Kwa mtazamo wangu watanzania tunahitaji muungano wa serikali moja, yaani Zanzibar na bara zote zikubali kusurrender autonomy zake kwa serikali na nchi moja tu ya Tanzania. Nionavyo mimi, serikali mbili ama tatu zitaturudisha kulekule kwenye matatizo ambayo tunapaswa kuyakimbia tena kwa speed ya 250km/h.
Serikali mbili zitaendeleza migogoro na mivutano ileile ambayo tulishaichoka.
Serikali tatu ndo balaa, yaani muundo huu ni sawa na mwanaume aliyeshindwa ndoa ya wake wawili kisha akaamua kuongeza mke mwingine. Kiukweli muundo huu utatugharimu. Kiusalama kwa mfano, nchi washirika wakigoma kuziwezesha wizara zenye dhamana ya usalama nchi imekwisha!, marais wa nchi washirika wakiamua kuuhujumu muungano ni rahisi sana kwenye serikali tatu. Inshort miungano ya serikali mbili au tatu haifai!
Kama ni hivyo basi, dawa ni muungano wa serikali moja. Faida yake kubwa ni kwamba itaimarisha utaifa wetu haijawahi tokea. Pili itaondoa malalamiko ya kila upande wa muungano kuona unakandamizwa na upande mwingine. Kubwa zaidi itatuongezea nguvu mbele ya maadui kwani "umoja ni nguvu"