Museveni alarmed by human capital flight

Museveni alarmed by human capital flight

Wanasiasa na wala si wasomi ndio wanaosababisha matatizo chungu nzima Tanzania. Wasomi wengi wameshajiondokea au wako mbioni kujiondokea na huko waliko wanafanya mavitu babu kubwa kimya kimya na wanathaminiwa. Hawa wanasiasa uchwara ndio chanzo cha matatizo yetu chungu nzima, kama hutaki kuamini hivyo utajiju...nimeshakupa mifano hai ya jinsi wanasiasa wanavyoiangamiza Tanzania.

Karamagi pale madini kishavurunda vya kutosha, Balali pale BOT kishavurunda vya kutosha na kuna ushahidi tosha wa kumfungulia mashtaka, Meghji pale Fedha kishavurunda vya kutosha na baadhi ya mawaziri wengine pia wamevurunda, lakini "Msomi" wetu kawaacha wandelee kupeta pamoja na manung'uniko chungu nzima toka kwa wananchi...Oops! I forgot that the wasomi are the one to blame for many problems in our beloved country....🙂

Mtu anataka tu kuwa Rais wa nchi au Waziri mkuu wala hana sera zozote bali ni alinacha tu, huko kote alikopita aliacha madudu tu hakuna chochote alichonafanikisha na kwa kuwa Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu hatuwahoji watu hawa mbona huko kote mlikopita mlifanya madudu na nafasi hizo zilikuwa ni ndogo ukilinganisha na Urais au Uwaziri Mkuu? Bali tunawapa nafasi hizo na kisha kuimba nyimbo za Komba nyingi CCM ni nambari one (nambari one kwa kuiangamiza nchi), anameremeta wakati nchi inaendelea kudumaa!
 
Tanzanians tumeezidi na ubabaishaji. WE HAVE DECIDED TO DELEGATE OUR RIGHT TO BE AT THE BATTLE FRONT TO DEMAND AND DEFEND OUR RIGHTS! HAKUNA MTU WA KUKUPIGANIA NI WEWE. SIO LOWASSA WALA JK! Haiwezekani tukawa na huu mtizamo na tukajidanganya kwamba tutaendelea. watu wako majuu, hawafikirii kwamba hiyo majuu ilitafutwa! Au unafikiri huko wasomi wetu wanakothaminiwa walizaliwa wakiwa wanathaminiwa? Its a process na huo uhuru na freedom watu mnayoienjoy huko mliko, kuna watu walipigana kiume mpaka wakaupata huo uhuru ingawa hawakuufaidi. Talk of Martin Luther King NA HAKI ZA WEUSI USA! Leo mtu mweusi anatembea kuifua mbele USA. lakini hajiulizi ni kiasi gani cha gharama watu walilipa kusudi mtu mweusi akombolewe! wengine walifungwa magerezani miaka mingi, wengine walikufa vifo vibaya, kikubwa ni kwamba walikuwa wanahangaikia kitu ambacho walikiamni na leo wewe na yule ndo mko proud kusema kwamba mnathaminiwa huko mliko! Ingawa aliyepigana na kulipa gharama, hakufaidi chochote!

Jamani kuendesha nchi sio kuendesha kampuni binafsi you need the art of compromise! JK cant do each and everything on his own, sasa kama wenye mawazo mazuri mnaogopa kuyatoa eti mtalalamikiwa na system, harafu bado tunalaumu. You will know the pain f the system ukiijoin na wala sio kuwa outsider critique! wasomi inabidi tutumie elimu yetu kuyabadilisha mazingira. hakuna anayeweza kutubadilishia haya mazingira!

Wangapi hapo mko tayari kuacha maisha ya ulaya na kurudi bongo? Kisa eti mazingira duni! Get life!

Muungwana hapo juu kanena na mimi nasema, wasomi ndo tunairudisha nyuma Africa! WE WANT GOOD THINGS BUT WE ARE NOT PREPARED TO PAY THE ULTIMATE PRICE!

Kama jamaa alivyosema, wasomi tutazidi kupokezana vijiti vya ufisadi kwa sababu tunataka kuishi peponi wakati hatutaki kuilipia hiyo pepo kwa gharama stahili! Usitegemee babu au mjomba wangu wa Kwimba apambane na Lowassa wakati mimi mwenye elimu kama Lowassa nimekimbia uwanja wa mapambano. Mi ndo mwenye hoja, common man anakuangalia wewe MSOMI! sasa ukikimbia yeye atafanya nini?
 
