Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
- Thread starter
- #101
MAMA NA MWANA
Mbawala : shikamoo Mama, nimefukuzwa shuleni.
Mama : marhaba mwanangu Mbawala, hivi ndo nimetoka kijiji cha Mkomanzi kwa rafiki yangu kuchukua pipa nikoroge pombe, nikiuza nitakutumia mwanangu, kazana kusoma.
Mbawala : Sawa mama naomba na pesa ya matumizi, nitashukuru.
Mama: Sawa mwanangu.
Mbawala: Mama shikamoo, nashukuru nilipata ile pesa naomba nisaidie na pesa ya mtihani mama tumeanza usajili.
Mama : Mwanangu sina hela kwa sasa jana tumelalia uji na wadogo zako, nitajitahidi niende kwa Mzee Mwaka nikakope pesa za palizi nitaenda kupalilia shamba kwa wiki nzima, jitahidi usome mwanagu nakuombea, akamaliza chuo.
ukafika muda wa kwenda chuo.
Mbawala : Mama sina pesa kabisa, nimeomba mkopo nimekosa sijui nifanye nini mama.
Mama : Mwanangu kama nimekusomesha kote huko chuo nitashindwaje ??, nipo tayari kujaza madeni usome.
Baada ya kumaliza chuo na kupata kazi nzuri.
Mama : Mbawala siku hizi haunikumbuki mwanangu shida nini ??, hata simu haunipigii mwanangu !!!.
Mbawala : Yaani mama majukumu ya kazi yamekuwa mengi huwezi kuamini, juzi nilikuwa Zanzibar hivi ndiyo nimerudi majuzi hapa Dar, utanisamehe tu mama'ngu.
Mama : Kwani huko Zanzibar kuna mitandao tofauti na ya huku ??
Mbawala : Hapana, halafu mkwe wako mjamzito kwa hiyo muda mwingi nakuwa na mhudumia naporudi nyumbani.
Mama : Mdogo wako amefukuzwa shule kwa ajili ya ada inasumbua, nilichukua pesa kidogo niliyouza pombe nikampa wameenda lakini wamemfukuza tena.
Mbawala : Mama hivi bado unatengeneza pombe ??, hivi BIBLIA inasema nini kuhusu pombe Mama, Hapana Mama hapo unanikwaza kwa kweli.
Mama : Mwanangu kumbuka nimekusomesha kwa kuuza pombe na laiti ungenipunguzia mzigo huu wa kusomesha, na kunituma pesa kidogo za matumizi ningekuwa nimeacha.
Mbawala : Ningekutumia mama'ngu ila sasa hivi ninakimbizana na ujenzi,
hata nikikuahidi sasa hivi nitakudanganya,
nilichukua mkopo benki kwa hiyo wananikata,
nitakupigia baadae kuna simu inaita hapa.
Siku nyingine ikafuata
Mama : mwanangu nataka nije huko mjini kumsalimia mjukuu wangu mwezi huu.
Mbawala : daaahhh, yaani kwa sasa hatuna pesa kabisa mama, mjukuu wako kwa mwezi mmoja tu zimenitoka kama Milioni mbili.
daaahhh, na bahati mbaya zaidi likizo hii mimi na mke wangu tutakuwa UINGEREZA kusherehekea birthday ya mtoto wetu, tukirudi tutafanya utaratibu uje kutusalimia.
Tunakwama wapi watoto ???
niambie tupo akina Mbawala wangapi leo hii..?