Duh! Aisee bro. acha kupotosha watu kwa mafundisho yasiyo na pumzi ya uhai. Biblia yenyewe imetamka Divai(pombe) wewe unatuambia Roho Mtakatifu!!!!. Yani washerehekeaji katika harusi za enzi hizo walikuwa wakinywa roho mtakatifu halafu ikatokea huyo roho mtakatifu akaisha ndipo ikambidi Yesu atengeneze roho mtakatifu mwingine??? Je, kuna madaraja (Grades) ya Roho Mtakatifu? Hili swali linakuja kwani walipokunywa yale maji yaliyopata kugeuka kuwa divai watu walimhoji mkuu wa meza (Master of ceremony) mbona hii divai nzuri hivi imewekwa (imefichwa) hadi mwishoni tofauti na desturi kwamba divai iliyo njema hunywewa mwanzoni halafu ndipo baadaye huletwa iliyo dhaifu?
Kitendo cha Yesu kuongeza divai(Pombe) ni ishara wazi na ya kuthibitisha kwamba Yesu hapingi na hakatazi (Ni ruksa)unywaji wa pombe. Ni bahati mbaya kwamba maandiko hayasemi kama Yesu alikunywa au hakunywa. .
Maandiko hayana bahati mbaya ndugu. Labda tu kukusaidia ili ujifunze, maandiko SIO novel kwamba uyasome kama hadithi za abunuwasi. Maandiko yanataka TAFAKARI. Niliposema divai na habari za Roho Mtakatifu sikuwa mlevi bali nikitumia tafakari ya maandiko. Sina muda wa kuandika sana ila nakupa tafakari kidogo tu:
1.
Kumbukumbu la Torati 14 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
²³ Nawe utakula mbele za Bwana, Mungu wako, mahali atakapochagua apakalishe jina lake, zaka ya nafaka zako, na divai yako, na mafuta yako, na wazaliwa wa kwanza wa makundi yako ya ng'ombe na ya kondoo; ili
upate kujifunza kumcha Bwana, Mungu wako, daima.
²⁴ Na njia ikiwa ndefu mno nawe, usiweze kuzichukua kwa kuwa mahali ni mbali nawe mno atakapochagua Bwana, Mungu wako, apakalishe jina lake, hapo atakapokubarikia Bwana, Mungu wako;
²⁵ ndipo uzibadili ziwe fedha, na kufunga zile fedha uende nazo mkononi mwako, hata
mahali atakapochagua Bwana, Mungu wako;
²⁶ na zile fedha zitumie kwa cho chote itakachotamani roho yako, ng'ombe, au kondoo, au divai, au kileo, au roho yako itakacho kwako cho chote; nawe utakula huko mbele za Bwana, Mungu wako;
tena furahi, wewe na nyumba yako;
²⁷ na Mlawi aliye ndani ya malango yako usimwache, kwani hana fungu wala urithi pamoja nawe.
Sasa katika Agano la Kale divai ilinywewa MAHALI ALIPOPACHAGUA MUNGU, sio kila mahali. Ingawa Waisraeli walijinywea ty, lakini agano la Mungu linasema hivyo. Lengo ni hili:
1. Wajifunze kumcha Mungu
2. Wapate kufurahi katika Bwana
Haya yote leo hii yapo katika Roho. Hatujifunzi kumcha Mungu kwa kunywa bia bali kuongozwa na Roho Mtakatifu.
Warumi 14 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁶ Basi, huo wema wenu usitajwe kwa ubaya.
¹⁷ Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni
haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu.
Waisraeli walikuwa wakiiendea nchi ya ahadi Kanaani, lakini sisi nchi yetu ya ahadi ni katika roho, sio ya kimwili.
2. HARUSI KANA YA GALILAYA - hoja yako imeonyesha jinsi gani huyafahamu maandiko.
Yohana 2:
John
3 Hata divai ilipowatindikia, mamaye Yesu akamwambia, Hawana divai.
3 And when they ran out of wine, the mother of Jesus said to Him, "They have no wine."
4 Yesu akamwambia, Mama, tuna nini mimi nawe?
Saa yangu haijawadia.