Kama walivyosema wenzangu hapo juu, hao wote mnaowalalamikia kuwa ni wasomi na wengine kutoka kwenye hizo shule za ivy league. Mmewasikia wakina Obama,Hillary na Edwards wakitambiana nani amesoma zaidi? Wanabishana kuhusu uwezo wa kuongoza na vision itakayoweza kuwatoa watu wao kutoka hapo walipo hadi mahali bora zaidi. Na si kusema tuu, wanatoa programmes ambazo zinajadiliwa na wenye uwezo. Leo sisi badala ya kuzumnguzia namna gani tutajitoa hapa tulipo, majibu mepesi kama tukiuza hayo mashangingi neema itapatikana, tukilipana $1,500 bila kuainisha nani ndiye atalipwa hizi $(daktari aneyaanza kazi, mhandisi, rubani wa ndege, fundi mchundo, mwalimu wa praimari, afisa kilimo, afisa mifugo, afisa utawala,hakimu wa mahakama ya mwanzo n.k?) mambo yatakuwa mema,tuweke kompyuta kwenye ofisi zote na serikali, tuuze ndizi ulaya n.k. Hao wanaoangamiza hii nchi wanalipwa hizo Benjamin na ndio wametufikisha hapa. Hakuna mtu anawatetea watu wanaoifanyia maovu nchi yetu. La, tunachokisema ni kuwa badala ya kuwa watu wa ishu moja tuonyeshe usomi wetu na uwezo wa kuongoza kwa kuonyesha njia mbadala ya kututoa katika hali duni tuliyokuwa nayo. Sisi tulio nje, tusiwakebehi wale tuliowaacha ila tuwape moral support kwa kutoa mawazo yenye kusidio la kujenga nchi na kuongeza kipato cha watanzania WOTE ( wale tunaoishi Dar es Salama tuu na vidigrii vyetu mkweche pamoja na wale wa Kibondo, Kasulu, Manda, Tandahimba, Machame, MbambaBay n,k ) na kuwaunga mkono kwa nguvu zote pale wanapogundua maovu. Kuwatusi kwa ndoto za alinacha ni kuongeza chumvi kwenye kidonda.
 
Fundi Mchundo

Pengine kweli ni mgeni katika huu ukumbi au umebadili jina ulikuwepo kwa muda mrefu au ulikuwa msomaji tu. Sina sababu ya kumtukana mtu yoyote tena ambaye simjui lakini kitu ambacho utakutana nacho kwenye forums ni kukubaliana kutokubaliana au vinginevyo.

Kuna mada nyingi sana katika forum hii na huwezi kupata jibu kwenye thread moja na kufikiria umepata majibu unayoyategemea katika nyanja mbalimbali.
 
Oh, hivi mwanasiasa hawezi kuwa Msomi?

Hapo ndipo dugu yangu BUBU nashindwa kumuelewa maana wanasiasa ndio walio hudhuria madarasa .
USOMI WA WATANZANIA UNAUWALAKINI MKUBWA
unajua kuna kupita darasani na usielimike vilevile kama wengi tulivyo ndio maana nikakutolea mfano SHABAN ROBERT alikomea darasa la saba lakini alikuwa ameelimika vya kutosha.

mimi ningeshauri MFUMO WA ELIMU UTAZAMWE UPYA
maana inaonekana mtu anayejua kukariri vizuri ndiye msomi ndugu yangu BUBU usomi ni IQ ILIYO KICHWANI.

NA nchi bila kuwa na wasomi wa kweli kamwe haiwezi kuendelea na ndicho kinachoendelea leo hii TZ.
 
Point taken!
Mimi ni mgeni na sijakusudia kumtukana mtu. Nisichopenda ni mtu kuwa condescending kwangu. Haunijui, sikujui, let's treat each other with due respect. Tunapotofautiana, tukubali kutofautiana. Hatari ya hii forum ni kutupa "delusions of grandeur" na kuamini kweli tunajua kila kitu, mimi nikiwa mmojawapo. Kwa kifupi, mheshimiwa Dua, sikubaliani na msimamo wako lakini una kila haki ya kufikiria hivyo unavyofikiria. Na mimi vile vile. Labda litakuja suala hapo baadae tutakuwa upande mmoja. Pengine sivyo. Lakini naombea tuweze kufanya hivyo kwa kuheshimiana.
Kama unahisi nimewahi kukutukana, samahani sana.
 
