Musukuma: Nilikuwa bingwa wa kutorosha dhahabu. Alifilisika na kuuza ngano 'inayoharibika'

Musukuma: Nilikuwa bingwa wa kutorosha dhahabu. Alifilisika na kuuza ngano 'inayoharibika'

Marekani kuna jamaa mmoja anaitwa vlad Ana podcast yake inaitwa vlad TV
Huwa anawahoji watu maarufu, wasanii nk
Wengine wakihojiwa wanafunga sijui nliuza unga,sijui nliiba nk
Kumbe feds wanafatilia interview zile,jamaa wengi wameokotwa

Ova
I hope na huyu wamkamate na kuangalia mtandao ni kina nani

Yaani jamaa anajitolea ushahidi halafu wanamchekea na yeye anaona ni sawa

Hao wa US bora wana akili kuliko mazombi yetu
Saa hizi ilikuwa awe anahojiwa
 
Ulishawahi sikia jayz akikiri hadharani kuuza cocaine

Ova




Life doesn't come easy you gotta fight hard men unless you wanna be avarage.
NB. Si support drugs ila pambana unavyoweza kuvunja poverty viscous cycle kwenye familia yako.
 
Akamatwe jinai haifutiki. Hii ndio tofauti ya tajiri mwenye shule na asie na shule
kweli mkuu. shule ni muhimu nimemsikiliza muda wakipindi umeisha anaombwa kustopisha mazungumzo bado anaendelea kun'gan'gania mike!!! nidhamu zero yuko on air anatamka neno "pumbavu"

anakiri akiwa na mabasi yake alikuwa akiwatukana matusi madereva na utingo hii ni baada ya mchangiaji mmoja aliyetuma ujumbe kwenye radio na kumsema alikuwa akitukana sana enzi akiwa kwenye ma bus yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijawahi iba wala dhulumu
Faulo za hapa na pale kawaida

Tatizo lako we hujaelewa point
Yangu,huwezi ukawa public figure
Ukaanza kusema,oh mm nliuza unga, niliiba,nliuwa,nilipora
Huo ni ujinga

Ova
hapa ndiko tofauti ilipo kati ya mwenye elimu na asiye na elimu. mwenye elimu hawezi kiri huo upuuzi kwahiyo akiwa kama public figure anatushauri tuibe tuwe kama yeye? Idiot

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akamatwe.
Kwani mtu akitangaza hadharani kuwa alikuwa muuaji ila sasa ameacha serikali itamchekea tu?
Kama aliweza kutorosha mpaka kg 50 kwa mara moja , je, jumla katorosha gunia ngapi za dhahabu kwa kipindi chore?
Serikali imepoteza sh.ngapi?
Ni zaidi ya muuaji
Imepoteza pesa..
 
Msukuma utampenda tu kumsikiliza hata masaa 10, jamaa kuanzia leo shabiki yake ni muwazi sana nani alikuwa anajuwa JPM alikuwa anaendesha Taxi usiku? andika kitabu msukuma ni hatari sana...
Sema JPM alipitia mengi ndo maana alikuwa ana machungu..... yaani uhuni uhuni wote wa town hakuna kitu unaweza mdanganya. Ogopa sana dereva teksi wa usiku.
 
Bongo imeshakuwa kawaida mtu aliyekuwa jambazi kuhojiwa kwenye chombo cha habari. Kuna siku kwa Millard Ayo kuna mtu wa Babati alikuwa anaelezea jinsi alivyokuwa jambazi Nairobi. Nikabaki nashangaa. Siku nchi ikianza kufuata sheria kilio kitakuwa kikubwa sana kwasababu karibu wote tunapata mali kijanja kijanja. Hakuna cha CCM wala CHADEMA linapokuja suala la pesa. Hawa wapinzani waliovaa upinzani feki ukihadithiwa dili zao ni hatari na nusu. Kwa mfano kwenye ule uzi wa KULA TUNDA KIMASIKHARA kuna kesi nyingi mno za ubakaji ni vile tu wahanga waliamua kukaa kimya. TUBADILIKE
 
Hawa ndio wana CCM sasa! Wanatoka kuwa majambazi na kuwa wabunge then mawaziri harafu tuamini wamegeuka kuwa malaika! Na wengine tulisikiaga walikuwa wauza ngada, sijui tuwasubiri waitwe redio mawingu wakiri.
Tusijisahaulishe; jasiri haachi asili.
 
