fikirikwanza
JF-Expert Member
- Jan 25, 2012
- 7,452
- 3,071
HUU NDO UKWELI, NCHI MOJA SERIKALI MOJA, kama Zanzibar hawataki maana ni rahisi sana kuwa hakuna muungano
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
serikali 1 ndo mpango mzima
Hahahaaa kwanza waondoke kwenye wizara zetu huku bara.
wabunge wa zanzibar inabidi waache kuja dodoma huu ni unyonyaji
Sioni kama hawa uliowataja hapa wanataka muungano uvunjike/uvunjwe.
Mimi nimeshajaribu kuonesha ni lazima tuirudishe serikali ya Tanganyika na jina Tanganyika kama hatua ya kumaliza mazingaombwe lakini kila wanapoandika wanasema "tuwasaidie wazanzibari wajitoe"
Rai niliyotoa mimi ni kuwa tutumie rai ya mwasisi wa Muungano ya kuunda EAF. Huko tupeleke timu mbili.Serikali ya Tanganyika kivyake na serikali ya Zanzibar kivyake. Hapo ni kuwa huu muungano wa kisanii unaisha na tunaanza na Muungano wa kikweli.
Hawa dugu zangu, wananiweka njia panda.wananiona mimi UAMSHO. Bila Tanganyika na serikali ya Tanganyika ni kuendelea na kiini macho halafu tunalalamika Tanganyika inapata hasara. Entity ambayo haipo inapata hasara vipi?
Hakuna kati ya hawa anayetaka serikali ya Tanganyika.
JokaKuu unasema Tanganyika imemezwa? Imemezwa na nani?
Kama jibu ni Muungano, Muungano ni baina ya nchi ipi na nchi ipi?
Ile ngao ya adam na hawa ni nembo ya serikali ipi? Ile katiba ya Muungano imepatikana vipi?
Mkuu Nguruvi3 anasema Tanganyika ni sleeping general....alalae usimwamshe....
Jamani watanganyika tuamke!
Ya tanganyika.
Mkuu Mzee Mwanakijiji, sijui wakati mwingine mimi ninakuwaga wapi?!, hii sikuiona ndio naiona leo!. Kumbukumbu yangu ya mwisho kwako kuhusu Zanzibar, ni ile let Zanzibar Go!.Tusikubali kwenda serikali tatu. Kwa vile tumekatazwa kutaka kuvunja Muungano - japo waliotukataza hawana uwezo huo - na kwamba tunaweza kujadili "muundo" bora wa Muungano. Ninawasihi watu wa bara kudai "Serikali moja, taifa moja, na nchi moja". Haya mambo ya serikali mbili nchi mbili au serikali tatu nchi mbili hayaingii kichwani na ni jitihada za kujaribu kuibeba Zanzibar. Wakati umefika tudai uwepo wa serikali moja tu ya kitafa kwenye nchi moja.
Ninafahamu kabisa matokeo ya watu wa bara kutaka hili. Jambo pekee ambalo tusikubali kuuziwa (CCM na upiinzani wanataka hili) ni serikali tatu. Serikali tatu ni mzigo ambao hatuwezi kuubeba na wala hatupaswi kuubeba. Nawasihi wenzangu tukate kuongezewa mizigo. Tuwe na serikali moja, taifa moja na nchi moja. Sasa kama hili lina maana Zanzibar iwe "serikali moja, taifa moja na nchi moja" na bara iwe "serikali moja, taifa moja na nchi moja" basi na iwe.
Tuwasaidie Zanzibar watoke kwenye Muungano kama hawataki serikali moja kwani mbili hawataki na tatu tutajipa mzigo zaidi!
SAY NO TO SERIKALI TATU!!
Iambie tume ya Warioba - hatutaki serikali tatu!!
Na wa Pwani nao wanadai serikali yao
Nitaendelea kuimba daima kwamba serikali moja ndio destination sahihi ambayo huu muungano ulipaswa kufikia,lakini katikati ya safari yetu kwenda huko,imejitokeza ukweli kwamba NI VIGUMU MNO KUWAUNGANISHA WATU WABINAFSI KUWA KITU KIMOJA.Kinachoendelea sasa ni revelations tu za ukweli huu.Lakini pia kuna ukweli mwingine ambao haujajitokeza bado kwa vile haujapata nafasi hiyo.Ukweli huo ni kwamba BINADAMU HAJAUMBWA AWE MBINAFSI.Kwa hiyo pale revelations za UBINAFSI zitakapotimia na UBINAFSI kutawala mifumo yote,hapo ndipo huu ukweli mwingine utapata nafasi ya kujitokeza na kutuonyesha kwamba HATUTAKIWI KUWA WABINAFSI.Wenye akili mmenielewa.