ZNZ ni kweli wanamtegemea Tz Bara kwani bila Bara kwao ni full njaa na fujo kwani ni walalamishi kupindukia hata wapewe nini hawaachi kulaamika hata wakijitenga Watagombana wenyewe kwa wenyewe Na hao waarabu wanaotaka kuludisha koloni watagombana tu kwani hawatavumilia ulalamishi toka kwa watu ambao wanawasaidia Na Ndoto ya Mafuta Pemba wakumbuke ipo na Bara Pia kwani Bara kuna Bahari kubwa sana Tokea Tanga hada Mtwara imejaa mafuta tele ZNZ watambue Kuwa wao watakuwa Raia wa Kigeni Bara pindi wakijitenga na itakula kwao kulipia viza na vibali vya kuishi na kufanya kazi Bara kinyume na hapo waishi Kama wakimbizi TZ Bara ni Nchi tajiri sana na wananchi wake si walalamishi sana Ndio Maana wana endelea kuwahudumia pasipo ubaguzi
Utajiri kweli mnao, na POPULATION kubwa mnayo. Na eneo kubwa la kigeographia mnalo, kwahiyo, mkumbuke ya kwamba hata kama unakipato kikubwa lkn familia ni kubwa mahitaji yatakuwa hayatoshelezi, ikisha kama nyinyi sio walalamishi mbona Nyerere alikataa kuunganika Africa nzima akadai tuanze regional. Kama haitoshi, uchumi mdogo wa zanzibar ikiwemo bandari kufifia ni sera maalum ya watanganyika. Mapato ya kodi plus vyanzo vya mapato vyote vya mambo ya muungano yaliyopo mwanzo na yaliyoongezwa kama vile misaada nk, yote huishia kwenye serikali ya muungano na matumizi yake hutumika kwenye mambo ya muungano na mambo yasiyo ya muungano ya tanganyika kwani Bajeti inajadiliwa pamoja, ambapo mambo ya muungano yanayokwenda zanzibar kama vile polisi jeshi nk, haifiki hata asilimia 10% ya pato la mambo ya muunganno linalotumika kwa ajili ya zanzibar. Hela nyengine yote inakwenda wapi?
Kuna misaada mingapi ilitakiwa ije zenjy, serikali ya muungano ilikataza? Ukija kwenye suala la Ajira, maeneo yote ya muungano karibu 28 walioajiriwa wengi ni watanganyika, kwahiyo basi kama hayo yote yatatoa ajira kwa wazanzibari wenyewe, huoni kama wazanzibari wote watakuwa na ajira? Kwa mfano elimu ya juu, ni wazanzibari wangapi wanaosoma Tz bara, na wangapi wa tanganyika? Kwaiyo na nyinyi mtabeba mzigo wenu wenyewe.
Kwa kuhitimisha, toeni bandari, mambo ya nje, sarafu na uhamiaji viwe tanganyika pale na zanzibar pake baada ya miaka miwili tuje tufanye tathmini uchumi wa nani umekuwa?!!
Tanganyika hamtaki kupumua kwani?