Muundo wa Muungano: Tanganyika tunataka 'Serikali moja, nchi moja, taifa moja'!

Ukifa kabla ya kuona serikali mmoja mpe salaam Mwalimu Nyerere mkumbushe hii sentensi "Watu wazima mnazungumzia serikali tatu maskini kabisa nyie! wakati wazungu wanazungumzia kuunganisha ulaya moja yenye nguvu"
 
Niliona katika ndoto yangu nchi za jiarani zikiingalia Tanzania kwa namna ya kutaka iwe na serikali moja kwanza ndipo wajiunge nayo kufanya nchi kubwa sana yenye nguvu. Nikaona mataifa ya magharibi yakichukia!
 
Niliona katika ndoto yangu nchi zz jiarani zikiingalia Tanzania kwa namna ya kutaka iwe na serikali moja kwanza ndipo wajiunge nayo kufanya nchi kubwa sana yenye nguvu. Nikaona mataifa ya magharibi yakichukia!
Hakuna Tanzania kama hakuna muungano!! kuna Tanganyika na Zanzibar..serikali moja unayoota ni ya nchi gani kati ya hizi mbili?
 
Na tazama nikaona.....angalia usijekuta unakaribia kutoa kitabu chako cha ufunuo wa kakati.
 
najiuliza tu ZANZIBAR wakiwa na NEC yao...mpaka ma kantupe yatagraduate
 
Hakuna Tanzania kama hakuna muungano!! kuna Tanganyika na Zanzibar..serikali moja unayoota ni ya nchi gani kati ya hizi mbili?

Kweli hakuna Tanzania bila muungano. Tanzania ipo kwa kuwa muungano upo na pia Tanzania itakuwepo hata tukiwa na serikali tatu. Tanzania itakuwa halisi zaidi itakapoanzishwa serikali moja. Yaani ndoto yangu itakapotimia.
 
Na tazama nikaona.....angalia usijekuta unakaribia kutoa kitabu chako cha ufunuo wa kakati.

Na hapo watasema ... ufunuo wa Kakati wa serikali moja ya Tanzania imetimia na hapo watu wataona nguvu kubwa itakayorudisha nafasi ya afrika ulimwenguni
 
Kesho ukiota ndoto uko na yule Profesa wa ccm usiache kutuandikia.
 
Wale wote wanaotaka Tanzania tuwe na serikali Moja yenye kufuata Mfumo wa kuwa na serikali za kimajimbo TUUNGANE na tuifikishe hoja yetu hiyo kwa wananchi kama ndiyo njia pekee ya kuuokoa Muungano wetu. Unguja na Pemba zitakuwa na serikali zao za ndani za kimajimbo na kwa Upande wa Tanganyika majimbo yatagawanywa kwa kufuata mapendekezo yatakayotolewa na wananchi wenyewe.
 
unachofikiria ni sawa na mtoto kulilia mwezi
 
Wale wote wanaotaka Tanzania tuwe na serikali Moja yenye kufuata Mfumo wa kuwa na serikali za kimajimbo TUUNGANE na tuifikishe hoja yetu hiyo kwa wananchi kama ndiyo njia pekee ya kuuokoa Muungano wetu. Unguja na Pemba zitakuwa na serikali zao za ndani za kimajimbo na kwa Upande wa Tanganyika majimbo yatagawanywa kwa kufuata mapendekezo yatakayotolewa na wananchi wenyewe.

Kigarama kwa nini wewe sio miongoni mwa wanaotakiwa kuheshimu mawazo ya Watanzania????Tujifunze kuheshimu mawazo ya walio wengi,,,wahenga walisema MKATAA WENGI NI MCHAWI...Wananchi wanataka Serikali tatu..Tuheshimu mawazo yao
 
Kuheshimu mawazo ya wengine kutakuja pale tutakapopiga kura ya maoni kuamua ni mfumo gani utuongoze huko tuendako!! Kwa sasa kila mtu anaruhusiwa kuleta ushawishi wake!!
 
