Muundo wa Muungano: Tanganyika tunataka 'Serikali moja, nchi moja, taifa moja'!

Kwa kweli ni upuuzi; as a matter of fact ni kana kwamba hawajui hesabu za seti! Hivi Mbunge mwanamke atakuwa anawakilisha wanawake tu kwenye hilo jimbo na Mwanaume atawakilisha wanaume watupu?


kasome katiba ya kenya na nchi nyingine, ndo njia pekee ya kuachana na viti maalumu, hata sasa hujui kuwa kila mkoa una mbunge mwananmke wa viti maalumu? tofauti ni kuwa sasa tutawapigia kura na hawatateuliwa na vyama vyao! it is the best idea.

hili la serikali moja haliwezekani, warioba anakumbuka alikuwa mwasisi wa hili kwenye lile kundi la g55 lakini ilishindikana
 
Tunataka serikali moja.Zaidi ya hapo ni mbwembwe za makundi masilahi.Kama serikali moja hatutaki bora kila nchi isimame ki vyake ila jina la tanganyika lazma libadilishwe.Hilo jina kwa sasa halina mvuto tena kulirudisha.
 


Kuna msemo; Ukila na kipofu usimguse mkono. Sasa hayo hatuwezi kuyazungumza sasa, tutamchokoza bure mzee wetu mwanakijiji.
 

As you said, that is next to impossible kwa upande wa zanzibar. Kumbuka Ismail ameshasema kuwa tunadai mambo saba yaliyobaki.
Halafu rasimu inapendekeza kuwa nchi washirika warusiwe kuingia mikataba na nchi au mashirika ya kimataifa. Kwa hiyo, kwa pendekezo lako itakuwa ngumu hawa mawaziri wakuu kuingia mikataba ya kimataifa bila rais wa Muungano. Rasimu inasema watatoa ( wataomba ruhusa tu?) taarifa kwa serikali ya MUUNGANO tu.
 
Hapa pia naunga mkono hoja.
 

Zanzibar hivi sasa wana CAG yao, Katiba ya Muungano inamtambuo CAG aliyeko Tanzania bara ambaye ndiye hukagua hesabu za mambo ya Muungano na yale ya Tanzania bara lakini Zanziba hatii mguu......huu ni mmoja wa mikanganyo iliyoko kwenye serikali mbili
 

Kwenye bold nyeusi nakubaliana na wewe. Kitu ambacho sijakipata hapo kwenye red una maana zanzibar inabaki kama nchi au na yenyewe ina kuwa na Majimbo yenye serikali zake kama huku tanganyika?
 
Mzee Mwanakijiji, The history of constitution making in peacetime demonstrates that,unless consensus is built on the draft through realistic pre-negotiations by the protagonists in full realization that whatever the results, the country has to move on, the process becomes flawed and counter productive. Observers of Tanzania's political scene fear that, unless the issue of the referendum is handled cautiously, the country might cease to exist as we know today. The fact that democratic traction has failed to hold and corruption in all its manifestation continue to drain national resources, Tanzanians should brace for hard times.
 
Serikali moja tosha kabisa, wabunge 50 bara na 2 tu Zanzibar . Awepo Makamu wa Rais au Waziri Mkuu.
 
Naunga mkono hoja,hakika wewe ni mzalendo,uchu wa uroho wa watu unahofia hili,mzigo wa serikali tatu haukubaliki hata kidogo mailings,serilali moja taifa moja
 
Wakenya wameanzisha upuuzi huu kwenye uchaguzi uliopita. Tunalo tatizo la kuiga mambo ya kijinga na kuacha yale yenye manufaa kwa jamii.
 
Ndiyo serikali moja ya Tanganyika!Hakuna ulazima wa Muungano.
 

Mkuu hapo kwenye Red natofautiana na wewe,
Mosi, Karume aligombana na wenzake kwenye NEC akitaka wazanzibar wasikilizwe maoni yao kuhusu Muungano. Akawatukana wenzake kwenye NEC kuwa wana vichwa kama SAMAKI. Je, unajua kuwa alikuwa anatetea Zbar kujitenga na yeye ndo Mkiti wa Taifa za Zanzibar Mstaafu?