Nchi yetu ni kubwa mnoo,Nchi yetu ni muhimu kuliko yeyote..Nchi yetu itaendelea kudumu miaka 100,200,300,600,1000 ijayo..

Utawala wa sheria ni dhana pana sana na Nguzo muhimu ktk kudumisha,amani,Mshikamano,utulivu na maendeleo..Hakuna alie juu ya sheria..Wananchi wote tuna wajibu wa kutii na kuheshimu sheria zilizowekwa..

Haitokuwa vema kushangilia au kutumbuiza au kishabikia uasi,uovu,uharibifu na unajisi wa sheria..Uhujumu uchumi si kosa dogo..effects yake ni kubwa..

Vyombo vya ulinzi na usalama havipaswi kuruhusu dharau,kejeli na unajisi wa utawala wa sheria na mfumo wa usimamiaji haki..

Confession ya Mh Msukuma ni mtihani na jaribu jingine kwenye mihimili yetu kitaifa..
 
Mbunge wa Geita, Musukuma amesema alikuwa bingwa wa kutorosha dhahabu mpakani akibeba mpaka kilo 50 mwilini.

Musukuma amesema mwaka 1996 alikuwa na umbo dogo kimwili hivyo kuonekana kama mtoto, askari wakishusha watu kwenye basi ili wasachiwe, walikuwa hawasachi watoto hivyo alikuwa hakaguliwi kwakuwa alionekana kama mtoto japo alikuwa na mtoto mmoja tayari.

Kishimba
Musukuma amemtaja mbunge mwenzie, Kishimba kufungua ofisi ya kurudisha fedha kwani pia ilikuwa changamoto kuzifusha.

Kufilisika
Pia ameongea kufilisika mwaka 1998 baada ya kutapeliwa mpaka kuamua kutoroka kwani alikuwa anatafutwa na polisi ilhali yeye alikuwa anawaogopa sana. Alipotoroka alitelekeza familia na kuwa shoe shine Korongwe pamoja na kwamba alishakuwa mfanyabiashara mkubwa namba 3 Mwanza.

Kuibuka tena
Msukuma amesema kuna mfanyabiashara mpakistan alimsaidia wakati ana duka Mwanza, alileta ngano na TRA ikaishikilia na mpaka anafanikiwa kuitoa ilishaanza kuharibika. Ilipotoka akamtafuta msukuma ambae alifanya 'namna' ikauzwa nje. Msukuma amesema ile ngano alikopeshwa kwa miezi mitatu lakini alipouza tu alimlipa mhusika ndani ya siku 5.

Musukuma ameongea hayo leo July 6 wakati akihojiwa kwenye kipindi cha Power breakfast.
Pamoja na yote ilikuwa interview moja tamu sana, uzuri wa Darasa la 7 ni kuongea tu vitu kwa Uhalisia wake bila kuchuja maneno, kama Mlevi tu wa Whisky🤣🤣
 
Hivi ukimsikiliza Musukuma unajifunza kitu gani?!

Huyo jamaa kwangu huwa ni bogus tu, anayetumiwa na wajanja kwa manufaa yao, tena wakati mwingibe hata kuweka rehani maslahi ya taifa.

..hata mimi najiuliza kwanini mtu mwenye criminal record anapewa wasaa wa kuhojiwa ktk kipindi cha redio maarufu?

..hivi jamii yetu imeishiwa watu waliofanikiwa kwa njia halali wa kuhojiwa na vyombo vya habari ili na wengine wajifunze toka kwao?
 
Back
Top Bottom