TataMadiba
JF-Expert Member
- Feb 7, 2014
- 9,879
- 5,765
Aliyekuwa Kiongozi wa Kundi la kihalifu la South Side Compton Crips Nchini Marekani, 63, Duane “Keffe D” Davis, amehukumiwa kifungo cha miaka 40 hadi maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kuhusika katika kupanga mauaji ya Rapa maarufu duniani, Tupac Shakur, yaliyotokea mwaka 1996 Jijini Las Vegas.
Hukumu hiyo imetolewa Oktoba 13, 2026, katika Mahakama ya Las Vegas, Marekani, na Jaji Carli Kierny baada ya Davis kutiwa hatiani mwezi Agosti kwa kosa la mauaji ya kukusudia kwa kutumia silaha hatari.
Davis ambaye ndiye Mtu pekee aliyewahi kufunguliwa mashtaka kuhusiana na mauaji ya Tupac, hatakuwa na sifa ya kuomba msamaha wa kuachiwa kwa masharti hadi atakapofikisha angalau umri wa miaka 100, hata baada ya kuzingatia muda ambao tayari amekaa kizuizini.
Mauaji ya Tupac yalitokea Septemba 1996, wakati Rapa huyo aliposhambuliwa kwa risasi akiwa ndani ya gari karibu na eneo la Las Vegas Strip, akiwa na umri wa miaka 25 ambapo kwa miaka mingi, mauaji hayo yalibaki kuwa kitendawili hadi Davis alipoanza kueleza hadharani kuhusu tukio hilo kupitia mahojiano mbalimbali na kitabu chake, jambo lililochangia kufunguliwa upya kwa uchunguzi wa mauaji