Tanzanians tumeezidi na ubabaishaji. WE HAVE DECIDED TO DELEGATE OUR RIGHT TO BE AT THE BATTLE FRONT TO DEMAND AND DEFEND OUR RIGHTS! HAKUNA MTU WA KUKUPIGANIA NI WEWE. SIO LOWASSA WALA JK! Haiwezekani tukawa na huu mtizamo na tukajidanganya kwamba tutaendelea. watu wako majuu, hawafikirii kwamba hiyo majuu ilitafutwa! Au unafikiri huko wasomi wetu wanakothaminiwa walizaliwa wakiwa wanathaminiwa? Its a process na huo uhuru na freedom watu mnayoienjoy huko mliko, kuna watu walipigana kiume mpaka wakaupata huo uhuru ingawa hawakuufaidi. Talk of Martin Luther King NA HAKI ZA WEUSI USA! Leo mtu mweusi anatembea kuifua mbele USA. lakini hajiulizi ni kiasi gani cha gharama watu walilipa kusudi mtu mweusi akombolewe! wengine walifungwa magerezani miaka mingi, wengine walikufa vifo vibaya, kikubwa ni kwamba walikuwa wanahangaikia kitu ambacho walikiamni na leo wewe na yule ndo mko proud kusema kwamba mnathaminiwa huko mliko! Ingawa aliyepigana na kulipa gharama, hakufaidi chochote!

Jamani kuendesha nchi sio kuendesha kampuni binafsi you need the art of compromise! JK cant do each and everything on his own, sasa kama wenye mawazo mazuri mnaogopa kuyatoa eti mtalalamikiwa na system, harafu bado tunalaumu. You will know the pain f the system ukiijoin na wala sio kuwa outsider critique! wasomi inabidi tutumie elimu yetu kuyabadilisha mazingira. hakuna anayeweza kutubadilishia haya mazingira!

Wangapi hapo mko tayari kuacha maisha ya ulaya na kurudi bongo? Kisa eti mazingira duni! Get life!

Muungwana hapo juu kanena na mimi nasema, wasomi ndo tunairudisha nyuma Africa! WE WANT GOOD THINGS BUT WE ARE NOT PREPARED TO PAY THE ULTIMATE PRICE!

Kama jamaa alivyosema, wasomi tutazidi kupokezana vijiti vya ufisadi kwa sababu tunataka kuishi peponi wakati hatutaki kuilipia hiyo pepo kwa gharama stahili! Usitegemee babu au mjomba wangu wa Kwimba apambane na Lowassa wakati mimi mwenye elimu kama Lowassa nimekimbia uwanja wa mapambano. Mi ndo mwenye hoja, common man anakuangalia wewe MSOMI! sasa ukikimbia yeye atafanya nini?

Wenye ubabaishaji ni wanasiasa ndio maana Watanzania wameanza kuamka na kuwabana kuhusu ahadi zao. Na wanapoonekana wanaongea upupu hata kuzomewa wamezomea na hili halikuwepo Tanzania miaka ya nyuma.

Ndio majuu ilitafutwa na majuu sheria ni msumeno hata ukiwa nani umefanya makosa ya ufisadi, kula rushwa kutumia nafasi yako kujitajirisha basi utafunguliwa mashtaka na lupango ndio kutakuwa nyumbani kwako. Tanzania bado kulindana kumeota mizizi si unakumbuka usemi wa "Mwacheni mzee wetu astaafu kwa amani" majuu huyu angefunguliwa mashtaka na mvua zingemnyeshea bila kujali alikuwa nani katika serikali.

Watanzania wengi leo wanngependa kuona kashfa chungu nzima dhidi ya Mkapa zinachunguzwa na kama kuna ushahidi wa kutosha kuhusu kutumia wadhifa wake kujitajirisha, kupokea rushwa kwenye miakata aba mbali mbali, basi afunguliwe mashtaka na mali alizozipata kwa njia za haramu zifilisiwe, hili ndio Watanzania wa kila kona wanataka kuliona kwamba hakuna Mtanzania ambaye anastahili kuwa juu ya sheria.

