Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Pamoja na mambo yake mabaya mengi tu hasa ya kubinya demokrasia, Museveni ameweza kufanya kilichowashinda marais wengi wa kiafrika, ametunga sheria rasmi ya mambo yote yanayohusiasa na ushoga.
Vita ilikuwa kali, vitisho vilikuwa vingi lakini alishikilia msimamo wake.
Wengi wa viongozi wetu hawako tayari kuona ushoga unashaniri kwenye nchi zao, hawapendi kabisa lakini misaada inawaponza, wakitishwa kidogo tu wanakaa kimya huku wakikwepa kabisa kulizungumzia hilo jambo.
Misaada! misaada! misaada! Ndio pingu na gereza la kuifunga Afrika mpaka inashindwa kujiamulia mambo yake mengi kwa uhuru na uwazi.
Pongezi kwako Kaguta Yoweri Museveni. Tunasubiri kuona wengine wanafuata nyayo zako.