Music Label sio ushkaji ni Biashara

Music Label sio ushkaji ni Biashara

el nino

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2013
Posts
4,712
Reaction score
5,058
Naandika uzi huu baada ya kuona nyuzi nyingi huku zikizungumzia masuala ya label kama msaada wakati ni biashara.

Hebu fikiria, umekutana na msanii huko mtaani amejaliwa kipaji unaamua kuwekeza fedha nyingi kwake akashoot video South Africa, promotion kwenye redio na Tv, fedha za Kula, kuvaa na matumizi mengine, ili haya yote yafanyike inabidi uyarasimishe kwa kuingia katika makubaliano na kijana huyo mwenye kipaji.

Kwa muktadha huo utakuwa umefanya uwekezaji katika kipaji cha msanii husika ukitegemea kurudisha gharama za uwekezaji na faida. Kichekesho huwa kinakuja baada ya msanii kuanza kupata show mbali mbali na kuona hela zinaingia, kwa akili fupi za wasanii wengi wanakuwa wanataka kuchukua Lions share ya fedha wanazoingiza wakisahau kuwa mpaka wao kupata hizo show kuna hela iliyowekezwa, wanataka uwekezaji uliofanyika kwao ugeuke kuwa msaada au ushkaji .

Muziki ni Biashara Kama biashara nyinginezo na anayewekeza fedha kwenye kipaji cha mtu hana uhakika wa gharama za uwekezaji kurudi achilia mbali faida, hivyo huwa nawashangaa sana wanaolalamika wananyonywa as if walichofanyiwa ni hisani, mfano Diamond alitoa zaidi ya Dola elfu 10 (zaidi ya milioni 22 za kibongo ) kwaajili nyimbo ya Aiyola Peke yake, mpaka kufikia kwangwaru hatujui alikuwa ameshatumia shilingi ngapi na kiasi gani kimerudi hadi sasa, ndio maana Harmonize ameambiwa akitaka kuvunja mkataba lazima hesabu zipigwe Kama akikutwa na deni alipe mzigo wote na vilevile hatimiliki lazima WCB iendelee kufaidika na uwekezaji iliyoufanya.


Kimsingi Muziki ni Biashara Kama biashara nyingine na kuna mstari mnene sana kati ya Biashara ya Muziki na ushkaji
 
Harmonize anatakiwa akamuliwe vya kutosha....!!!
 
Mbongo akimtoa kwenye shda Na
Akapata channel za maisha dharau znakuja
Juu anasahau uliko mtoa
 
Wengi wenu mnaelezea hili suala mkiwa biased. Mnaangalia upande mmoja bila kujua ili hio record label ifanye kazi kuna watu wawili - Anaewekeza na anayewekezewa.

Kwa case ya harmo mnapoteza muda. Hii ni ishu ya mpito tu Ku attract attention. Ukitaka kuamini hill angalia email ya booking za harmonize - bado ni ile ile.
 
Si ashasema anawalipa hela zenu mnazomdai

Kwani yeye hajawahi waingizia hela kutokana na show?
 
Binafsi silaumu Harmonize kutoka WASAFI as long as analipa hizo gharama coz hakusain mkataba wa maisha.Ila anapaswa kuendelea kumheshim Diamond maisha yake yote coz bila Mondi Harmonize tusingemjua.Ni Harmonize pekee aliyemcopy Mondi na akatoboa kimziki.Ila somo kubwa wanamuziki wachanga wakishapata majina wanaanza kuvimba na kuona wananyonywa wanasahau nani aliwafikisha hapo walipo sasa.Kila la heri Harmonize hope ulichokikosa WCB utakipata huko uendako.Adios amigo!
 
Binafsi silaumu Harmonize kutoka WASAFI as long as analipa hizo gharama coz hakusain mkataba wa maisha.Ila anapaswa kuendelea kumheshim Diamond maisha yake yote coz bila Mondi Harmonize tusingemjua.Ni Harmonize pekee aliyemcopy Mondi na akatoboa kimziki.Ila somo kubwa wanamuziki wachanga wakishapata majina wanaanza kuvimba na kuona wananyonywa wanasahau nani aliwafikisha hapo walipo sasa.Kila la heri Harmonize hope ulichokikosa WCB utakipata huko uendako.Adios amigo!
Kubebwa na fulani pekee hakutoshi kama msanii mwenyewe kipaji chake ni cha kusuasua. Wapo wasanii wengi walibebwa lakini hawafika mbali kwa sababu walikuwa na vipaji vya ku beep.
Harmonize anastahili pongezi kabebwa akabebeka
Diamond anastahili pomgez kabebwa akabebeka na yeye akawabeba wengine.
Ni wakati wa harmonize kuwabeba wengine.
 
Back
Top Bottom