4 Jesus said to her, "Woman, what does
your concern have to do with Me? My hour has not yet come."
Nimekuwekea tafsiri ya Kiingereza rahisi uweze kupata uhalisia wa kile alichosema Yesu Kristo. Tafsiri ya Kiswahili imepotosha ukweli.
Angalia pale aliposema saa yangu haijawadia, hapo ndipo penye siri inayohitaji tafakari. Saa ipi? Kwa vipi bado? Kwa Mariamu divai aliichukulia kama kiburudisho tu, lakini kwa Yesu Kristo ilikuwa na maana kubwa kiroho. Mara zote Yesu alisema kuwa yeye ni MZABIBU WA KWELI. Kwani hizi zabibu za kawaida zilikuwa feki? Na kama Yesu ni mzabibu WA KWELI basi saa ya yeye kutoa DIVAI MPYA ilikuwa HAIJAWADIA. Ndio maana ya kusema SAA YANGU HAIJAWADIA. Akawapa divai waliyozowea wanywe wafurahi KAMA ILIVYO DESTURI (kwenye harusi/sherehe na wakati wa chakula ilikuwa desturi za Mayahudi). Sasa ukisema Yesu huko Kana alitengeneza Roho unakosa ufahamu, kumbuka wakati akiwa duniani hakuwa amemwachilia Roho Mtakatifu mpaka alipopaa, ndio maana aliwapa divai ya kawaida tu.
Yohana 12 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
²⁷ Sasa roho yangu imefadhaika; nami nisemeje? Baba, uniokoe katika saa hii? Lakini ni kwa ajili ya hayo
nilivyoifikia saa hii.
Sasa uneona saa aliyokusudia Yesu Kristo? Jiulize saa hii ya kuteswa na kusulubiwa mpaka kifo inahusiana vipi na DIVAI? "Mimi ni mzabibu wa kweli na Baba yangu ni mkulima.. Yoh 15". Kwa kufa na kufufuka kwake alitupatia divai mpya kwa damu yake.
Mathayo 26 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
²⁷ Akakitwaa kikombe, akashukuru, akawapa, akisema, Nyweni nyote katika hiki;
²⁸ kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi.
²⁹
Lakini nawaambieni, Sitakunywa kabisa tangu sasa uzao huu wa mzabibu, hata siku ile nitakapokunywa mpya pamoja nanyi katika ufalme wa Baba yangu.
Tafakari, ni ufalme upi huo? Yesu Kristo aliwapa DIVAI halafu akasema ni DAMU yake. Hilo ndilo agano Jipya, agano la milele. Yesu Kristo anasema "sitokunywa kabisa TANGU SASA..." kwa sababu saa yake IMEFIKA, atakapotoa DIVAI MPYA kwa ajili yao wote walioalikwa kwenye karamu ya mwanakondoo, sio baa. Tangu saa ile divai mpya ni Roho Mtakatifu, yale mnywayo makanisani ni kumbukumbu tu, habari za baa hakuna. Divai mpya hunywewa kwenye ufalme wa Mungu pamoja na Kristo ambaye ndiye mzabibu wa kweli. Roho Mtakatifu ndiye atuingizaye kwenye ufalme wa Mungu.
Kwenye Agano la Kale divai ndio iliburudisha moyo, hii ilikuwa
KIVULI cha mambo yajayo, Roho Mtakatifu. Walikunywa DIVAI ya nchi ya ahadi, nasi tunakunywa
DIVAI MPYA pamoja na Kristo katika nchi ya ahadi. Kama huna Roho Mtakatifu huwezi kuelewa fundisho hili kamwe, hasa kama wewe ni mlevi.