Pili, Maalim Seif ameshasema majuzi kuwa Karume na Kamando Salmin marais wastaafu wote kutoka ccm wanaunga mkono hoja ya Zanzibar kuwa serikali huru. Wenyewe hao marais mpaka leo hawajakanusha kauli Maalim Seif. CCM kupitia kwa msemaji wao wakawasemea kuwa siyo kweli. Wanasema Maalim Seif anawagonganisha marais wastaafu na Rais Shein. Umeshajiuliza kwa nini hawa Karume na Dr Salmini hawaendi public na kukanusha kauli ya Maalim seif kama siyo kweli. Kiukweli wanzabar wote ccm na CUF lao ni mmoja --- zanzibar huru.
Na kwa taarifa yako, hii ndo ilikuwa siri ya kuunganisha CUF na CCM au Karume na Maalim Seif.
 
mzee mwanakijiji, naomba nitofautiane kabisa na wewe, kwanza hebu fikiria ukija na wazo la serikali moja wazanzibari watareact vipi! ndio utakuwa mwanzo wa kuanzishwa vikundi vya revolution struggle! umeshalifikilia hilo?

kwa sasa tuu na muundo uliopo wa serikali mbili kuna kundi linaona limemezwa! je itakuwaje pindi litakapo mezwa kwe na kuwa na serikali moja? si tutakuwa tunajitangazia vita?

kwa upande wangu naona kwa uhuru na usalama wa pande zote mbili serikali tatu itawapa amani wazanzibari! na hata huku kwetu pia! hebu zama ufikiri kiundani kidoogo
 
kwa ujumla suala hili lina kaunafiki kanako wakabili wenzetu.mimi nadhani pengine wapewe wanachotaka.
 
Naunga mkono hoja,hakika wewe ni mzalendo,uchu wa uroho wa watu unahofia hili,mzigo wa serikali tatu haukubaliki hata kidogo mailings,serilali moja taifa moja


Mkuu, serikali ya Muungano inayopendekezwa ina mambo saba tu - ni ndogo sana. Haishughuliki na Hopitali, barabara, elimu nk. Fahamu hilo. Ina mambo machache kama uraia na uhamiaji, mambo ya nje, ulinzi, vyama vya siasa, Fedha na benki kuu na (Nimesahau 2)

Pili, hakuna aliyeleta mchanganuo wa serikali wa bajeti ya kuendesha serikali 2 vs serikali 3. No research no right to speak.
Kumbuka serikali iliyopo ina taasisi nyingis sana ambazo zinatakiwa kufutwa ili kuondoa dublication ya vyeo na kuongeza gharama bila ulazima wo wote Kwa mfano wakuu wa wilaya/mkoa nk. Ngazi ya Halmashauri kuna utitiri wa vyeo vya kuondoa. kWA HIYO, hili la gharama siyo hoja kwa sasa kwa kuwa hatuna aliyefanya utafiti.
 
Kwa nini viongozi wa CCM wanang'ang'ania muungano?
Hii kitu nimekua nikijiuliza tena na tena bila kupata majawabu. Pengine hawataki ku admit kuwa walifanya makosa huko awali!!...lakini kosa siyo dhambi. Hata dhambi tunaamini inasamehewa. Sasa sababu ni nini? Na hili jina Tanganyika kwa nini hawataki kulisikia?

Back to topic,
Mtoto akililia wembe mwache. Akishajua matumizi yake atauacha mwenyewe....when it is too late.

Eti tutapata misaada toka arabuni. Eti Zenji kuwa kama Dubai, na kadhalika, na kadhalika, na kadhalika.

Kuna mtu anaweza kuacha kujiendeleza yeye badala yake afikirie kukuendeleza wewe, mtu baki..? For free?? Hivi hakuna wanachama wengine wa OIC? Hadi sasa wamefaidika na nini?
Tungejifunza kutoka kwao.

But, waacheni waende jamani. Tunawanyonya!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…