Sisi wazenji hatutaki jaribuni kuwaomba majirani zenu muungane hivyo mfano Kenya ,Uganda,Zambia,Malawi n.k
 
Kwa mtazamo wangu watanzania tunahitaji muungano wa serikali moja, yaani Zanzibar na bara zote zikubali kusurrender autonomy zake kwa serikali na nchi moja tu ya Tanzania. Nionavyo mimi, serikali mbili ama tatu zitaturudisha kulekule kwenye matatizo ambayo tunapaswa kuyakimbia tena kwa speed ya 250km/h.

Serikali mbili zitaendeleza migogoro na mivutano ileile ambayo tulishaichoka.

Serikali tatu ndo balaa, yaani muundo huu ni sawa na mwanaume aliyeshindwa ndoa ya wake wawili kisha akaamua kuongeza mke mwingine. Kiukweli muundo huu utatugharimu. Kiusalama kwa mfano, nchi washirika wakigoma kuziwezesha wizara zenye dhamana ya usalama nchi imekwisha!, marais wa nchi washirika wakiamua kuuhujumu muungano ni rahisi sana kwenye serikali tatu. Inshort miungano ya serikali mbili au tatu haifai!

Kama ni hivyo basi, dawa ni muungano wa serikali moja. Faida yake kubwa ni kwamba itaimarisha utaifa wetu haijawahi tokea. Pili itaondoa malalamiko ya kila upande wa muungano kuona unakandamizwa na upande mwingine. Kubwa zaidi itatuongezea nguvu mbele ya maadui kwani "umoja ni nguvu"
 
  • Thanks
Reactions: ELX
wachaw wetu ni wanasiasa,,hili suala la muungano walilidandia kwa maslah yao kisiasa..nani sa hv atakusikiliza ndug yang wakat serikal 2 ilishapitishwa zaman,,Dodoma wapo ushahid tu
 
Tanganyika tuli surrender sovereignty yetu wakati wa serikali 2 hadi Zanzbar walipodai yao na kukubaliwa kubadilisha katiba yao, sasa basi! Kama ni noma na iwe noma, Tanganyika irudi kwani hata bila muungano inatutosha!
 
Kwa mtazamo wangu watanzania tunahitaji muungano wa serikali moja, yaani Zanzibar na bara zote zikubali kusurrender autonomy zake kwa serikali na nchi moja tu ya Tanzania. Nionavyo mimi, serikali mbili ama tatu zitaturudisha kulekule kwenye matatizo ambayo tunapaswa kuyakimbia tena kwa speed ya 250km/h.

Serikali mbili zitaendeleza migogoro na mivutano ileile ambayo tulishaichoka.

Serikali tatu ndo balaa, yaani muundo huu ni sawa na mwanaume aliyeshindwa ndoa ya wake wawili kisha akaamua kuongeza mke mwingine. Kiukweli muundo huu utatugharimu. Kiusalama kwa mfano, nchi washirika wakigoma kuziwezesha wizara zenye dhamana ya usalama nchi imekwisha!, marais wa nchi washirika wakiamua kuuhujumu muungano ni rahisi sana kwenye serikali tatu. Inshort miungano ya serikali mbili au tatu haifai!

Kama ni hivyo basi, dawa ni muungano wa serikali moja. Faida yake kubwa ni kwamba itaimarisha utaifa wetu haijawahi tokea. Pili itaondoa malalamiko ya kila upande wa muungano kuona unakandamizwa na upande mwingine. Kubwa zaidi itatuongezea nguvu mbele ya maadui kwani "umoja ni nguvu"

Mmmh, hayo wezako kule Unguja hawataki kusikia jambo hilo. Serikali3 ni busara tu ya Wananchi, hasa ilitakiwa 1, mbili nayo haitakiwi
 
Wazo lako mtoa mada nadhani uliliwaza wakati wa haja kubwa chooni,sikia,zanzbr kumezwa total na mkoloni mweusi kupitia muungano imeshindikana,na kama mnataka kulazimisha kuimeza itawakwama kwenye koo,jaribu kuuliza kwa nn nyerere ilimshinda kuimeza zanzibr,ukoloni mweusi ndio utakao surrunder na lazima itaitema zanzbr,kama tanzania ilizaliwa 1964 basi na mwaka wake wa kufa upo,zanzbar kwanza.
 
Back
Top Bottom