Muuaji anayetumia pikipiki akamatwa na polisi maeneo ya Tabata Dar es salaam

Muuaji anayetumia pikipiki akamatwa na polisi maeneo ya Tabata Dar es salaam

Madam amekamatwa tungependa awekwe hadharani ili watu wamtambue huenda wangetoa mengi zaidi kwa wale watakao mtambua.
 
si ile thread nyingne kuna mt alisema amekutana nae uso kwa uso segerea?sa ni nini tena?

Yule wa Segerea ni yule aliyekuwa anaua wake za watu gesti, huyu sniper wa bodaboda ni mwingine...
 
Kwa usalama wa watanzania mods fanyeni hima muweke picha ya huyu serial killer hapa. Please do the needful!!! Pengine wako wengine nyuma yake.
 
semeni ni nani huyo mbona hamfafanui? wengine hatujui huyo jamaa ni nani!
 
Hii imetokea leo mapema.source afande wa oysterbay

nina mashaka hizi ni propaganda za kiinteligensia ya polisi ili kuhamisha mawazo ya watu kutoka kwenye movie ya Lwakatare waliyoshindwa kuuthibitishia umma wa watanzania kuwa ni yake. watz walikuwa wanaona chenga na ukungu mzito, movie haikuonekana na wameshindwa kurudi studio kurekebisha, tusubiri tutaambiwa kuna gaidi mwingine amekatwa mwanza au kokote usikokujua tena wanweza kusema ni member wa alikaida na safari hii anaweza kuwa mwarabu koko ili kughilibu fikra za watz

fuatilia ndio utajua hili, hakuna wakati wowote ule ambao serikali ilikuwa imebanwa na kushindwa kujibu tuhuma za kweli palikosekana tukio la kuhamisha akili za watu , mfiano michache tu...
1. kipindi watu wakiandamana kushinikiza serikali isilipe fedha za Richmondi na iwashughulikie mafisadi wa EPA, mabomu ya Gongo la Mboto yalilipuka,
2. pindi madai ya fidia na kujengewa nyumba kutokana na uharibifu huo kutokea, babu wa loliondo alitokea na kupewa nguvu kubwa na serikali yote kuanzia mkuu wa kaya
3. .. likatokea la dr. ulimboka, kupoza hali ya hewa akakamatwa mkenya feki,
4. kabla la dr. ulimboka halijaisha yakatokea mengi tu yakiwemo watu kuuawa na police katika mikutano ya chadema, kuuawa mwandishi Daudi mwangosi kisha la kibanda, la kibanda lilipokosa majibu likatokea la lwakatare n.k

hii ndio system ya usalam wa taifa inavyofanya kazi kwa kushirikiana na majeshi yetu

ww fuatilia watu wakiwabana kumjua huyo muuaji majibu halisi yatakosekana na litaibuka jambo jipya la kuwasahaulisha la kwanza

haya ndio maisha ndio maana neno serikali linatokana na neno siri kali
 
kakamatwa nilikwenda oysterbay na kamanda swai alithibitisha.walimpeleka sitaki shari.kakutwa na bunduki 3 moja ndio ya halali.confirmed
 
kakamatwa nilikwenda oysterbay na kamanda swai alithibitisha.walimpeleka sitaki shari.kakutwa na bunduki 3 moja ndio ya halali.confirmed

Mkuu Ndevu Mzazi, kwa kweli unatunyima raha wenzako maana unapoleta ujumbe kama huu ambao ulisubiriwa kwa hamu sana na kwa mda mrefu ulichotakiwa kutupatia ni jinsi alivyokamatwa muda na wahusika wa ukamataji. Alikiri nini na mambo mengine kama hayo. Lakini umeleta short and clear kisha ukakaa kimya tena hutaki hata kuulizwa. Bwana lete uhondo huo maana hakukamatwa kirahisi tupe hao waliomkamata walijuaje kuwa ndiye na kadhalika......
 
kakamatwa nilikwenda oysterbay na kamanda swai alithibitisha.walimpeleka sitaki shari.kakutwa na bunduki 3 moja ndio ya halali.confirmed
Inawezekana raia ukabeba bunduki ukiwa katika pikipiki na isionekane? Labda iwe ni usiku na uwe umevaa koti refu. Mimi nilidhani alikuwa akitumia bastola/pistol.
 
Gavar nilopata hivi punde kwamba muuaji wa padri zanzibar kashapatika na jina lake omari mussa mkaazi wa mwanakwerekwe zanzibar.
 
source pliiz..ni habari sensitive sana hii.
 
si polisi wamemjibu Pengo kuwa muuaji sio kondoo...
 
Good job Ditective walifikiri inahitaji fedha zakigen ili kukamatwa tatizo lao wanafikiri watu hawana akili haya sasa The Hagy ileeee
 
Dah! Mkuu source muhim sn, na hata km amekamatwa bado ni mshukiwa tu hadi pale mahakama itakapothibitisha uhusika wake baada ya kupitia na kusikiliza ushahidiwa pande zote mbili
 
si polisi wamemjibu Pengo kuwa muuaji sio kondoo...

Kama kanisa huyu DCP Isaya Mngulu hatakiwi kupewa wala kuhiriki sakaramenti yeyote ndani ya kanisa unless awe mpagani, hawezi kumjibu kiongozi wa kiroho maneno ya kejeli kama hayo, Mungu atamuadhibu kama alivyofanya kwa bosi wake DCI Manumba ambaye haja zake zote alizitimiza kitandani.
 
Back
Top Bottom