el nino
JF-Expert Member
- Nov 5, 2013
- 4,712
- 5,058
Naandika uzi huu baada ya kuona nyuzi nyingi huku zikizungumzia masuala ya label kama msaada wakati ni biashara.
Hebu fikiria, umekutana na msanii huko mtaani amejaliwa kipaji unaamua kuwekeza fedha nyingi kwake akashoot video South Africa, promotion kwenye redio na Tv, fedha za Kula, kuvaa na matumizi mengine, ili haya yote yafanyike inabidi uyarasimishe kwa kuingia katika makubaliano na kijana huyo mwenye kipaji.
Kwa muktadha huo utakuwa umefanya uwekezaji katika kipaji cha msanii husika ukitegemea kurudisha gharama za uwekezaji na faida. Kichekesho huwa kinakuja baada ya msanii kuanza kupata show mbali mbali na kuona hela zinaingia, kwa akili fupi za wasanii wengi wanakuwa wanataka kuchukua Lions share ya fedha wanazoingiza wakisahau kuwa mpaka wao kupata hizo show kuna hela iliyowekezwa, wanataka uwekezaji uliofanyika kwao ugeuke kuwa msaada au ushkaji .
Muziki ni Biashara Kama biashara nyinginezo na anayewekeza fedha kwenye kipaji cha mtu hana uhakika wa gharama za uwekezaji kurudi achilia mbali faida, hivyo huwa nawashangaa sana wanaolalamika wananyonywa as if walichofanyiwa ni hisani, mfano Diamond alitoa zaidi ya Dola elfu 10 (zaidi ya milioni 22 za kibongo ) kwaajili nyimbo ya Aiyola Peke yake, mpaka kufikia kwangwaru hatujui alikuwa ameshatumia shilingi ngapi na kiasi gani kimerudi hadi sasa, ndio maana Harmonize ameambiwa akitaka kuvunja mkataba lazima hesabu zipigwe Kama akikutwa na deni alipe mzigo wote na vilevile hatimiliki lazima WCB iendelee kufaidika na uwekezaji iliyoufanya.
Kimsingi Muziki ni Biashara Kama biashara nyingine na kuna mstari mnene sana kati ya Biashara ya Muziki na ushkaji