Muundo wa Muungano: Tanganyika tunataka 'Serikali moja, nchi moja, taifa moja'!



Hoja imefika lakini mbona ndugu yangu hoja yako umeijenga katika mambo mengine yasiyokuwa ya kweli?
zanzibar ikiwa na serikali kamili ndiyo ya kuonewa huruma kwani inajukumu la kuwaendeleza na kuwahudumia watu wake kwa yale yanayoambiwa si ya muungano na baadae kuja kuchangia katika jungu kubwa ambalo sehemu kubwa inaliwa na walio wengi na ambao matumizi yao hayatenganishi baina ya walichozalisha wao au wenzao.
Hili la kutotafautisha baina ya kipato na matumizi ya pamoja na yale ya Tanganyika pekee ndio hufanya wazanzibari wawepo bungeni ambako hayo matumizi hufanywa. Kule zanzibar matumizi yanayopangwa na wawakilishi ni ya zanzibar peke yake sasa hiyo haja ya kuwaleta watu wasiohusika ya nini?
Hata hivyo nakubaliana nawe kuwa hakuna uwazi na hili lazima lilete manunguniko, na dawa yake ni rahisi tu, tuchukue mfano wa zanzibar wa kuwa na serikali yake na hivyo Watanganyika watajuwa nini wanachuma na nini wanatumia kwa serikali yao na kama tunahitaji tuwe na mambo fulani ya pamoja basi tufanye donation kwa mujibu wa tumbo la mtu na anavyokula!
 
sio rahisi kuwatawala wa huku Bara, lakini wazanzibari ilikuwa rahisi. kwani kinaogopwa nini serikali tatu? Huko ndio tutakojuwa maana ya kuungana na faida zake na ni rahisi kuamuwa basi iwapo hakuna faida. Baadhi ya wazenji wanataka mkataba ,jamani hamuoni hilo ni wazo zuri zaidi kwa dunia yetu ya leo?
 
muungano wa kisawa ni huu hapo chini.. sote kwa pamoja washirika wa muungano tunaongoza jeshi letu.. sote kwa pamoja tunaongoza nchi.. yako wapi leo hii... liliobakia sasa kwa sisi wana wa kizanzibari ni kuendelea kudai cha kwetuna kuwaelimisha tanganyikaz.. mlikua mnatuona machizi but now mpo kila mahala mnajadili tuloanzisha na kuendeleza sisi wazanzibari.. mnaona eihhhhh.. nyote sasa mnajadili hii kitu muungano.. angalia picha hiyoangalia step zote.. nani kamzidi mwenzake hapo.. huo ulikua usAWA.. SASA LEO IWEJE KUJIFANYA KAMIZINGA MNATAKA MPIGIWE NYINYI TUUUU NA MNAUMIA MZENJ AKIPIGIWA.. AKILI NDOGO HIZO KUTOKA KWA WASEMAJI WENU BUT IT IS WHAT IT IS.. TUKO IMARAA WAZANZIBARI TUNASONGA MBELE.. MTATUFATA TUU KUDAI CHA KWENU...
 
Binafsi huwa mara nyingi naamini muungano ni kitu kizuri, lakini nina mashaka makubwa kama nchi zetu hizi za Tanganyika na Zanzibar zimefikia hatua ya kudeal na mambo mazito tena na ambayo ni optional i.e muungano.

Kwa hatua tuliopo katika na kama kweli tuna viongozi wasio na ubinafsi wenye kutazama na kujua jinsi ya kueka priorities, basi muungano ni suala ambalo linatakiwa liondoke kabisa katika mawazo ya wananchi.Tunatakiwa tujikite zaidi katika kuboresha standard of living na kuimarisha uchumi na kuwa nchi zenye kujitegemea.

Shortly nashauri kukagawana mbawa!
 


