Nuru
Nuru gizani...Yes hii ndio kanuni ya utakatifu, ndio maana hata Ikulu yetu ni mahali patakatifu, hivyo aliyepo ikulu yetu anapaswa kuwa ni mtakatifu, na ndio maaa sisi wengine tunamuita mtukufu rais!.
Ili kupata uhalali wa kushughulikia utakatifu, kwanza lazima wewe mwenyewe uwe mtakatifu!, hivyo kufuatia Museveni kusimamia mchakato wa utakatifu wa Nyerere, sisi kwetu Museveni anapaswa kuwa mtakatifu, hata kama in reality kule kwao huyu ni shetani, lakini kwetu sisi huyu ni mtakatifu, kwa jinsi ile ile wakati sisi Watanzania kuna watu wanalia na Magufuli, watu wanapigwa risasi 38 mchana kweupe!, miili ya watu inaopolewa kwenye viroba!, watu wanapotea katika mazingira ya kutatanisha, kina Ben Saanane, Azory Gwanda na wengineo!, vifo vya kikatili vya ajabu kama kifo cha kamanda Mawazo!, etc, etc, lakini kuna wenzetu wanatulilia tuwaazime Magufuli wetu awanyooshe hata kwa mwaka mmoja tuu utawatosha!.
P.