- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Uganda president Yoweri museveni says this is the last time he is vying for presidency in Uganda, urges Ugandans to come in large numbers and vote for him for the last time.
- Tunachokijua
- Mwezi Agosti Chama cha NRM nchini Uganda kilimteua Rais Yoweri Museveni kugombea tena urais katika uchaguzi mkuu wa Januari mwakani (2026), hatua itakayompa nafasi ya muhula wa saba.
Museveni mwenye umri wa miaka 80 alichukua madaraka mwaka 1986 na tangu hapo ameshinda chaguzi zote baada ya kuondoa ukomo wa mihula na kikomo cha umri wa kugombea.
Madai
Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo Instagram kumekuwapo na kipande cha video kinachomuonesha Rais wa Uganda Yoweri Museveni akiwahimiza wafuasi wake kujitoleza kwa wingi kupiga kura kwani anagombea Urais kwa mara yake ua mwisho.
Uhalisia wa taarifa hiyo
JamiiCheck imefuatilia na kujiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli.
Ufuatiliaji kwa njia ya mtandao umebaini kuwa video hiyo imehaririwa sauti na haihusiani na mchakato wa uchaguzi unaondelea nchini Uganda kwa sasa.
Utafutaji kwa kutumia google reverse image search, JamiiCheck imebaini kuwa video hiyo imekuwepo mtandaoni kuanzia mwezi wa nane ambapo Rais Museveni alikuwa akihutubia nchini Misri.
Rais Museveni alifanya ziara ya siku tatu nchini Misri kuanzia Agosti 11, na Agosti 12, 2025 alipewa nafasi ya kuzungumza na mwenyeji wake Rais El-Sis ambapo pamoja na mambo mengine Rais Museven alieleza wao na Misri ni rafiki wa muda mrefu huku akisisitiza kuwa umoja wao huo unachagizwa na uwepo wa mto Nile.
Wakati wa hotuba yake hiyo hakuongelea chochote kuhusu uchaguzi wa nchini mwake wala kuhusu Bobi wine na badala yake video zinazosambazwa zimehaririwa kwa kuwekewa sauti nyingine.
Aidha hakuna chanzo chochote cha kuaminika kinachomnukuu Rais Museveni akieleza kuwa baada ya uchaguzi wa mwaka 2026 hatogombea tena.