Mkuu!
1+1=1 ndio jibu sahihi.Hii inawezekana kwani pakiwepo na mawaziri wakuu wawili
watakaochaguliwa na wananchi/Rais awe na makamu wawili
watakaojulikana kama mawaziri wakuu mmoja kutoka Zanzibar na mwingine kutoka Tanganyika.
 
Mkuu!
1+1=1 ndio jibu sahihi.Hii inawezekana kwani pakiwepo na mawaziri wakuu wawili
watakaochaguliwa na wananchi/Rais awe na makamu wawili
watakaojulikana kama mawaziri wakuu mmoja kutoka Zanzibar na mwingine kutoka Tanganyika.

nakubaliana na wewe mkuu robert josephat

lakini nchi iwe kama ifuatavo

JINA : ZANZIBAR

CAPITAL CITY: ZANZIBAR TOWN

AGREEMENT: MUST BE 100 YEARS

MINISTERS: 50/50 TANGANYIKA/ZANZIBAR

F. EMBASSIES: MUST BE IN ZANZIBAR

ALL GOVERNMENTAL INSTITUTIONS: HQ IN ZANZIBAR

CENTRAL BANK: MUST BE IN ZANZIBAR

UHUAMIAJI: MAKAO MAKUU ZNZ

POLISI, JESHI, NAVY U NAME IT
 
Ukitaka kuwatibu waZanzibar waambie swala muungano wa serikali moja
Hatakuelewa kamwe
 
Ukitaka kuwatibu waZanzibar waambie swala muungano wa serikali moja
Hatakuelewa kamwe

Na ukitaka kuwatibua wadanganyika waambie zanzbr iwe huru,wanaweza kukuwa.
 

Hata mimi nakuunga mkono ndugu ni bora kila nchi ikabaki kivyake kuliko kuendelea kutupigia kelele humu janvini. Kwani undugu wetu utaendelea kuwepo.
 
Watanzania waishio Mtwara imesemwa waeliweshwe kuhusu umuhimu wa kusafirisha gesi kutoka Mtwara kwa bomba kuelekea Dar es Salaam. Swali ninalouliza nguvu hiyo ya uelimishaji kwa nini pia isielekezwe kwa watanzania wanaoishi Zanzibar ili wakubali tuwe na serikali moja?
 

Acha kupotosha umma, USA kuna serikali 51! Yaani serikali za majimbo 50 zinazo ongozwa na magavana waliochaguliwa na wananchi kwa kura, na kuna serikali kuu ya shilikisho inayo ongozwa na Obama. Kila jimbo lina sheria zake, polisi wake, mahakama zake nk. Serikali 3 ni jibu la matatizo ya muungano.
 
Nilikuwa ndotoni. Nikaona watanzania wanaunda serikali tatu 2014. Katika ndoto hiyo nikaonaona ghafla baada ya serikali hizo tatu kuundwa Wazanzibari na Watanganyika wanajitizama na kujishangaa. Na mara wanaanza kudai katiba mpya tena ili kufanya muungano wa serikali moja. Mara ninaamka. Naitafakari ndoto yangu. Ndiyo, natamani ndoto yangu itimie katika siku chache, kabla sijafa!
 
kwani unakufa lini?...usisahau ukiota na kuona ndoto haitimii "unatakiwa urudi kulala kuitimiza ndoto yako"
 
kwani unakufa lini?...usisahau ukiota na kuona ndoto haitimii "unatakiwa urudi kulala kuitimiza ndoto yako"

nakadiria kufa kwangu kutakuwa kati ya leo na miaka 50 ijayo. Siwezi kurudi kulala kwa kuwa ndoto yangu haijatimia. Nitaendelea kusubiri itimie, nina matumaini itatimia kabla sijafa.
 
Umeota mchana.

Hapana sioti mchana, niliota usiku na nilipoamka majukumu yakanitinga, sasa ndiyo nimepata nafasi kidogo ya kuweza kuwashirikisha wenzangu hii ndoto yangu ambayo nadhani ndani yake kunaweza kuwa na unabii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…