How can you pay ultimate price when what you receive as your remuneration is not sufficient enough to last a month! 😕
Workers must receive good remeneration in order to be able to contribute to our economy, otherwise it is impossible!

Pepo haiwezi kulipiwa na wasiokuwa nacho! Kama tunapambana na mafisadi, wala rushwa na viongozi waroho wa utajiri basi tutaongeza cake yetu na kuweza kuwanufaisha Watanzania wote, badala ya mafisadi wachache ambao wao, familia zao na marafiki zao wanakuwa mabilionea wakati asilimia kubwa ya Watanzania wanaendelea kuishi maisha ya dhiki na wakati huo huo wakiendelea kuimba wimbo wao maarufu wa "nchi yetu maskini." The puck must stop somewhere, and in my opinion the puck must stop to our selfish politicians who don't give a damn about the future of Tanzania.

Mikataba fake ya madini, rada, Richmond na kuwa na gharama kubwa za uendeshaji wa serikali kwa kutaka kuendesha magari ambayo ni ghali mno, mawaziri chungu nzima ambao hatuwahitaji. Mpaka hapo asilimia kubwa ya Watanzania watapofumbua macho na kujua ni nani wa kulaumiwa kuhusiana na matatizo ya nchi yetu, mafisadi, wala rushwa na viongozi waroho wa utajiri wataendelea kuneemeka kupitia migongo ya Watanzania.

Kamwe Tanzania haiwezi kuendelea kama sheria inawabana wanyonge tu na sio viongozi na matajiri. Hawa wataendelea kupindisha sheria kila kukicha kwa manufaa yao na kwa kuwa Tanzania hawa watu wako above the law basi wanyonge ndio wataendelea kuishi maisha ya dhiki wakati mafisadi, wala rushwa, viongozi wanaoutumia nafasi zao kujitajirisha wakiendelea kufaidi utajiri wa Tanzania. Mwenyezi Mungu ibariki Tanzania.
 
Hapo ndipo dugu yangu BUBU nashindwa kumuelewa maana wanasiasa ndio walio hudhuria madarasa .
USOMI WA WATANZANIA UNAUWALAKINI MKUBWA
unajua kuna kupita darasani na usielimike vilevile kama wengi tulivyo ndio maana nikakutolea mfano SHABAN ROBERT alikomea darasa la saba lakini alikuwa ameelimika vya kutosha.

mimi ningeshauri MFUMO WA ELIMU UTAZAMWE UPYA
maana inaonekana mtu anayejua kukariri vizuri ndiye msomi ndugu yangu BUBU usomi ni IQ ILIYO KICHWANI.

NA nchi bila kuwa na wasomi wa kweli kamwe haiwezi kuendelea na ndicho kinachoendelea leo hii TZ.

Kwenye usomi kuna ethics na code of conduct ambazo zinatakiwa zifuatwe na wasomi mbali mbali. Kwa mfano Wahandisi, Wahasibu, Wanasheria na wasomi wengine wana ethics zao na code of conduct ambazo ni lazima wazifuate ili waendelee kupractice kile walichosomea. Wanapokiuka taratibu hizi basi huadhibiwa na kuzuiliwa kabisa kupractice katika nyanja walizosomea.

Kwenye siasa hasa za Tanzania ni bora liende tu hata ukivurunda mara ngapi wewe bado unapeta tu hakuna ethics wala code of conduct. Hapo ndio tofauti kubwa ya wasomi na wanasiasa. Kwa maoni yangu wanasiasa wengi wa Tanzania hawastahili kuwekwa kwenye kundi la wasomi.

Unapokuwa na wadhifa wa kisiasa ambao hauhitaji elimu yako ili uweze kupewa wadhifa huo, basi kwa maoni yangu hapo unakuwa ni mwanasiasa. Kwa mfano Sarungi alikuwa ni daktari mzuri wa mifupa pale Muhimbili lakini alipewa nafasi ya kisiasa kama waziri wa ulinzi. Nafasi ile haikuhitaji elimu yake ya udaktari ili aweze kukabidhiwa wadhifa ule maana hakuwahi kabisa kupitia jeshini. Na baadhi ya nyanja za usomi ukishakaa kwa kipindi fulani bila kupractice kile ulichosomea huwezi kuruhusiwa kupractice maana unaweza kabisa ukafanya madudu na kutia dosari kubwa nyanja hiyo.
 