Mfanano:
Agano la Kale walikunywa divai mahali
ALIPOPACHAGUA MUNGU. Agano Jipya tunakunywa DIVAI kama kumbukumbu mahali
ALIPOPACHAGUA MUNGU, sio baa:
1 Wakorintho 11 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
²⁰ Basi mkutanikapo pamoja
haiwezekani kula chakula cha Bwana;
²¹ kwa maana kila mmoja hutangulia kutwaa chakula chake katika kule kula; hata
huyu ana njaa, na
huyu amelewa.
²² Je!
Hamna nyumba za kulia na
kunywea? Au
mnalidharau kanisa la Mungu, na kuwatahayarisha hao wasio na kitu? Niwaambieni? Niwasifu? La! Siwasifu kwa ajili ya hayo.
Ona sasa, wakorintho walikumbwa na wimbi la ulevi (kama wanaopigania pombe makanisani leo hii), sababu ikiwa wanakimbilia kujichotea chakula kingi cha kushiba, tena walevi hujimiminia divai nyingi wapate kulewa. Hili lilivuruga kabisa kusudio la meza ya Bwana, ambayo ni kufanya kumbukumbu tu.
Paulo anauliza kama hakuna mabaa na vilabu vya pombe mpaka kuleta dharau kubwa namna hiyo kwenye Kanisa. Kwamba ulevi kwa wana wa Mungu ni dharau kubwa kwa Mungu.
Sasa nimepata kuwasikia wahubiri mbalimbali wakisema, Paulo anamaanisha WANGEKWENDA KUNYWA BAA, huu ni uongo. Anapouliza kwani hamna nyumba za kunywea anasema kama mmechagua kuwa wanywaji mwende kwenye nyumba maalum kwa hilo, mfano baa, ambazo huko HAKUNA UTUKUFU WA MUNGU bali shetani anatamalaki.
…
²⁵ Na vivi hivi baada ya kula akakitwaa kikombe, akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu;
fanyeni hivi kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu.
Niendelee? Yapo mengi sana yapasayo tafakari, nami nayasema kwa kifupi:
1. Je, wajua walawi MAKUHANI hawakuruhusiwa kabisa kunywa divai waingiapo mbele za Bwana wasije kufa? Sasa leo hii waamini WOTE ni walawi kwani tumeitwa kuwa UFALME WA MAKUHANI (Ufunuo 5:9,10). Tena sisi ni hekalu la Roho Mtakatifu, hivyo MUDA WOTE TUNAPASWA KUWA MBELE ZA MUNGU.
2. Siku ya Pentekoste wanafunzi walidhaniwa wamelewa, hiyo ndio divai mpya kwenye ufalme wa Mungu.
3. Yohana Mbatizaji hakugusa divai ili aongozwe na Roho Mtakatifu.
4. Mithali inaonya kuwa mvinyo hauwafai wafalme, leo hii waamini tumeitwa kuwa wafalme na makuhani, hivyo mvinyo hautufai.
Mithali 31 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁴ Ee Lemueli, kunywa mvinyo hakuwafai wafalme, hakuwafai wafalme; Wala haifai wakuu waseme, Ki wapi kileo?
⁵ Wasije wakanywa na kuisahau sheria, Na kuipotosha hukumu ya mtu aliye taabuni.
5. Ufalme wa Mungu unatekwa na wenye nguvu, sasa kama wewe huwezi kuutiisha mwili kwenye pombe, utawezaje kuuteka ufalme?
6. Usijenge furaha yako kwenye mambo ya kuharibika bali afadhali kuviuza vyote uununue ufalme wa Mungu. Achana na KULILIA ULEVI kwa visingizio eti Yesu Kristo aligeuza maji kuwa divai. Ukimuua kweli itakuweka huru.
7. Jifunze kupitia maisha ya mitume na Kanisa la kwanza (Matendo ya mitume) tena usitegemee tafsiri za kisasa za viongozi wa makanisa.
MWISHO KUMBUKA WEWE NI KUHANI NA HEKALU LA ROHO MTAKATIFU, SIO ROHO MTAKA POMBE.