Muundo wa Muungano: Tanganyika tunataka 'Serikali moja, nchi moja, taifa moja'!

Muundo wa Muungano: Tanganyika tunataka 'Serikali moja, nchi moja, taifa moja'!

Sasa wewe unaleta mambo ya rais wa Malawi ya outdated Heligoland treaty. Tanganyika inafahamika mipaka yake. Zanzibar ni visiwa vya Unguja na Pemba. This is also known.


Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
Hilo la Malawi limeisha? Kama bado kwa nini Zanzibar wasidai mipaka ya enzi za Utawala wa Sultani na hasa Mtwara, Bagamoyo na Dar es Salaam?
 
Nakubaliana na Mwanakijiji, tunataka serikali moja tu. Kama hilo haliwezekani, tuiache Zanzibar, tukutane nao kwenye East Africa Community.

Nadhani sasa umefika wakati wa kuwaacha Wanzanzibar wadai nchi yao wenyewe. Hata sisi Watanganyika tunataka nchi yetu, full stop. Hatutaki muungano...
 
rasimu hii sijui warioba alijifungia chumbani na mkewe akaitunga au alizingatia maoni yetu? kifupi hii rasimu ni upuuzi na ushuzi wa warioba sio maoni ya wananchi.
Kwa kweli tokea siku ilipotolewa nilipitia faster na kubaini hayahaya uliyoyasema, hata Tuko alisimama kidete sana kubainisha madudu ya Rasimu hii ilipokuwa ikitangazwa ajabu kuna watu walikuwa wakimuona mwehu. Siamini kama hii tume ilizunguka nchi nzima na kwamba hayo ndiyo mapendekezo ya wananchi, ni kama wamejifungia na kuandika wanavyotaka wao, kwani kila hoja waliyoitoa haina justification yoyote. Jimbo moja wabunge wawili wa jinsia tofauti(kwani tunataka waoane?)! Mambo ya Muungano saba, mawaziri 15, vichekesho; Manaibu waziri kutamkwa katika Katiba? vichekesho maana yake nini kwamba wizara kuwa na wajumbe wawili wa Baraza la Mawaziri? Uhuni. Serikali tatu lakini hakuna mapendekezo ya hizo serikali ziweje, na ziongozwe vipi; yaani wamezunguka nchi nzima wamekuja na mapendekezo ya kurekebisha muungano uliopo? Kwa kifupi wamefanya as if ni Tume ya Kurekebisha Muundo wa Muungano. Sioni majibu ya matatizo na vilio vya watanzania
CC: Tuko
 
Kifungu cha maraisi katika rasimu ya katiba yetu inanakera sana.Tutakuwa na maraisi wangapi?Ingekuwa vizuri kama tungekuwa na rais mmoja tu na nchi ya Tanganyika na Zanzibar zingeendeshwa na Mawaziri Viongozi kwa kimombo Chief Ministers
 
Kwa kweli ni upuuzi; as a matter of fact ni kana kwamba hawajui hesabu za seti! Hivi Mbunge mwanamke atakuwa anawakilisha wanawake tu kwenye hilo jimbo na Mwanaume atawakilisha wanaume watupu?

Tulianza na viti maalum kwa muda wa miaka kama kumi na tano hivi. Nia ikiwa kumnanyua mwanamke (affirmative actions); Natumaini sasa hivi wamama na wababa wanaweza kusimama na kunadi sera zao bila kuangalia mfumo jike au mfuko dume!

Genius Warioba na kundi lake wanakuja kinamna na kutengeneza aina nyingine ya viti maalumu. Jaribu kuangalia mfano, mbunge mwanamke anaweza kugombea na mbunge mwanamume na akashinda kisha kuna mbunge mwanamke anatakiwa agombee na mwanamke mwenzake kwa hiyo hilo jimbo linakuwa na wabunge wanawake wawili. Ulimwengu wa kisiasa Tanzania umebadilika na hilo wazo la kuwa na 'viti maalum' limepitwa na wakati. Ni kuongeza mzigo tu kwa watanzania.
 
hujaisoma rasimu wewe. Usikurupuke nawe uonekane umeweka post.
 
Kifungu cha maraisi katika rasimu ya katiba yetu inanakera sana.Tutakuwa na maraisi wangapi?Ingekuwa vizuri kama tungekuwa na rais mmoja tu na nchi ya Tanganyika na Zanzibar zingeendeshwa na Mawaziri Viongozi kwa kimombo Chief Ministers

ni vigumu kumtenganisha mtu mweusi na madaraka/mamlaka! km ilivyo vigumu kumtenganisha shetani na dhambi!
 