BUBU
Sasa tupe njia mbadala serikali ifanye nini?? Na. ukizingatia kuwa kila tutayemweka pale mwandirifu atageuka kuwa FISADI ili ajitosherezee mahitaji yake mfano kuna jamaa hawataki kurudi wakiogopa ujira mdogo ina maana hawa wakirudi na wamezoea ma pound na madola mostly like watakuwa MAFISADI. na ikumbukwe serikali ile na masikini sana.TUFANYE NINI NDUGU YAGU????
 
Bubu! Mengi unayosema nakubaliana nayo. Tatizo ni huku kudai remuneration pekee ndio tiba ya matatizo yetu. Bila kuwa na mazingira mazuri ya kazi, uwajibikaji na naam, kuthamini na kutumia kwa busara rasilimali yetu (natural na human) hatutafika mbali. Hao unaowaita mafisadi wanalipwa vizuri sana ( wengine walikuwa nje na kurudi nchini ati kutumikia taifa) na wamesoma vizuri lakini wote wana hili tatizo la "sense of entitlement" bila kuwa na uchungu wa taifa letu. Kwa vile unakataa kuwaita wanasiasa wasomi,basi tupe definition yako ya usomi.
 
Ewaa!...Now you're talking!...🙂 Kusema ukweli nimekutana na Watanzania wengi wasomi na wengi naweza kusema kwamba wana uchungu wa kweli na Tanzania. Kinachowakosesha raha ni kuona Tanzania hainufaiki na rasilimali zetu na sera mbovu zinazorudiwa mwaka hata mwaka pamoja na kutokuwa na mafanikio yoyote katika sera hizo. Pamoja na kelele miaka nenda miaka rudi hadi leo wachukuaji bado wanachukua tu, kama utakumbuka kelele za mikataba ya madini zilianza tangu wakati wa Mkapa. Pia kinachowauma ni kuona wazungu ambao kielimu hawakusoma kama Watanzania wanalipwa vizuri sana wakati wa Tanzania wanaendelea kulaliwa kwa kazi zile zile wanazozifanya au wakati mwingine Watanzania kufanya kazi zaidi ya wazungu. Kingine ni kiburi cha viongozi wetu. Hata pale ambapo kunapokuwa na ushahidi tosha kwamba jamaa kavurunda atainuka na kuonyesha kiburi chake cha hali ya juu kama vile yeye ni Mungu Tanzania 'the untouchables'.

Case in point Karamagi baada ya kuvurunda pale madini alitamka mbele ya kadamnasi kwamba sijiuzulu ng'o na mpaka leo bado anapeta. Na hata kwenye tetesi za mabadiliko ya baraza la mawaziri tulizoanza kusikia tangu mwaka 47 anaweza kuendelea kuwepo. Balali naye vivyo hivyo sasa hapa kuwajibika hapa kuko wapi!? Mtu kavurunda awekwe pembeni na kama alinufaika kinyume na sheria basi sheria iachwe ifuate mkondo wake bila upendeleo wowote. Kingine ni cha mtu mmoja kukumbatia vyeo lukuki. Yeye huyo huo ni Waziri, Mbunge, Mjumbe wa NEC, Mjumbe wa CC, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya kampuni A,B, C, na D. Nchi yenye idadi ya watu 39 millioni kuna watu chungu nzima ambao wanastahili kabisa kushika nafasi hizo, ni kwanini mtu huyo mmoja akumbatie nafasi zote hizo na kote huko analipwa kama si allowance ya vikao basi mshahara na marupurupu mengine chungu nzima. Hili nalo linawakera sana Watanzania walio wengi. Kwa kumalizia yaliyotokea mwaka huu mpaka vingunge kuzomewa yanaelekea yatakuwa ni mwanzo mzuri wa kuhakikisha viongozi wanawajibishwa na pia kupunguza kama siyo kuondoa kabisa viburi vyao, lakini bado tuna safari ndefu sana.

