ulaji wao. Hamna cha uzalendo. Tusimtupe mtoto na maji yake!
Export zinazoweza kuboreshwa ni pamoja na kuuza nyama ya ng'ombe EU, kuongeza ubora wa packing katika matunda yote yanayooza kila mwaka na kuuza EU kwa sababu wana shida ya matunda, kufufua zao la Zabibu kule Dodoma na kuuza kwa fujo. Kuongeza ulimaji wa mazao ya chakula na kuuza popote pale duniani wanakohitaji, kuongeza airport charges kwa wageni hadi kuwa $50 kwani hii ya $20 ni ya tangu miaka ya 1980. Kuweka kipaumbele kwenye kilimo matrekta ya ukakika yanunuliwe badala ya mashangingi, kukuza utalii, kuuza madini as finished products sio kuuza mchanga. Kukuza utumiaji wa gesi ambayo tunayo nyingi ya kutosha n.k. List ni ndefu sana...... vile vile lazima uzingatie kuwa na civil servant ya wafanyakazi wachache na wanaolipwa vizuri, kufanya computerization ya hali ya juu kwenye idara zote za serikali.
Nimejaribu kukueleza kuwa kuuza E.U sio kama sokoni. Kuna kitu kinaitwa Tariffs. Kuna kitu kinaitwa standards ambazo zinatumiwa vizuri kutuzia kuingia kwenye soko lao. Ndiyo maana waheshimiwa hawajaweza kuelewana kwenye mzunguko wa Doha.S.Africa na Angola wanauza nyama ya ng'ombe E.U? Mimi nilidhani Botswana ndio wauzaji wakubwa wa nyama ya ng'ombe.Lakini si unakumbuka Tanganyika packers ilivyotushinda. Na aliyekuambia E.U wana shida ya matunda nani? Machungwa etc yanatoka Spain,Egypt,Israel Ecuador wanamwaga ndizi etc. hata hizo tariff wakizitoa, tutauweza ushindani wa latin amerika, afrika kusini na nchi za mediterranean? Vile vile mvinyo. Unaamini napo kuwa tulima zabibu, halafu tukamwage Dodoma wine ulaya? Unajua soko hili lilivyo competitive? Unaujua ugomvi unaoendelea kati ya Afrika Kusini na E.U kuhusu mvinyo? Unajua wakulima wachampagne walivyo wakali kuhusu zao lao? Unajua wareno wanavyong'aka kuhusu port? Halafu kuna waAustralia, waArgentina na wenzetu wa Napa valley? Leo unaamini utawapelekea Dodoma wine bwelele?
Finished madini? Utashindana na wadachi? Unadhani mhindi yuko tayari kunua heleni zako za dhahabu? jiulize kwa nini viwanda vya korosho vilikufa?
hayo matrekta tukishayanunua badala ya mashangingi tutayafanyia nini? Kwa maneno mengine tutayafikishaje huko shambani? Tuwape bure wakulima wetu, tuwakopeshe au tuwauzie? Hawa ni wale hata pampu za Tanira ziliwashinda kuhudumia?
Gesi tunayo kweli lakini si nyingi kama unavyodhani. Pamoja na hayo, tuifanyie nini? Tuzalishe umeme ambao nasikia wenzangu wa Mtwara na Lindi hawawezi kuutumia? Tuusambaze kwenye majumba kama wenzetu wa ulaya wanavyofanya? Viwanda vingapi vinauwezo wa kutumia gesi yetu. Au tuzalishe mbolea ambayo soko la dunia limejaa? Zaidi ya hapo inapingwa na wanamazingira kwa kupunguza rutuba katika ardhi.
Haya ndugu yangu msomi, civil servant ya wafanyakazi wachache maana yake nini? Kwa upeo wangu mdogo, nadhani unamaanisha civil service ya watu wachache. Kama tena nimekuharibia mpangilio wa sentensi yako uniwie radhi. Hao civil servant surplus ambao sasa hivi wanafukuza chawa maofisini wakipunguzwa waende wapi? Kwa bahati mbaya si ofisi zote za serikali ziko Dar es salaam. Hizo za Kasulu, Manda, Mbaba Bay na zenyewe tuzicomputerise? Wakati hata umeme wa hakika hamna?
Mimi ninachokisema ni hiki tuu. Nchi yetu masikini sana ingawa ina potential. Ni sisi kwa kujituma ndio tunaweza kujitoa kwenye haya matatizo. Safari itakuwa ndefu na ngumu, tutakatishwa tamaa na wenzetu wenye uchu wa utajiri wa haraka haraka na wasio na uchungu wa nchi yao, hatuna mjomba uko nje ambae atatukomboa sisi ila tukijitahidi tutafika. Lakini si kesho. Tuwekeza kwenye elimu itakayomuempower mwananchi, tukabili matatizo yaliyo ndani ya uwezo wetu ( kupunguza vifo vya wakina mama wazazi,watoto wadogo,maji safi vijijini n.k) tuwatumie kikamilifu wataalamu wetu walio nchini na nje ya nchi, tujifunze kutokana na makosa tunayoyafanya badala ya kutafuta visingizio, tufungie kazi ubadhirifu wa aina yeyote ( ikiwa pamoja na kujipangia mishahara tusioyostahili, kutumia magari ya kifahari, kusafiri kifahari-si kila mtumishi wa umma lazima asafiri First class,tupunguze matumizi ya nishati katika maofisi yetu), tujifunze kwa waliotutangulie, turejeshe kiburi cha utaifa,tuishi kulingana na kipato chetu haswa haswa wale walio katika nafasi za uongozi,tuwekeze katika elimu,tutumie rasilimali yetu ya lugha ya Kiswahili ( tuwe kitivyo cha sinema, uandishi n.k za kiswahili), tuenzi mazingira yetituwekeze katika elimu, tuwekeze katika elimu, tuondoe usiri katika shughuli za serikali ikiwa ni pamoja na mikataba yote, tuwe wakweli na wazi katika shughuli zetu. Wengine wanaweza kuongezea.
Lakini kwako wewe Mheshimiwa Dua na Bubu, sidhani kama tutakuja kukubaliana. Naomba kiutuuzima na hasa ukilinganisha ugeni wangu na kutobahatika kwenda shule kama wenzangu,tukubali kutofautiana na tuendelee na hoja nyingine.Huna sababu ya kunizulia mambo ambayo mimi sikuyasema.