Hiyo Serikali ya Tanganyika ikipatikana ule ukanda wa Pwani uliokuwa chini ya himaya ya Waarabu ikiwemo Bagamoyo na DSM itakuwa sehemu ya Tanganyika yetu au Zanzibar? King of Zamunda
Mlivyooana mlipokutana ndivyo mtakavyoelekea mtakapoachana. Halihitaji kuuumiza kichwa hili
 
Hukutoa maoni yako nini kifanyike notradamme
maoni yangu ni kinyume kabisa na MWANAKIJIJI.. serikali ni jambo lisilokubalika kabisa mbele ya macho ya wazanzibari.
imagine!!! hizi serikali mbili mfumo ambao unawapa baadhi ya vitu vinavyowatambulisha kama taifa wanaukataa, je ukija mfumo wa serikali moja tu ambao utawapokonya hata hiki kidogo walichonacho itakuwaje?????? tafakari tafadhali.
naunga mkono hoja ya serikali mbili kama ilivyo sasa na kama sivyo labda serikali tatu kama yalivyo mapendekezo ya tume. huo ndio ushauri na maoni yangu
 
Kuna suala la kukinzana kwenye hiyo Rasimu, sehemu mojawapo jamaa wanataja ' Jamuhuri ya Tanganyika' na sehemu nyingine wanataja ' Tanzania Bara' kwa nini tume inakuwa very sensitive inapokwepesha neno 'Tanzania Visiwani' na kuendelea kulinda neno 'Zanzibar'?
 
Mimi tangu shule ya msingi hadi leo sijaeleweshwa umuhimu wa muungano kwa pande zote mbili - siujui. Muungano kwa jinsi ulivyo una maana ya Changu ni changu peke yangu (Zbar) ile chako (Tanganyika) ni chetu sote (Zbar na Tanganyika). Hii siyo sawa. Bahati nzuri sana wazanzibar ambao Muungano ni wa wote yaani wana haki bara na visiwani ktk mambo mengi ya muungano ndo hao hao wanaodai kujitenga. Sisi wabara au watanganyika tunahofu nini kujitenga au kuunda serikali tatu. Hii ndo maana napenda sera ya Chadema kuhusu Muungano. Wanataka serikali tatu.
 
sawa....lakini why rely on getting results by default rather than structuring it in the first place?

the point is....let's do a correct thing the first time. tuamue sasa tunataka kuwa na serikali ngapi badala ya kusubiri idadi ya serikali kupatikana by default!
Heko, yaani uwe unajua 2+2=4, lakini unaweka 3 kwa makusudi ili upate nafasi ya kufanya tena swali hilohilo? Haiwezekani,
 
mpango wa serkal 3 n ndoto za mchana


Mkuu ni ama tuwe na serkali tatu au tuuvunje muungano. Hofu ya kuvunja Muungano ni nini? Na kwanini hofu hii inawakumba wabara peke yao ni siyo wazanzibar? Kwa nini tunawabania wanzanzibar ambao wanadhani kuna neema zaidi endapo watajitenga? Kwa nini wazbar wawe chini ya ukoloni wa wabara? Kwa maani yangu tuwape wanzanzibar fursa wanayoitaka.
Pili, Pendekezo lenyewe la Rasimu hii ina usanii ndani yake. Wanasema nchi washirika zitaruhusiwa kukopa kutoka mashirika au nchi za nje baada ya kuwasiliana na serikali ya Muungano. Wewe unaona hapa kuna muungano au usanii tu. Nadhani huko mbele kuna utata zaidi.
 
Kasheshe baba cdm mama ccm halafu wote wabunge wa jimbo moja hebu angalia picha itakuwaje nilipoisoma hii rasimu nikaona inatoka manyema fc
 
Mimi tangu shule ya msingi hadi leo sijaeleweshwa umuhimu wa muungano kwa pande zote mbili - siujui. Muungano kwa jinsi ulivyo una maana ya Changu ni changu peke yangu (Zbar) ile chako (Tanganyika) ni chetu sote (Zbar na Tanganyika). Hii siyo sawa. Bahati nzuri sana wazanzibar ambao Muungano ni wa wote yaani wana haki bara na visiwani ktk mambo mengi ya muungano ndo hao hao wanaodai kujitenga. Sisi wabara au watanganyika tunahofu nini kujitenga au kuunda serikali tatu. Hii ndo maana napenda sera ya Chadema kuhusu Muungano. Wanataka serikali tatu.

