Muundo wa Muungano: Tanganyika tunataka 'Serikali moja, nchi moja, taifa moja'!

Muundo wa Muungano: Tanganyika tunataka 'Serikali moja, nchi moja, taifa moja'!

Hili la serikali tatu ni sawa kwa kuwa muda si muda tutakuwa na akina Yeltsin watakaowaacha akina Gorbachev bila nchi ya kutawala na hivyo Tanganyika kuwa nchi peke yake bila unyonyaji wa Zanzibar na Zinzibar kubakia peke yake bila unyonyaji wa Tanganyika. Juzi nimewasikia wakililia kiti chao UN basi tukimpata Yeltsin wetu nao watakuwa na kiti chao huko UN. Wacha zije lakini tatu hazitadumu.
Urusi iliposambalitika wengine wamechoka lakini Rusia imebaki Kuwa Tajiri hata ZNZ wakijitoa haitawaathili Bara sana sana Bara atakuwa tajiri kwa kuuza umeme zenji Ada za viza na vibali vya kuishi na kufanya kazi Bara kwani wazenji wote watakuwa Raia wa Nchi Jilani
 
rasimu hii sijui warioba alijifungia chumbani na mkewe akaitunga au alizingatia maoni yetu? kifupi hii rasimu ni upuuzi na ushuzi wa warioba sio maoni ya wananchi.

Kwa asilimia kubwa ni maoni Yao binafsi hususani la serikari tatu
 
Tuuvunje muungano hatuutaki zanzibar mmetunyonya vya kutosha!!
 
Ukweli Hakuna lisilowezekana tukiamua inawezakana sisi ni ndugu moja ya nini kuunda Maserikari kibao kwa Nchi changa Kama hii?Nchi inaitwa nchi ya Amani iweje imeshindwa kunitumia Amani kuwaunganisha wananchi wa Bara na Visiwani na Kuwa wamoja?kisha waunde serikari Moja imara kama ilivyokuwa kwa Ujerumani. Jamani tuachane na serikari tatu tujikite kuitengeneza serikari moja tu inatosha
 
Mimi nashangaa, sasa kama tumeungana Tanganyika na Zanziba hivi vipande vya serikali tatu vyatoka wapi?. Yaani kabla hatujaungana tunaserikali mbili, tukiungana serikali zinakuwa tatu! Hapa kuna mantiki kweli?.
 
sometimes sikuelewi Mwanakijiji... wewe ni mmoja wanaobwabwaja sana kuhusu zanzibar lakini huna idea inayosimama wima, unayumba kama shamba la mpunga tu

Hakuna haja ya muungano... PERIOD!
 
Tatizo lenu hamjielewi watanganyika,hebu jiulizeni kidogo tu,je kama inchi nyengine itatamani kujiunga na muungano huu je serekali zitakuwa ngap?
 
sometimes sikuelewi Mwanakijiji... wewe ni mmoja wanaobwabwaja sana kuhusu zanzibar lakini huna idea inayosimama wima, unayumba kama shamba la mpunga tu

Hakuna haja ya muungano... PERIOD!

Sawa sasa Zanzibar wanaweza kuondoka vipi?
 
Kama tutakuwa na serikali tatu, je uuzaji wa gesi (through pipeline) kati ya Tanzania bara na na nch jirani kama Kenya utakuwa chini ya usimamizi wa serikali gani?
 
Wenye nchi tunaamka sasa, liwalo na liwe, ni Tanzania Moja kwenda mbele, hatutaki 2 wala 4. ubarikiwe mwanajiji.
 
Kampeni hii wapigie watanganyika wenzako sio waz'br,waz'br ni mamlaka kamili ikifuatiwa na muungano wa mkataba na nchi yoyote sio lazima iwe tanganyika.
 
Rasimu kama inataka muungano uendelee wangebariki serikali za majimbo mawili. Tanganyika na Zanzibar yenye kuongozwa na magavana. Majimbo haya yakiwa chini ya Serikali kuu ya Tanzania. Yangeendesha serikali zao kamili. Lakini sasa upuuzi huu wa serikali3 zenye uwakilishi wa jinsi ya wabunge 50 kwa 20 ni matusi kwa watanganyika. Milioni 40 kwa milioni 1 Hawa Wazenji wana nini cha kuzidi kuwabeba. Hawatutaki tunauawa tukienda kule tunachomewa mali zetu. WAONDOKE wana MaBaba zao waarabu tunanufaika nini na hawa jamaa. Wanatubagua tunawalisha.
Waarabu hawana uwezo wa kuwapa cchochote bali hatimae watajifunza kujitoa muhanga tu ambayo ni ishara ya kukata tamaa. Tume imetoa rasimu inatia aibu mapendekezo mengine kama mwanamke tunamhesabu kuwa sawa kupat fursa sawa kwa nini apewe upendeleo mara zote. Wabunge wawili wawili mme/mke ni fedheha tume yenye wazee kama hawa. Namalizia hapo mtanyosha wadau
 
liwalo naliwe serikali moja,taifa moja,nchi moja,rais mmoja,huo ndo muungano

liwalo na liwe serikali tatu ama uvunjwe muungano.nchi zetu ni masikini kuungana kwao ni kuendeleza umasikini.
 
Sawa sasa Zanzibar wanaweza kuondoka vipi?

si tayari wako zanzibar?? wafanye referrendum yao, wafuate taratibu na wasikilizwe ili watoke... hakuna haja ya kukaa tunalumbana na kanchi kenye kelele wakati productivity hakuna


mimi naamini kabisa kama zanzibar wangekua na nia ya dhati ya kujiondoa kwenye muungano wangeweza, ila wameishia kupiga perepete ili tu wawe wanapata watakacho, ni kama mtu mwenye gubu

kuhusu serikali tatu, nadhani itasaidia zaidi ile transition ya kuanchana na zanzibar, tutakua na migogoro mingi mno kati ya hizo serikali tatu mwisho tutafanikiwa kutengana.... ni sawa na kusema ndoa ina matatizo basi ulete mama mkwe akae hapo ndani kutatua - NDIO HIYO SERIKALI YA TATU AMBAYO ITAKUA NA MAMLAKA YA KUSADIKIKA ZAIDI, I DONT MIND UKIRITIMBA IF THAT IS WHAT IT TAKES KUVUNJA MUUNGANO
 
Too late mkuu, boti lishaondoka bandarini!
Its the Zanzibaris who need convincing, and they wont buy this.
Na kwa upande wa waTanganyika we are almost fed up with them!
 
Naitaka Tanganyika yetu yenye maadili ya kiuongozi! Hizo sirikali tatu ni zao wao!
 
Mkuu Mwanakijiji,
Na hili hili la wabunge wawiliwawili (jinsia tofauti) kwa jimbo unalionaje? Mbona kwa wenzetu waliotutangulia kwenye maswala ya demokrasia hatujawahi kusikia upuuzi huu? Kituko tulicholetewa na Warioba hakilingani na gharama tulizowalipa.

Sintoshangaa nikisikia wananchi wanapendekeza zaidi kuwe na "marahisi" wawili mke na mume! na mawaziri wawiliwali wa kike na kiume, ni mwendo wa kuji-balance balance na kujipa nafasi, bila kufikiri mantiki yake ni nini.
Kwa ujumla mimi naona hio rasimu ni kichekesho kitupu hakuna chamaana kilichopendekezwa! Ni kama watu wametumbua posho kwa posho. Hivi hao wanasheria wame-practice wapi? Khaaa!
 
Back
Top Bottom