Librarian 105
JF-Expert Member
- May 6, 2023
- 261
- 356
Hili vuguvugu la harakati za Gen Z lililoanzia Kenya kisha kuhamia Uganda hivi karibuni. Ni kiashiria cha mahitaji ya mabadiliko ya kiuchumi na kijamii yenye kupiganiwa na vijana.
Kwa vile mifumo na sera za fedha na ajira limegeuka kupe dhidi yao katika maisha ya kila siku. Walakini viongozi wao wakitia pamba masikioni huku baadhi yao wakidai kuna nchi za kigeni hasa Marekani zinafadhili vuguvugu la harakati hizi.
Kwa upande wa kwetu Tanzania nitoe ushauri Kwa mamlaka : busara ni kujifunza kupitia makosa yako na makosa ya wengine.
Mustakabali wa vuguvugu hili kwetu sisi naona tungali tuna muda wa kujitathmini na kurekebisha sera za ajira, fedha, Kodi na uchumi Kwa ujumla endapo viongozi wetu wataitanguliza Tanzania mbele.
Japokuwa wanaweza kupuuzia kinachoendelea Kwa majirani zetu, ila wahenga walipata kusema " ukiona mwenzako ananyolewa nawe tia maji kichwa chako".
Lakini nikitazama hali halisi tuliyonayo : uchawa na ukoloni mweusi unaweza kufunika kombe ili mwanaharamu apite.