Hii imetokea leo mapema.source afande wa oysterbay
nina mashaka hizi ni propaganda za kiinteligensia ya polisi ili kuhamisha mawazo ya watu kutoka kwenye movie ya Lwakatare waliyoshindwa kuuthibitishia umma wa watanzania kuwa ni yake. watz walikuwa wanaona chenga na ukungu mzito, movie haikuonekana na wameshindwa kurudi studio kurekebisha, tusubiri tutaambiwa kuna gaidi mwingine amekatwa mwanza au kokote usikokujua tena wanweza kusema ni member wa alikaida na safari hii anaweza kuwa mwarabu koko ili kughilibu fikra za watz
fuatilia ndio utajua hili, hakuna wakati wowote ule ambao serikali ilikuwa imebanwa na kushindwa kujibu tuhuma za kweli palikosekana tukio la kuhamisha akili za watu , mfiano michache tu...
1. kipindi watu wakiandamana kushinikiza serikali isilipe fedha za Richmondi na iwashughulikie mafisadi wa EPA, mabomu ya Gongo la Mboto yalilipuka,
2. pindi madai ya fidia na kujengewa nyumba kutokana na uharibifu huo kutokea, babu wa loliondo alitokea na kupewa nguvu kubwa na serikali yote kuanzia mkuu wa kaya
3. .. likatokea la dr. ulimboka, kupoza hali ya hewa akakamatwa mkenya feki,
4. kabla la dr. ulimboka halijaisha yakatokea mengi tu yakiwemo watu kuuawa na police katika mikutano ya chadema, kuuawa mwandishi Daudi mwangosi kisha la kibanda, la kibanda lilipokosa majibu likatokea la lwakatare n.k
hii ndio system ya usalam wa taifa inavyofanya kazi kwa kushirikiana na majeshi yetu
ww fuatilia watu wakiwabana kumjua huyo muuaji majibu halisi yatakosekana na litaibuka jambo jipya la kuwasahaulisha la kwanza
haya ndio maisha ndio maana neno serikali linatokana na neno siri kali