Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 7,672
- 9,039
View attachment 2598986
Japo nalaani mauaji ya kinyama yaliyofanyika huko Kilifi Kenya, nina wasiwasi kama sheria zetu za kiingereza zinaweza kumtia hatiani.
Zifuatazo ni sababu nuzuhu za kisheria:
Mosi, si rahisi kuthibitisha kuwa Mackenzie aliwashawishi wahanga kutokula. Na kama aliwashawishi, si kosa kumshawishi mtu kufanya kitu anachoamini binafsi kina tija. Dini zote zinaendeshwa kwa ushawishi. Ndiyo maana zimeruhusiwa kufanya uhuni wote bila kufungiwa, kuchunguzwa wala kushitakiwa. Wahusika waliamua kwa hiari yao wakiwa na akili timamu kufunga hadi kufa wakiamini walichoambiwa yaani pepo au kukutana na Bwana.
Pili, Hakuna namna waendesha mashtaka watathibitisha mashtaka yao bila wahanga kuwapo ili watoe ushahidi. Kama Mackenzie hakuwapa sumu au kuwaua kwa kuwanyonga au kwa namna nyingine zaidi ya kuwaaminisha, hana hatia hata kidogo. Rejea wanaoahidi kutenda miujiza ya kuondoa watu kwenye umaskini na kuishia kuwaibia na kuwafanya maskini na watumwa zaidi. Hata wahanga wakifufuliwa, hawawezi kuthibitisha kuwa walilazimishwa kufunga wakijua walichokuwa wakifanya na matokeo yake.
Tatu, sheria za kiingereza zinamtaka anayedai kuthibitisha madai yake. Si rahisi washitaki kuthibitisha kuwa Mackenzie aliwarubuni zaidi ya kuwahubiri nao kwa hiari yao , wakiwa watu wazima wakaamini na kutekeleza.
Nne hata akifunguliwa kwa makosa ya kuua watoto, hawampati kwa vile halikuwa jukumu lake kisheria kuangalia wale watoto zaidi ya wazazi wao. Rejea mnavyobatiza au kuingiza watoto wadogo kwenye dini zenu.
Mwisho, kwa vile dini zote zinatumia mfumo ule ule, kumpata Mackenzie na hatia, ima bunge litunge sheria mpya ambayo nayo itagonga mwamba kwa vile itakuwa illegal tokana kuwa retrospective au wafute dini kwanza ndipo mhusika ashikiwe.
Hata hivyo, itakuwa vigumu kumfunga vinginevyo wamuonee. Akipatikana na hatia si ya mauji bali uzembe au kuficha vifo na vitu kama hivyo ambavyo navyo kisheria, kama atapata wanasheria mahiri anaweza kushida.
Akifungwa, basi iwe ni kama kwenye kesi ya Mwamwindi baada ya kumuua Dk Kleruu.
Somo kubwa hapa ni kwamba tunaendeshwa na mifumo mibovu ya dhuluma