Sasa ndugu yangu mchundo jamaa kasomea udaktari anapewa wizara ya fedha na hili lipo sana nchini, huyu mara nyingi hajui chochote kuhusiana na dr na cr, sasa huyu akivurunda pale wizara ya fedha kuna haja ya kuwalaumu wasomi wote wa Tanzania?

Popote pale ulipo Mtanzania usikae kimya kuona nchi yako inaendelea kuliwa na wageni na watu wachache wanaojiita viongozi. Lazima tuhakikishe rasilimali tulizojaliwa na Mwenyezi Mungu zinainufaisha Tanzania na Watanzania wote!?
 
Kama nilvyosema,Bubu, mengine nakubaliana na wewe , mengine sikubaliani. Daktari kushindwa kuongoza wizara ya fedha si kwa sababu hajui dr au cr, ni kwa sababu ana walakin katika uongozi. Kiongozi ni yule mwenye upeo (vision) na anayeweza kuwavuta wanaomfuata kuamini katika vision hiyo. Kiongozi (bora) ni yule anayeangalia na kutambua nguvu na udhaifu wa wale anaowaongoza na akautumia ipasavyo. Kiongozi(bora) ni yule anayetambua limits au udhaifu wake na kuukabili ipasavyo. Katika hali hiyo, anakubali kukosolewa na kuomba ushauri pale inapobidi. Kama hajui dr au cr, anahakikisha anapata mtu anayejua hizo na kumtumia kikamilifu. Kiongozi (bora) hatasita kuwaambia anaowaongoza ukweli wa hali halisi na kuchukua hatua zinazotakiwa hata kama zitakuwa na hasara kwake binafsi. Kwa maneno mengine, si populist!Kiongozi(bora)anaongoza kwa mfano-kama kujibana mikanda, wote tunajibana. Kiongozi bora anawaheshimu anaowaongoza akitambua hao ndio watakaomletea yeye mafanikio. Kiongozi si lazima awe msomi au mtaalam. Kwa mfano; Yesu Kristu, mtoto wa fundi seremala, Mtume Mohamed S.A.W hakwenda shule, Buddha mtoto wa mfalme aliyedekezwa kabla ya kuamua kuondoka na kwenda kutafuta ukweli, Malcolm X alikuwa pimp,drug dealer,convict; akajibadilisha na kuongoza mapambano ya kudai haki ya wetu weusi nchini Marekani, Bill Gates-college drop out n.k. Kiongozi anaweza kuwa msomi, kwa mfano Waziri Mkuu wa kwanza wa Singapore Lee, ameliongoza taifa lake kutoka kwenye umaskini hadi hapo walipo sasa. Viongozi bora wa kiafrika ni wakina Lumumba, Mandela ( aliyeongoza taifa lake kusameheana,utakumbuka alikubali kuitwa mahakami kama raia mwingine na hakujiona Mungu mtu), Nyerere (pamoja na madhaifu aliyokuwa nayo, hakuna mtu aliweza kudoubt integrity yake na pale alipoona mambo yamemzidi alimpisha mwingine),Thomas Sankara (aliwaongoza wa Bukinabe kwa mifano ;k.m. alikataa kununuliwa gari la kifahari na kuendelea kutumia VW aliyokuwa kiiendesha kabla ya kuwa mtawala), Castro, Mahatma Ghandhi, na wengine zaidi. Uongozi si unyapara kama tunavyodhani. Kukaripia tuu,kufokea, kudhalilishana peke yake si uongozi bora. Unahitaji ku'motivate' hao unaowaongoza.
Ukiwa na kiongozi bora utafanya kazi kwa bidii zote kwa vile unajua yuko pamoja nawe.
Naona niishie hapa maana nimeshaongea mno!!
 
Mpeleke mtu mwenye vision kwenye chumba cha upasuaji kama ataweza kufanya chochote kama hakusomea mambo ya upasuaji. Vision bila ya ujuzi wa kile unachokifanya ni ZERO maana hata hao wasaidizi wako wakiamua kukudanganya utadangayika tu maana hujui chochote kuhusiana na kile wanachoongea. Vision itakusaidia tu pale una ujuzi wa kile unachokifanya.
 
