Musukuma: Nilikuwa bingwa wa kutorosha dhahabu. Alifilisika na kuuza ngano 'inayoharibika'

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Mbunge wa Geita, Musukuma amesema alikuwa bingwa wa kutorosha dhahabu mpakani akibeba mpaka kilo 50 mwilini.

Musukuma amesema mwaka 1996 alikuwa na umbo dogo kimwili hivyo kuonekana kama mtoto, askari wakishusha watu kwenye basi ili wasachiwe, walikuwa hawasachi watoto hivyo alikuwa hakaguliwi kwakuwa alionekana kama mtoto japo alikuwa na mtoto mmoja tayari.

Kishimba
Musukuma amemtaja mbunge mwenzie, Kishimba kufungua ofisi ya kurudisha fedha kwani pia ilikuwa changamoto kuzifusha.

Kufilisika
Pia ameongea kufilisika mwaka 1998 baada ya kutapeliwa mpaka kuamua kutoroka kwani alikuwa anatafutwa na polisi ilhali yeye alikuwa anawaogopa sana. Alipotoroka alitelekeza familia na kuwa shoe shine Korongwe pamoja na kwamba alishakuwa mfanyabiashara mkubwa namba 3 Mwanza.

Kuibuka tena
Msukuma amesema kuna mfanyabiashara mpakistan alimsaidia wakati ana duka Mwanza, alileta ngano na TRA ikaishikilia na mpaka anafanikiwa kuitoa ilishaanza kuharibika. Ilipotoka akamtafuta msukuma ambae alifanya 'namna' ikauzwa nje. Msukuma amesema ile ngano alikopeshwa kwa miezi mitatu lakini alipouza tu alimlipa mhusika ndani ya siku 5.

Musukuma ameongea hayo leo July 6 wakati akihojiwa kwenye kipindi cha Power breakfast.
 
Akamatwe.
Kwani mtu akitangaza hadharani kuwa alikuwa muuaji ila sasa ameacha serikali itamchekea tu?
Kama aliweza kutorosha mpaka kg 50 kwa mara moja , je, jumla katorosha gunia ngapi za dhahabu kwa kipindi chore?
Serikali imepoteza sh.ngapi?
Ni zaidi ya muuaji
 
Wameanza kutaja siri zao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu ana mambo mengi sana ya kishirikina naona anaanza kufunguka polepole. Tutasikia mengi.


Haha huyu jamaa huyu

Video au audio evidence please

404: Page Not Found

Tupe Link tukasome

Namsikiliza hapa

Yuko radioni

Akamatwe.
Kwani mtu akitangaza hadharani kuwa alikuwa muuaji ila sasa ameacha serikali itamchekea tu?
 
wasukuma ni matapeli na wanafiki sana
 
Mtu anakiri ujangili anaachwa huyu alipwaswa akamatwe haraka
 
Mtu anakiri ujangili anaachwa huyu alipwaswa akamatwe haraka
Sasa huo ndio ujangili? magendo hatujaanza leo jamaa mkweli na hizo biashara mpaka leo watu wanafanya, na kama sote tutakuja hadharani na kuwa wa kweli tumepata wapi mali zote tutaishia jela hakuna msafi humu wewe wala mimi hakuna. Wewe ulitaka wale wanaosema nilianza na alfu 50 tu leo na billion fake people. Musukuma yuko real huwezi kuwa tajiri bila kupiga short cut hata hao kina Mo kama wataongea ukweli wamepiga sehemu..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…