Misimamo mikali ya aina yoyote haifai. Tunakosea sana tunapowagawa makardinali katika makundi mawili haya ya kiholela. Kufanya hivyo ni sawa na kulichukulia Kanisa kama taasisi ya kawaida kama vile IMF au Benki ya Dunia, badala ya kulitazama kama Mwili wa Fumbo wa Kristo.
Baba Mtakatifu ni mrithi wa Mtume Petro na anaitwa kuwa alama inayoonekana ya Kristo – kiongozi anayeakisi uwepo wa Yesu katika Kanisa.
Hata hivyo, hali ya sasa duniani – ikiwemo masuala kama utoaji wa mimba, ushoga, uhamiaji haramu, vita, na wakimbizi – yanahitaji msimamo wa wazi wa Kanisa. Na kwa namna ya kipekee, watu wanatazama kwa makini ni msimamo gani Papa atauchukua kuhusu mambo haya.
Kuwa upande wa mrengo wa kushoto (liberal) kupita kiasi kunaweza kumaanisha kupoteza maana halisi ya Kanisa kama alama ya Kristo duniani. Vilevile, kuwa wa mrengo wa kulia (conservative) mno kunaweza kufanya Kanisa lishindwe kuelezea Injili ya Kristo kwa njia inayoeleweka katika muktadha wa changamoto za dunia ya sasa.
Kwa sababu hiyo, kuna haja ya kuwa na Papa mwenye msimamo wa wastani – mtu anayeweza kuruhusu mabadiliko pale yanapohitajika, bila kupuuza Injili, na wakati huo huo kuilinda taswira ya kweli ya Kanisa, bila kuipoteza kwa kisingizio cha mageuzi.