Unachanganya tena ,Bubu! Surgeon kiongozi ( lead surgeon)anayeongoza upasuaji si mtaalamu wa kila kitu, na anajua hilo. Ana mtaalam wa nusu kaputi(anaesthetist), ana kiongozi wa manesi n.k. Kama ni surgeon mzuri anawaunganisha wote hawa katika kuhakikisha mafanikio ya operesheni. Hasemi eti kwa sababu mimi ni surgeon basi nitamwelekeza mtu wa nusu kaputi nini cha kufanya. Anashauriana nae halafu wote wanaanza safari ya kuokoa maisha ya huyo wanaempasua. Kiongozi mkuu wa hospitali sio lazima awe daktari. Huyu mara nyingi ni administrator anayehakikisha utaalam wote ulio katika hospitali unatumika ipasavyo. Hii aina maana kuwa akiwa daktari ni vibaya. La hasha, ili mradi awe na uwezo wa kuongoza. Kwani wapi wanasomea uraisi? Anayetakiwa ni mtu makini anayeweza kuliongoza taifa lake kuelekea huko kwenye neema zaidi! Chini yake watakuwepo maprofesa ( wengine waliosoma zaidi yake), walalahoi, wafanyabiashara, watoto wadogo, vibaka n.k. Wote hawa inabidi awaongoze. Wale wakukemewa na kuadabishwa, wanakemewa na wale wenye kuhitaji motivation, ana wamotivate n.k. ili mradi wote hawa wanamuangalia yeye kama kiongozi. Unajua kwa kuzania vyeti ndio kumesababisha ubabaishaji kwa baadhi ya wanao tuongoza. Wamejaa maPh.D ( genuine na fake), maprofesa, wana taaluma, wakishindana kuongea kiingereza n.k. bila kutuonyesha chembe ya uongozi makini! Bila kushabikia upande wowote,kwa mfano, kuna waliosoma kuliko Zitto, wenye experience kuliko Zitto lakini wako wapi? Utawaita hao ni viongozi? Kama ni kiongozi mzuri, utadanganywa mara moja tuu na pale watakapoona hatma ya yule anayedanganya hawatarudia tena. na kama nilivyosema awali, kama hao ulionao wanajua uko nao hawatasita kukueleza ukweli maana wanajua ndicho unachotaka na wao wanajua mafanikio yeyote yatakayopatikana ni yao pia. Tunachohitaji ni viongozi makini wenye uchungu na taifa letu. Kama kuna waomi wana huo uchungu na uwezo wa kuongoza sawa. Mimi binafsi nina wasiwasi na mtu anaesema niko tayari kama mtanitendea hili na lile bila kuangalia uwezo wangu wa kumtendea hayo. Tunahitaji kiongozi ambaye atakuwa na mimi kawenye shida na neema. atakaemwangalia yule alie dhaifu katika sisi wote na kumuinua na kumtumia yule mwenye nguvu kuwasaidia wale wasiokuwa nazo! Utopiac? Pengine. Lakini tusipokuwa na ndoto tutabakiwa na nini?
 
M7 kasahau kutoa chanzo cha tatizo la Africans kukimbia nchi zao. Yeye na watawala wengine ni part ya chanzo kwani politics in Africa is the most paying job. Academicians wanafanya kazi kwa matakwa ya politians na mshahara wa mwanasiasa ni mkubwa zaidi ndo maana wasomi wetu wa vyuo vikuu wanakimbilia siasa badala ya kufanya kazi za kuheshimika kwa jamii. Ndio siasa inaheshimika lakini mara nyingi wanasiasa wengi si wastaarabu.

Hizo kazi nzuri za serikalini mbona wanapeana watoto wa vigogo?

Tatizo la wanasiasa wana threshold ya kufikiri na wanafikiri wenyewe ndo yardstick ya upeo wa wengine kufikiri. Tatizo la kutojiamini linawakumba wengi. Kwamba bora ashauriwe na ngozi nyeupe kuliko kushauliuwa na jirani yake ambaye infact anaweza kuwa mzuri kuzidi mzungu. Kwanza hawa wazungu eti wanafanya consultancy hakuna kitu cha maana kwa wengi kwani wanategemea mawazo, utendaji, data collection toka kwa weusi, wenyewe wanachofanya ni compillation na presentation. Kwa mfano unafikiri kulikuwa na haja gani ya kuipa NETGROUP kuendesha Tanesco, au hawa wazungu wa Canada kuendesha management ya TTCL. Bila aibu mtu anasema eti ni lazima management ipewe kampuni ya Kigeni.

