gimmy's
JF-Expert Member
- Sep 22, 2011
- 3,359
- 3,422
Kuna clip ya Mh Musukuma nimeiona akitaka wahusika ie Waziri wa Fedha na Waziri wa Viwanda na biashara wamfikishie ujumbe mh Rais kwamba hali ya biashara ni mbaya kwani wafanyabiashara wengi wanazidi kufilisika.
Mh Msukuma hivi hizi sheria kandamizi za kodi zinazosababisha wafanyabiashara wanafunga biashara nani alizitunga?
Nakupongeza sana Mh Musukuma walau umeupata ujasiri ukalisemea lakini ninyi wabunge tuliowachagua wengi wenu mwanzoni wakati wafanyabiashara wanalalamika, badala ya kuwatetea ninyi mliwaita wakwepa kodi badala ya kuwasikiliza.
Mitandaoni na hasa humu JamiiForums watu walipiga sana kelele wakieleza namna TRA inavyowafilisi wafanyabiashara lakini ninyi kama wabunge mlikuwa wapi?
Msukuma umesubiri mpaka watu tunamefilisika ndio unaamka kutoka usingizini?
Ok, yaliopita si ndwele tugange yajayo lakini mwelezi rais ukweli.
Mwembieni Rais apunguze kutumia nguvu zaidi, mwambieni huku chini hali ya biashara ni ngumu.
Mwambieni Rais hao anaowaita wanyonge tegemezi lao ni matajiri ambao kwa sasa wengi wanapumulia gesi, sasa ajiulize hali za wanyonge zikoje kwa sasa?
Mwambieni Rais ni kweli amefanikiwa kwani kwa sasa matajiri wanaishi kama mashetani lakini ajue wanyonge nao wanaishi kama misukule.
Mwambieni Rais apunguze kuanzisha miradi mingi kwa wakati mmoja kwani hii ndio chanzo cha tatizo.
Miradi mingi ndio imeletelezea kodi kandamizi na wakati huohuo deni la taifa kuongezeka kwa kasi.
Mwambieni Rais sisi tunaongea wasioyapenda sio kwakuwa hatuipendi Tanzania,pia ajue sisi sio vibaraka wa mabeberu ila sisi tunaitakia mema nchi yetu.
Nimalizie kwakusema Waziri wa Viwanda na Biashara na Waziri wa Fedha kama wanamuogopa na wanashindwa kumshauri Rais ni vema wakajiuzulu.