Mustafa Mkulo aibiwa laptop bungeni (bunge la katiba ) Dodoma

Mustafa Mkulo aibiwa laptop bungeni (bunge la katiba ) Dodoma

Ni aibu kwa wasimamizi wa ulinzi ndani ya bunge, walitakiwa waone hilo tukio kabla ya kutokea (CCTV camera monitoring crew) ambao hawa wana mpaka mtaalamu wa ugunduzi wa sura. Inakuwaje kitendo kama hiki kinatokea ndani ya bunge? kwa hivyo basi kama kuna Mbunge mwenye nia mbaya na taifa anaweza kujitoa mhanga na kujilipua ndani ya bunge na kusimamisha shuguli zote za katiba na mambo muhimu ya kitaifa.

Baada ya tukio kutokea wameshindwa vipi ku trace laptop na hasa kama ilikuwa connected kwa internet ni dakika 3 tu kuijua location yake? Inanikumbusha tukio la kuibwa kwa simu ya balozi ikulu .... da!!!
 
Ndio bunge hilo tunalotegemea litengeneze katiba itakayotutoa hapa tulipo washaanza kulizana? Nasubiri Android za Wizi na mie, where my flashing softwares at,lol
 
mwenye mchezo wa kutafuta nyaraka kwenye laptop za wenzie anajulikana...
 
Hainiingii akilini kitu kama hicho kutokea kwa watu walioaminiwa na kutumwa kufanya kazi kwa niaba yetu sie zaidi ya milioni arobaini.

Naanza kuona giza linaloisonga katiba yetu huko mbele.

Na mkishindwa kuipata niambieni nina msomi wangu wa it ataitafuta hata kama iko darini ataikuta huko;
 
Wacheni kulikosea bunge letu heshima, hizo ni tabia za mtu mmoja mmoja sio wabunge wote. Acha wezi hata mafuska wapo!
 
mwenye mchezo wa kutafuta nyaraka kwenye laptop za wenzie anajulikana...

Wanajulikana majangili pamoja na kiongozi wao aliyoko Arusha, na mambo swaaafi sembuse nyaraka! Muhimu, tuangalie kwa jicho la tatu hili ni Bunge kweli au genge la aina fulani ya watu kama alivyosema Mch. Mtikila kisha tutafakari la kufanya na kisha tufanye.
 
Hilo nalo neno, bilioni nane zote bila camera ndani? Kama camera zipo si tuna re-wind tu mkanda tunamwona mwizi - SIMPLE KWENDA NATEKNOLOGIA!

Mkuu inawezekana mwizi akaonekana ndani ya camera za cctv.. Lakin jee akiwa muheshimiwa wa kuheshimiwa wataweza kumvua nguo..? Rejea yale ya yule muheshimiwa alioonekana akimwaga vitu vyeupe kwenye viti bungeni kwa imani za kishirikina.. Alionekana kwenye cctv lakini ikawa aibu kumtaja lol..
 
Ni aibu kwa wasimamizi wa ulinzi ndani ya bunge, walitakiwa waone hilo tukio kabla ya kutokea (CCTV camera monitoring crew) ambao hawa wana mpaka mtaalamu wa ugunduzi wa sura. Inakuwaje kitendo kama hiki kinatokea ndani ya bunge? kwa hivyo basi kama kuna Mbunge mwenye nia mbaya na taifa anaweza kujitoa mhanga na kujilipua ndani ya bunge na kusimamisha shuguli zote za katiba na mambo muhimu ya kitaifa.

Baada ya tukio kutokea wameshindwa vipi ku trace laptop na hasa kama ilikuwa connected kwa internet ni dakika 3 tu kuijua location yake? Inanikumbusha tukio la kuibwa kwa simu ya balozi ikulu .... da!!!

Bunge hili naliona tofauti kidogo na mabunge mawili yaliyopita

Maafisa usalama walikuwa active sana tofauti na sasa....waliopo wengi ni wazee na mambo nayo yanaenda slow
 
Mtu mzima unatembea na malaya unategemea nini? wacha waibiwe tu zikauzwe udom kwa bei poa si hawataki kuwaongezea vijana posho! na mimi nasema waibiwe tu maana tumechoka sasa.
 
Hainiingii akilini kitu kama hicho kutokea kwa watu walioaminiwa na kutumwa kufanya kazi kwa niaba yetu sie zaidi ya milioni arobaini.

Naanza kuona giza linaloisonga katiba yetu huko mbele.

Na mkishindwa kuipata niambieni nina msomi wangu wa it ataitafuta hata kama iko darini ataikuta huko;

Tatizo ni imeibwa na nani?? akiiba "tall water" anaibadilisha inakuwa kibuyu hata aje mtaalamu wa IT toka wapi haipati.
 
Wanajulikana majangili pamoja na kiongozi wao aliyoko Arusha, na mambo swaaafi sembuse nyaraka! Muhimu, tuangalie kwa jicho la tatu hili ni Bunge kweli au genge la aina fulani ya watu kama alivyosema Mch. Mtikila kisha tutafakari la kufanya na kisha tufanye.

hapa tunatafuta laptop lakini....
 
Kweli Mkulo umelidhalilisha hilo Bunge Letu la Katiba. Ulikuwa wapi mpaka laptop ipotee? Hakuna hata jirani uliyemwambia waenda maliwato kidogo na utarudi? Tatizo ni uchovu wa safari mkuu. Ukasinzia kidogo ndo maana mnapiga marufuku mapaparazi mle ndani.
Mtaibiana sana humo. Huyu alichukia kuona mafaili yake yamepotea, je walioibiwa sm na pochi wakaona aibu kusema si ni wengi humo??
 
hapa tunatafuta laptop lakini....

Kuangalia ulipoangukia badala ya kuangalia ulipojikwaa mpaka ukaanguka, hutafuti suluhu ya jambo. Hata kesho utaanguka tena, kisha utatumia muda kutafuta ulipoangukia badala ya kazi husika! Wengine walioingia hapo mjengoni, laptop kwao ni mara ya kwanza kuona na wanafikiri ni kitu cha thamani sana bila shaka. Information ni muhimu, lakini sio za Mkulo ingawa yumo katika Bunge hilo maalumu la Katiba.
 
Back
Top Bottom