Ni hadi pale mwafrika atakapojikomboa kifikra na kujiamini ndo tutaweza kuendelea na kuacha kulalamika pasipokuwa na sababu.
 
Thank you Semanao!
 
Tunarudia makosa yale yale ya wali. Kurahisisha sana mambo.

Watu kama M7 ni moja ya matatizo tuliyo nayo Afrika. Alianza vizuri lakini naona sasa ameanza kuishiwa mawazo mapya.

Tatizo nionavyo mimi, si kuwa watoto wa vigogo kuwarithi wazazi wao. Ni namna wanavyopewa hizo sehemu ndio tatizo. Kama watashindana na wenzao katika level playing ground na wakashinda, basi na iwe hivyo. Tatizo ni katika kuhakikisha kuwa uwo uwanja wa mapambano kweli ni level!

Ninachopinga kingine ni kuwalaumu wageni kwa kila kitu.
1. Mtu yeyote aliyefanya research au consultancy, atakwambia kazi si kukusanya data, ni kwenye analysis na kutoa kilicho muhimu kwenye hizo data. Baada ya hapa ni kuweza kuwaconvince wenzako kuhusu umuhimu wa hicho ulichokifanya.

2. Si wageni peke yao ndio waliotuulia makampuni yetu. Kazi hiyo tuliianza wenyewe enzi za Gafco, Cosata, Napco,THB,mahoteli yetu(Kilimanjaro, Mikumi,Mafia etc) n.k. Si makuburu waliyoiua ATC. Ni sisi ambao tuliipeleka mpaka tukawa tunaiita Any Time Cancel, Airline of Total Confusion. Haya majina si dalili za shirika linaloendeshwa vyema. Uongozi mbovu hautegemei rangi. Wa Kenya waliingia ubia na KLM na unaona Kenya Airways inavyoendelea? Sisi tuliwachagua SAA kwa sababu zetu nao wakatusindikiza kaburini. Hakuna mtu anayeweza kukana kuwa hali ya vinywaji imekuwa bora baada ya makaburu kuichukua Tanzania Breweries. Ule wakati chaguo lilikuwa ni kati ya Safari baridi na Safari ya moto tumeishasahau. Ule wakati wa kupata bia kwa vikaratasi tumesahau! Mbona hatuwaoni hao ila tunawang'ang'ania wakina Net Group? Kwani hali ilikuwaje kabla ya wao kufika? Inflated bills mtindo mmoja, kuunganishiwa umeme mpaka umjue mtu! Sisemi kuwa hakuna wazungu matapeli, wapo, tena sana. Ni sisi tunaotakiwa kuwa makini tunapowatafuta watu wa kuingia nao ubia. Tukumbuke hao wote ni wafanyabiashara na hawako hapa ati kwa sababu wana uchungu na Tanzania. Wako hapa kufanya biashara na ku'maximise' profit. Vile vile tusimfunikia maovu mwenzetu ati kwa sababu tunafanana nae rangi. Kama mgeni anauwezo kuliko sisi tukubali hilo, tumkaribishe na tujifunze kutoka kwake. Kama mwenzetu anauwezo nae apewe nafasi ya kuonyesha uwezo wake. Akiboronga ajue hatutamuonea huruma ati kwa vile ni mwenzetu.Ni nani tutasema ana uchungu wa taifa lake mhindi Prof. Shivji au yule wakili mbunge maarufu kutoka Mara? mmoja ni wakili wa wanyonge na mwingine mzawa mwenzetu anadai $500 kwa saa!

Kama vile tunavyopinga kubaguliwa kutokana na rangi yetu,umefika wakati tudai kuhukumiwa kutokana na uwezo wetu na si kudai upendeleo kutokana na rangi yetu. Tutaweza kuendelea hapo tukapoanza kujikosoa wenyewe kwa dhati na kukubali pale ambapo tunaudhaifu badala ya kila saa kupiga hizo kelele za ubaguzi!
 
Back
Top Bottom