Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Nchi inaongozwa kwa sheria, siyo kwa biblia wala msahafu.Lakini pia vitabu vya dini vina sema
"Samehe Saba mara sabini" Yesu Kristu alitufundisha kusamehe hata kama umeumizwa kiasi gani mara ngapi.
Nahisi Musiba aliwatuma viongozi hawa wa kidini wakamuombee msamaha lakini huenda vigezo na masharti havikuzingatiwa, huenda akivizingatia atasamehewa.
Biblia inasema samehe hata saba mara sabini lakini usiubebe mstari huo pekee, soma biblia nzima.
Biblia pia inasema hakuna msamaha bila toba ya kweli. Biblia tena inasema ukienda hekaluni, ukataka kutoa sadaka, halafu ukakambuka ulimtendea visivyo ndugu yako, iacha sadaka yako madhabuhuni, nenda kwanza ukamwombe msamaha ndugu yako kisha uende ukatoe sadaka yako.
Pia ikumbukwe kuwa adhabu kuna wakati huwa ni sehemu ya msamaha. Ndiyo maana mtume Paulo anasema kuwa ukitaka kuonya, onya hata kwa ukali. Ukali unaotajwa hapo ni adhabu, alimradi iwe ninkwa dhamira ya kumrudi aliyepotoka na kutenda uovu.
Viongozi wa dini, wanatakiwa watambue kuwa nyumba za ibada siyo sehemu ya kuhifadhia uovu bali ni sehemu ya upatanisho baada ya kufanya toba ya kweli kwa uliyemkosea , na kwa Mungu wako.