...Nakubaliana na hoja zako hapo juu, lakini siamini kuwa serikali tatu ndiyo jibu la hayo, hapana, Serikali tatu siyo jibu lakini ni hatua muhimu kuelekea kwenye jibu lenyewe, yaan Serikali Moja ya Jamhuri ya Tanganyika. Nadhani mtu yeyote makini anayetaka kugombea urais uchaguzi ujao atachagua kugombea Urais wa Tanganyika kuliko ule wa Tanzania, maana si muda mrefu baada ya uchaguzi huo Rais wa Tanzania hatakuwa na kazi, wait and see...
 
Kuna suala la kukinzana kwenye hiyo Rasimu, sehemu mojawapo jamaa wanataja ' Jamuhuri ya Tanganyika' na sehemu nyingine wanataja ' Tanzania Bara' kwa nini tume inakuwa very sensitive inapokwepesha neno 'Tanzania Visiwani' na kuendelea kulinda neno 'Zanzibar'?

Hili nalo ni neno. Sisi tutakuwa na serikali ya Tanganyika wao ya zanzibar. Au Tanzania Bara na Tanzania visiwani au sote wawili tuwe na serikali ya Zanzibar na ya Tanganyika sawia. Vinginevyo ni usanii tu tusioutaka.
 
MwanaKijiji uko sahihi kabisa. Kama tunataka Muungano, tuwe na serikali moja na states kama ulivyopendekeza.
 
Rais wa Muungano atakuwa a very weak president katika kutenda kazi. Katika mfumo wa serikali tatu Tanganyika itaweza kufanya mambo mengi makubwa ambayo yatadhoofisha sana Rais wa Muungano hasa kama itatokea kuwa atakuwa ni Rais kutoka Zanzibar. Zanzibar itaona inazidiwa nguvu kubwa sana na Tanganyika. This is so obvious unless - Kuigawa Tanzania bara katika majimbo mengine ambayo nayo yatajitegemea...

Ndio maana mimi nadhani Rais wa muungano asiwe mkuu wa serikali. Awe tu mkuu wa nchi tumuachie mambo ya muungano and other ceremonial amenities. Kwa muundo uliomo kwenye rasmu haiwezekani akafanya kazi ipasavyo bila mgongano na Rais wa Tanganyika. The best scenario (close to ideal) ni unakuwa na Rais wa Jamhuri na mawaziri wakuu wa Tanganyika na Zanzibar. Mawaziri wakuu wanakuwa wakuu wa serikali na Rais anakuwa mkuu wa nchi. Kwenye uchaguzi tunachagua vyama. Chama kinachopata wabunge wengi kinaunda serikali. Lakini najua hii model wazanzibari hawaitaki kwa sababu kimsingi hawa wenzetu hawataki muungano.
 
I agree with you Mzee Mwanakijiji mzigo wa kuendesha hizi unatushinda elimu duni afya duni huduma duni yote hii ni uhaba wa fedha sasa serikali tati tena jamani hii tuseme hapana tuungane na ccm kuukataa

I disagree with you and mwanakijiji,

Mosi, hili la gharama siyo sahihi. Sasa tunajumla ya mawaziri karibu 60. Tukiwa na mawaziri kumi kwa mujibu wa rasimu hawazidi 15 tutakuwa tumeokoa Tsh ngapi kutokana na idadi hiyo ya mawaziri waliopungua? Gharama za ofisi hizo, magari, manaibu mawaziri, makatibu na manaibu, makamishna nk nk!!

Tukifuta nafasi za wakuu wa wilaya/mikoa tukatakuwa tumeokoa Tsh ngapi? Tukifuta ofisi ya Msajili Tfda inayogongana kila siku TBS, tukiunganisha mifuko yote ya hifadhi ya jamii nk tutakuwa tumeokoa Tsh ngapi?

Tukikusanya kodi seriously ktk maeneo yote muhimu mfano Tigo pesa na Mpesa hawalipi kodi Ipasavyo wajua hilo.
Misamaha ya kodi kwenye madini inayochimbwa nchi ni zaidi ya 10%, walijua hilo?

Kwa hiyo,
Siamini kwamba serikali tatu itakuwa na tofauti kubwa ya kuongeza mzigo wa waarijiriwa ktk serikali hizo. Kuna nafasi nyingi za kufuta ambazo zimeongezwa kizembe tu.
Pili, tukikusanya kodi vizuri tunaweza kupata fedha ya kutosha kujiendeleza na kuendesha serikali tatu. Tuache hofu isiyo na msingi. Naunga mkono sera ya chadema kuhusu Muungano = serikali tatu au tuuvunje muungano kama 3 tumeshindwa.
 
Back
Top Bottom