I agree with you
Mzee Mwanakijiji mzigo wa kuendesha hizi unatushinda elimu duni afya duni huduma duni yote hii ni uhaba wa fedha sasa serikali tati tena jamani hii tuseme hapana tuungane na ccm kuukataa
I disagree with you and mwanakijiji,
Mosi, hili la gharama siyo sahihi. Sasa tunajumla ya mawaziri karibu 60. Tukiwa na mawaziri kumi kwa mujibu wa rasimu hawazidi 15 tutakuwa tumeokoa Tsh ngapi kutokana na idadi hiyo ya mawaziri waliopungua? Gharama za ofisi hizo, magari, manaibu mawaziri, makatibu na manaibu, makamishna nk nk!!
Tukifuta nafasi za wakuu wa wilaya/mikoa tukatakuwa tumeokoa Tsh ngapi? Tukifuta ofisi ya Msajili Tfda inayogongana kila siku TBS, tukiunganisha mifuko yote ya hifadhi ya jamii nk tutakuwa tumeokoa Tsh ngapi?
Tukikusanya kodi seriously ktk maeneo yote muhimu mfano Tigo pesa na Mpesa hawalipi kodi Ipasavyo wajua hilo.
Misamaha ya kodi kwenye madini inayochimbwa nchi ni zaidi ya 10%, walijua hilo?
Kwa hiyo,
Siamini kwamba serikali tatu itakuwa na tofauti kubwa ya kuongeza mzigo wa waarijiriwa ktk serikali hizo. Kuna nafasi nyingi za kufuta ambazo zimeongezwa kizembe tu.
Pili, tukikusanya kodi vizuri tunaweza kupata fedha ya kutosha kujiendeleza na kuendesha serikali tatu. Tuache hofu isiyo na msingi. Naunga mkono sera ya chadema kuhusu Muungano = serikali tatu au tuuvunje muungano kama 3 tumeshindwa.