Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Idara ya Usalama wa Taifa unaoifanya iwe chini ya Usimamizi wa Rais watua Bungeni

Mabadiliko ni muhimu,ingawa yanahitaji elites na maoni ya wadau mbalimbali kwenye nyanja za ulinzi na usalama kabla ya kuwafikia waheshimiwa wabunge.
Ni vizuri kuchakata na kupitia neno kwa neno,kifungu kwa kifungu ili kama kuna mapendekezo au mabadiliko yeyote yawe kama mbadala wakati wa mijadala ya kibunge.
 
Haya ni maandalizi ya uchaguzi ujao, jamaa hawataki kutoka madarakani kwa kura. Kumbuka ni idara hii iliyoratibu wizi wa kura katika chaguzi ziliozopita. Mbowe maridhiano yako na Samia ni kiinimacho
Sio kwamba maridhiano ni takwa la kisaisa na hayagusi Sheria ya uanzishaji wa Idara husika?
Au mnasemaje wadau....!!?
 
Mama Samia haeleweki mara baridi mara Moto. Kwa hivyo maafisa usalama wakiua mtu kwenye utekelezaji wao wa majukumu sio kosa.
 
TISS wanaomba ruhusa kuwatesa zaidi watu wanaowakamata. TISS pia wanaomba wasishtakiwe kwa makosa yoyote wanayofanya.

On the surface, it would seem to be very frightening. Lakini mimi nadhani inafaa TISS wapewe kila wanachohitaji kuilinda nchi.

Kuna sheria katika kila kitu,na hizi Security Services duniani kote zinafanya kazi according to certain fixed rules.
Mimi nashauri TISS wapewe wanachotaka. Kushauri ni serious business. Kwa sababu mambo yakiharibika watu wanauliza,"Ni nani aliyetushauri kufanya hivi?"

Imeandikwa katika Biblia_And ye shall be guiltless before the Lord and before Israel"Numbers chapter 32 verse 22. Kwamba usifanye makosa mbele ya Mungu,na usifanye makosa mbele ya Taifa lako.
 
We Una uhakika wanaotaka haya ni TISS?

Unaamini TISS walikaa Kwa umoja wao wakaona wanahitaji sheria hii?

Binafsi naamini wanaotaka haya ni wanasiasa...TISS wanapokea maagizo kutoka Kwa wanasiasa na wao wameona sasa Bora iwepo sheria ...just in case huyo mwanasiasa ikitokea hayupo wasiulizwe maswali
 
Eti eeeh , haya bhana.. uzuri malipo ni hapa hapa...
unafikiri shida ipo kwangu

Shida ipo kwa wanaotunga hayo masheria mabovu lakini hata nikipinga haisaidii bali nitajiumiza tu roho yangu bora niache hivyo hivyo

Mambo yaende yatakavyotaka kwenda potelea pote
 
TISS wanatuhumiwa kuwaua Ben Saanane, Azory Gwanda; Pamoja na kumpiga risasi Tundu Lissu.
Ikiwa ni kweli, basi hawapaswi kupewa kinga yoyote ya kutoshitakiwa.
Hakuna binadamu yeyote duniani mwenyewe mamlaka ya kuua binadamu mwenzake.
 
TISS wanatuhumiwa kuwaua Ben Saanane, Azory Gwanda; Pamoja na kumpiga risasi Tundu Lissu.
Ikiwa ni kweli, basi hawapaswi kupewa kinga yoyote ya kutoshitakiwa.
Hakuna binadamu yeyote duniani mwenyewe mamlaka ya kuua binadamu mwenzake.
Ben Saanane na Tundu Lissu waulizwe Chadema Azory Gwanda waulizwe uamsho na magazeti ya Kenya. Kubenea na Kibanda waulizwe vifo Muhimbili wakati CHADEMA wakihamasisha madaktari wagome
 
Madhara ya marekebisho ya sheria ya usalama wa taif kufanyika mwaka 2023 yameanza kuonekana bayana mwaka 2024 mtu kuruhusiwa kuvaa matendo ya kinyama dhidi ya binadamu pasipo kuhojiwa na kufanywa chochote (immunity)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…